Mvutano: Ni kwanini Mungu alimruhusu mwanaume kuweza kuwa na mke zaidi ya moja kwenye biblia lakini makanisa yamekataza?

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,080
Hakuna sehemu yoyote ambayo Mungu alikataza hata manabii ama wafame waliomtumikia kuoa mke zaidi ya moja, ukimya wake katika jambo hili ni sawa na sisi wazazi tunapoona mtoto anafanya mambo kwa usahihi tunakuwa hatuna haja ya kumwambia anakosea.

Ni kweli kwamba mwanaume akiondoka kwao yapendeza aende kuanza maisha na mke wake kupata uzoefu wa ndoa lakini baada ya hapo anaweza kuongeza mwengine ndio maana hata manabii waliomtumikia Mungu waliweza kuongeza.

Hata Yesu alizikuta hizo ndoa zikiendelea na hakuwahi kuzikemea wala kuchukizwa nazo, katika mafundisho yake alitumia mfano wa mabikra kumi (10) kuolewa na mwanaume moja

Kuhusu suala la Adam na Eva huo ulikuwa ni uumbaji tu wala sio ndoa, hata Tetea kwa upande wa kuku aliumbwa moja tu na hata kwenye safina ya Nuhu aliingia Tetea moja tu na jogoo moja lakini haikuwa na maana jogoo awe na tetea moja

Mwanaume na Mwanamke kuwa mwili moja sio mwanaume kuwa na mke moja bali ni miili ya kiroho panapo makutano ya mwanaume na mwanamke hata katika uzinzi, hata mwanaume akitembea na kahaba huo tayari ni mwili moja, yapendeza miili hiyo iwe ya wanandoa si ya kizinzi, hata Sisi binadamu tuko wengi lakini mahusiano ya kila mwanadamu na Mungu ni roho moja takarifu na ndivyo ilivyo hata kwa mwanaume akiwa na wake wengi kila mwanamke atakuwa na mwili moja... 1 Wakorintho 6: 16-17- Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja. 17 Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye.
 
Mathayo 19:4
Akawajibu: “Je, hamkusoma kwamba yule aliyewaumba tangu mwanzo aliwaumba mwanamume na mwanamke 5 na kusema: ‘Kwa sababu hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye atashikamana na mke wake, na hao wawili watakuwa mwili mmoja’? 6 Basi wao si wawili tena, bali mwili mmoja. Kwa hiyo, kile ambacho Mungu ameunganisha mtu yeyote asikitenganishe.

Mungu alimpa Adamu mke MMOJA.
Kuoa wake wengi ni tamaa na kukengeuka.
 
Hata wafalme na manabii waliomtumikia Mungu walianza na mke moja ila wakaja kuongeza na Mungu wala hakuwakataza sehemu yoyote
 
Tupe hiyo sheria ya kuoa Wake wengi Mkuu.

Mungu hajawahi kumpa Ruhusa Mwanaume kuoa wake wengi na hajawahi kumkataza.
Ni suala la Utashi tuu.

Nazungumzia Mungu wa kwenye biblia
Manabii na wafalme kibao waliomtumikia Mungu walikuwa na wake zaidi ya Moja na Mungu hakuoneshwa kuchukizwa wala kuwakataza, kwa lugha nyepesi ni kwamba hakuona tatizo lolote na wala hakukuwa na dhambi

Ukimya wa Mungu kuhusu hili ni kwamba alipitisha wala hakuona shida
 
Hii ilikua kwenye agano la kale, agano jipya naona ni mke mmoja tu

Lakini bado sijauona mstari aliotangaza kwamba muwe na mmoja tu, nimeutafuta wee nimeukosa kwa kweli

Nikaja kugundua hii issue ilianza ukristo ulipofika roma, na roma ilikua ni lazima uoe mke mmoja
 
Unaombwa sheria unaleta hadithi.
Nabii gani alioa Wake wengi zaidi ya Yakobo tena kwa kuingizwa mkenge na mjomba wake?
 
Hii ilikua kwenye agano la kale, agano jipya naona ni mke mmoja tu

Lakini bado sijauona mstari aliotangaza kwamba muwe na mmoja tu, nimeutafuta wee nimeukosa kwa kweli

Nikaja kugundua hii issue ilianza ukristo ulipofika roma, na roma ilikua ni lazima uoe mke mmoja
Hata Yesu alijua uwepo wa hizi ndoa kihalali ndio maana alitoa fundisho kwa mfano wa mabikra watano kuolewa na mwanaume moja.
 
tangu mwanzo Mungu aliona si vyema adam akae peke yake,kutoka katika ubavu wake akampatia adam mtu mke,naye akamwita eva.

hapa ndipo tunapata malengo na mapenzi ya Mungu juu ya watu wake.

ndio sababu hata ktk mapenzi ni mwanamke mmoja tu huwa anafanikiwa kutuvuruga.
 
"
Tupe hiyo sheria ya kuoa Wake wengi Mkuu.
Lakini kwa sababu ya zinaa ni vyema kuoa kuliko kuzini...... "

Kuzini ni dhambi ambayo inafanywa na wengi sana akiwemo mitume na manabii.

Kuoa mke zaidi ya mmoja sio dhambi, hao kina mtume Paulo na team yake wakikutana na migogoro mingi ya ndoa za mitaala, hivyo wakaamua kuzuia hizo ndoa ili kuepusha migogoro, kwa kufuata utaratibu wa mtume Paulo na team yake ya wapindua ulimwengu, kuoa mke zaidi ya mmoja ni kosa (hasa kwa viongozi wa kanisa).

Kwa kufuata mpango wa Mungu kuoa mke zaidi ya mmoja sio kosa, na kama lingelikuwa kosa angeweka sheria ya kutoa mke zaidi ya mmoja.
 
Alafu Paulo NI muinjilisti tuu kama hawa unaowaona wanapita Mbezi stendi wakihubiri.

Unaposema Manabii Unazungumzia Ibrahim, Musa, Isaya, Daniel n.k.
 
Ile siku unamuumba mwanaume angemuumba na wanawake wengi
Au angesema mwaume utamuacha mama na baba yako ukaishi na wake zako

Na wewe mwanamke utamuacha baba na mama ukaishi na mume pamoja na wake wenza wako
 
Back
Top Bottom