matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 6,586
- 15,370
kuna msemo wa kirumi Vox Populi Vox dei ( Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu).
Huu msemo ni sahihi kisiasa sio kidini au kiimani. Wanasiasa walitumia huu msemo kujihalalishia mambo yao hata kinyume cha Mungu na wengine ilikula kwao. Sasa ni aibu kwa kauli hii kusikika kwa watu wa dini. Ibaki kutumika katika mimbari ya kisiasa sio dinini.
Ushahidi
Nebukadneza Sauti ya wengi ilimjaza na akajiona mungu. Mungu alimpa adhabu ya kuishi porini na wanyama miaka saba hadi kiburi kiliposhuka.
Sauti ya wengi ndio ilimkataa Samweli aloyetumwa na Mungu, na kutaka waisrael watawaliwe kama mataifa mengine kisiasa.
Sauti ya Wengi ingekuwa ya Mungu, basi Nuhu na familia yake ndio wangekufa kwa mafuriko huku wengi wakiokolewa na safina.
Sauti ya wengi ya kumsifu Herode ilimsabajishia apigwe na chango akafia kwenye mimbari za kisiasa huku waliomsifu wamemkimbia.
Wengi waliwahi kusema afunguliwe jambazi Baraba na asurubiwe Yesu Yusuph aliyewafufulia watoto wao na kuwatoa mapepo yaliyowatesa.
Sauti ya wengi ni sauti ya hao wengi sio lazima iwe sauti ya Mungu. Linaweza kuwa kundi la wengi waliopotoshwa au wenye maslahi jifichi kwa kumpakazia Mungu kuwa sauti zao ni sauti yake.
Ni hayo tu waungwana.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki afrika kusini mwa jangwa la sahara.