Utaratibu na gharama za kupata hatimiliki ya nyumba/kiwanja

habari wanajamvi. Naomba mnielekeze namna ya kupata hati miliki ya nyumba na kiwanja. Tunaishi katika nyumba na kiwanja tulichoachiwa na marehemu baba yetu. Nategemea ushauri na msaada wenu. ASANTENI.
 
fuata hatua hizi: 1. ukoo uteue msimamizi wa mirathi kisha athibitishwe na mahakama, 2. msimamizi agawe mali kwa watoto wa marehemu, 3. aliyepewa nyumba aende manispaa kuomba hati miliki
 
Kabla ya kujibu swali lako ni vyema ukafahamu kuwa hakuna kitu kimoja kinachoitwa hati ya nyumba, bali kuna hati ya haki ya kumiliki kiwanja( kipande cha ardhi).

hivyo basi majengo yaliyo juu ya kiwnja hicho yanatambulishwa na hati ile ile iliyotolewa wakati kiwanja kikiwa kitupu, aidha uthibitisho wa uhalali wajengo juu ya kiwanja hutambulishwa na kibali cha ujenzi wa jengo husika.

Naam, ili kujibu swali lako ni vyema ukajiridhisha iwapo kiwanja hicho kimepimwa au la kwa maana kwamba hati itatolewa tu iwapo kiwanja hicho kimepimwa( surveyed land).

Kama kimepimwa na ramani mnazo basi msimamizi wa mirathi anaweza kuanza mchakato wa umilikishaji kiwanja hicho kwa majina ya warithi, mchakato huu unaanzia ofisi ya halmashauri ambapo utapatiwa fomu rasmi za utambulisho wa majirani ambazo utazijaza na kupitisha kwa majirani zako unaopakana nao kiwanjani kisha utazipeleka kwa diwani na serikali ya mtaa wote wkishasaini watakugongea mihuri,

Hatua inayofuata wakaguzi kutoka halmashauri watakuja kukikagua ili waandike taarifa ambayo itamsaidia afisa ardhi mteule/kamishna wa ardhi kutoa maamuzi ya kukumilikisha au la,
 
kiwanja hakijapimwa. Mimi ndo niliteuliwa na kikao cha ukoo kuwa msimamizi wa kila kitu kama kijana mkubwa wa marehemu.
 
Ok kwa mantiki hiyo lazima uanze taratibu za upimaji kwa kuwasiliana na wapima (land surveyor) wa halmashauri au wizarani au makampuni ya upimaji
 
Wakuu,

Nina kiwanja ambacho hakijapimwa. Nani anaweza kunifahamisha kuhusu taratibu za kufuatilia hati katika mambo yafuatayo:

1. Taratibu za upimaji (surveying)
2. Makadirio ya muda, tangu umepima hadi kupata hati mkononi
3. Gharama za surveyor na nyingine zote ambazo zitahitajika kulipwa

Pia, kama wewe umeshawahi kupima hadi kupata hati ya kiwanja chako, ntashukuru kama unanishirikisha uzoefu wako.

Kiwanja kipo dar, maeneo ya Mbezi, Tangi Bovu.

Pia, kama unamfaham surveyor ambae sio longo longo (maana hii fani karibu wote ni longo longo), naomba unijulishe.

Natanguliza shukrani

Nyongeza: Kiwanya kina ukubwa wa 20m x 25m
 
Ramthods;

mpe survyor wa wizara(wanapatikana pale ardhi ghorofa ya tisa, wizarani) ya ardhi hiyo kazi kwa bei atakayokutajia, wiki 2 utapata hati, other than that subiri miaka mitatu kwenda mbele .....
 
Last edited by a moderator:
mpe survyor wa wizara(wanapatikana pale ardhi ghorofa ya tisa, wizarani) ya ardhi hiyo kazi kwa bei atakayokutajia, wiki 2 utapata hati, other than that subiri miaka mitatu kwenda mbele .....

hilo ni la ukweli kabisa
 
mpe survyor wa wizara(wanapatikana pale ardhi ghorofa ya tisa, wizarani) ya ardhi hiyo kazi kwa bei atakayokutajia, wiki 2 utapata hati, other than that subiri miaka mitatu kwenda mbele .....

Nilikua sijui kama unaweza pata hati kwa wiki mbili. Una uhakika uncle? Ni kwa nn watu huwa hawaendi huko? Hapa jirani yangu ni miezi minne sasa naona kweupe hata dalili za hati bado.
 
naombeni msaada wenu jamani mwenye kujua jinsi naweza kupata hati kwa haraka nina kiwanja na nyumba goba nahitaji hati ili nichukue mkopo.nimejaribu kufuatilia wilayani pale wanasumbua sana.mwenye kujua hili plz au km kuna mtu ulipata ulipataje ulichukua muda gani!.
 
hakuna njia rahisi ya kupata hati halali kwanza kuna hati aina mpili kwa hapa dar


  1. hati ya makazi ambyo hutolewa na halimashauli za wilaya
  2. hati ya kiwanja ambayo hutolewa kwa kiwanja kilichopimwa hutolewa na wizara ya aridhi na makzi kwa hiyo kama unauitaji hati ya wizara ya aridhi kwenye eneo ambalo halijaimwa kama hilo lako unatakiwa uende wizarani kwenye kitengo cha upimaji na ramani wao watakupa uataratbu unaotakiwa kuufuata
 
hakuna njia rahisi ya kupata hati halali kwanza kuna hati aina mpili kwa hapa dar
  1. hati ya makazi ambyo hutolewa na halimashauli za wilaya
  2. hati ya kiwanja ambayo hutolewa kwa kiwanja kilichopimwa hutolewa na wizara ya aridhi na makzi kwa hiyo kama unauitaji hati ya wizara ya aridhi kwenye eneo ambalo halijaimwa kama hilo lako unatakiwa uende wizarani kwenye kitengo cha upimaji na ramani wao watakupa uataratbu unaotakiwa kuufuata

taratibu zikoje za kupata hizo hati...?
 
huwezi kupata hati kabla hujapimiwa...inabidi uende ardhi umpate surveyor aje akupimie upate ramani ndo hati iweze kuandaliwa..ukishapata hati niite nikufanyie valuation (uthamini) uchukue mkopo
 
nilishaenda wilayani kufuatilia sasa kwa maelezo yao niliona km ntachukua hata mwaka mana uyo mwenyewe niliyemuuliza haelewi itachukua mda gani.asanteni kwa michango wote,ntafanyia kazi upya.
 
Habari.mi ndio nimeanza kufuatilia mijadala ya jf na nimeifurahia.Naomba mnisaidie namna ya kupata hati miliki ya kiwanja.(ninamkataba tu wa kuuziana)Utaratibu unakuwaje?
 
Kwa anayefahamu tabata chango'ombe sehemu ya mwembeni ile maeneo ya pembezoni mwa barabara je eneo hilo ni surveyed lipo kwenye master plan au ni squatter?
 
Habari wana Jamii Forums,.

Nina kiwanja changu Bagamoyo ekari mbili ila mpaka sasa sijafanikiwa kupata hati ya umiliki wa eneo langu, Naomba kufahamu ni utaratibu gani niufuate pamoja na gharama zote za kupata hiyo hati.

Natanguliza shukrani wakuu,
 
Bw chakii kiwanja kiko bagamoyo kwanini uende posta?tafuta simu ya mkurugenzi mtendaji Wa wilaya bagamoyo atakuunga ni sha na maafisa Ardhi wake
 
Back
Top Bottom