Utaratibu na gharama za kupata hatimiliki ya nyumba/kiwanja

marandu2010

JF-Expert Member
Aug 7, 2010
1,199
435
Ukiwa na nyumba au kiwanja bila hati miliki haiwezi kukusaidia kupata mkopo, naomba wakuu mnisaidie mchanganuo wa gharama za kuipata hati miliki na taratibu zake, ninaanzia wapi na kuishia wapi?

Natanguliza shukurani zangu wakuu
Utaratibu

1. Pata barua ya utambulisho toka kwa mjumbe wako wa shina.

2. Andika barua kwa mkurugenzi wa Halmashauri kumuomba kibali cha kupimiwa (survey) eneo lako. Barua hiyo inatakiwa kupitia ofisi ya serikali ya mtaa na ofisi ya afisa mtendaji kata.

2. Fikisha barua hiyo pamoja na vithibitisho vya umiliki wa kiwanja chako (makubaliano ya mauzo au urithi) kwenye ofisi ya Serikali ya Mtaa pamoja na barua ya kuomba kupimiwa eneo. Serikali ya Mtaa itakukata kodi ambayo ni asilimia 10 ya thamani ya kiwanja. Serikali ya Mtaa itakutengenezea hati ya umili na kukupa ndamba ya kiwanja. Hati hii unaweza kuitumia kulipa kodi ya ardhi kila mwaka.

3. Pitisha barua hiyo ngazi ya kata. Hata hakuna makato zaidi ya "kamchango" kadogo ka ofisi kama sh. elfu 5 hivi. Huwa kuna michango ya shuguli za maendeleo etc kupitia huduma kama hizi.

4. Peleka barua hiyo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri. Mkurugenzi atasubiri Baraza la madiwani likae ili kupitisha ombi lako iwapo eneo hilo halipo katika mpango wa matumizi mengine zaidi ya residency etc.

5. Baada ya kupata kibali toka kwa Mkurugenzi, tafuta kampuni ya survey wakupimie na kampuni hiyo itawasilisha ombi la title deed wizara ya ardhi kupitia kwa mkurugenzi.

6. Wizara ya ardhi itakukabidhi title deed iliyokamilika.


Kama umepata letter of offer maana yake kwamba hapo ofisi ya ardhi ya manispaa wanaandaa file mbili ambazo zote zinafanana yaani moja copy yako na nyingine nadhani itabaki kwa upande wa serikali imeandikwa CERTIFICATE OF OCCUPACY (Under section 29), THE LAND ACT, 1999 (NO. 4 OF 1999) ambazo watakupa uzipeleke kwa mwanasheria kuthibitisha kwamba wewe umekubali terms and condition.

Unarudisha Manispaa ambao watazipeleka (au unapeleka mwenyewe) ofisi ya Kamishina wa Ardhi ambapo utalipa stamp duty sh. 500 (mia tano ambayo hata hivyo itakuwa tayari imelipwa wakati kiwanja kinanunuliwa kama inavyoonekana hapo chini) kisha unaandikishwa kwenye daftari na kupewa siku maalumu ya kurudi kuona kama hiyo CERTIFICATE OF OCCUPANCY (ndio hati yenyewe) kama imesainiwa na Kamishina wa Ardhi pia inabandikwa na ramani ndogo ya viwanja vilivyopo eneo lako of which cha kwako kinawekewa alama nyekundu plus namba ya hati, ukubwa na vitu kama hivyo. Kama ikishasainiwa tu unapewa hati yako kabisa na unasepa zako.

Hiyo laki 350,000 hapo ni utata kwani gharama ya kiwanja hicho ime-include mambo mengi, embu check letter of offer yako uone jinsi mchanganuo wa gharama ya kiwanja kama ilivyo kwa mnunuzi wa kwanza, ukicheck utaona kuna

- Premium (hiyo ndio gharama ya kiwanja wanakuwa wameweka amount
- Fees for certificate of occupancy ambayo ni 3000 ila hata kama imepanda haiwezi kuwa juu sana (hii ilikuwa 2006)
- Registration fees ni 2106
- Survey fees 24,570
- Deed Plan fees 6,000
- Stamp duty on Certificate and Duplicate 1,000
- Land rent ya mwaka ambao amenunua kiwanja 11,000 (baada ya hapo kila July mhusika unakwenda kulipa
Hivyo ukijumlisha zote kuanzia premium mpaka hizo gharama nilizokuonyesha unapata gharama halisi ya kiwanja na ipo indicated kwenye letter of offer. Let say, kama gharama ya kiwanja ni milion moja (ambayo ndio imeandikwa premium kwenye letter of offer) maana yake gharama ya kiwanja jumlisha hizo cost ndogondogo.

Ukisoma hivyo vigharama utagundua kila kitu kilishalipiwa na mnunuzi wa kwanza ambapo kimsingi kilichofanyika ni kubadili jina tu condition zingine zinabaki vilevile, so hati ni bure in this case unless taratibu ziwe zimebadilika, gharama ambayo utaingia ni hiyo ya mwanasheria ambayo ukienda utalipa labda mwekundu anagonga mhuri na kupiga sahihi na wewe unapiga sahihi mbele yake.

Tafuta ofisi ya Kamishina wa Ardhi, huwa zipo kikanda upate taratibu.


 
Hhati miliki kwa sasa zinatolewa kwenye eneo ambalo lina master plan, tofauti na zamani ambapo hata kama ulikuwa na shamba ambalo haliko kwenye plan unaweza kuipata hiyo, kwa sasa imesitishwa.

Unachotakiwa kufanya ni kuchukua coordinate za shamba au kiwanja chako (UTM coordinate) kwa kutumia GPS, and then unaenda wilayani au Wizara ya Ardhi, pale kuna ramani zote na plan zake, kwa hiyo unaangalia zile coordinate zako zinaangukia kwenye plan gani, kwa sasa kama hizo coordinate zako zinaangukia kwenye plan ya shule au makaburi au hospital au kama hakuna plan kabisa basi inakuwa shida sana kupata HATI MILIKI.

Kuhusu mikopo sijui wewe upo eneo gani, lakini kuna maeneo haya ya makazi yasiyo rasmi (squater area), kama baadhi ya maeneo ya Mazense, Tandale, Mwananyamala na aina hiyo ya maeneo, hayo Maeneo sasa yanatambuliwa kiserekali na kuna kitu inaitwa HATI YA MAKAZI

Kwa wilaya ya kinondoni inapatikana pale Mwananyamala (DSSD) Jiji, karibu na Hospitali ya Mwanyamala, hiyo inatambilisha kuwa hii nyumba ni ya nani, somesort ya hatimiliki!

Sasa hiyo (hati ya makazi) kuna baadhi ya bank (Azania Bankcop) wanaikubali na wanatoa mkopo kwa hiyo na mara nyingi mkopo wao hauzidi 10m, regardless na thamani ya nyumba yako.


Kkama kuna cha ziada just ask!
 
kwanza unastahili shukurani sana kwa msaada wa kimawazo ulioutoa,,nyumba moja iko vingunguti maeneo ya spenko na nyingine iko gongo la mboto karibu na pugu,,je maeneo hayo yanapata hati ya makazi?? naomba pia unifafanulie kuhusu GPS na UTM cordinate..

halafu gharama zake zinakuwaje kwa zote mbili yaani HATI MILIKI na HATI MAKAZI,

asante sana mkuu kituko
 
Ukiwa na nyumba au kiwanja bila hati miliki haiwezi kukusaidia kupata mkopo,,naomba wakuu mnisaidie mchanganuo wa gharama za kuipata hati miliki na taratibu zake,,ninaanzia wapi na kuishia wapi???
Natanguliza shukurani zangu wakuu

Mkuu, Naona umelianzisha faster Nguvu mpya, Ari mpya mwendo mdundo.. sasa umeshajua ni biashara gani utaifanya ??? maana una chaguzi lukuki from shamba moro, spea za pikipiki, frame za maduka , ufugaji wa kuku !! kuajiriwa au kujiajiri ??? Nilijua kuna shimo lako limetema mkuu.... au unatafuta za kujazia - " I'm just kiddin'"
 
Originally Posted by marandu2010
Ukiwa na nyumba au kiwanja bila hati miliki haiwezi kukusaidia kupata mkopo,,naomba wakuu mnisaidie mchanganuo wa gharama za kuipata hati miliki na taratibu zake,,ninaanzia wapi na kuishia wapi???
Natanguliza shukurani zangu wakuu

Mkuu, Naona umelianzisha faster Nguvu mpya, Ari mpya mwendo mdundo.. sasa umeshajua ni biashara gani utaifanya ??? maana una chaguzi lukuki from shamba moro, spea za pikipiki, frame za maduka , ufugaji wa kuku !! kuajiriwa au kujiajiri ??? Nilijua kuna shimo lako limetema mkuu.... au unatafuta za kujazia - " I'm just kiddin'"

Na bado unatafuta biashara ya Internet Cafe, Shule n.k - ni wewe mwenyewe au ??

" Hizi hela (fungu) za uchanguzi ulizopewa zaweza kukufanya ukachanganyikiwa ndugu yangu "
 
kijana angalia,,nitakurushia kombola!! wewe unanichunguza tuu,,unajua nawahuhumia hawa vijana watakosa mtu wa kumkopesha kwa sababu watu wenye sifa hizo ni wachache,,si unajua mimi ndio mfalme wao,,ninataka kuwapa kariba kao waendelee kusogeza siku,,,si unajua mimi sio mbinafsi bwana!! napenda kuona mambo yanachangamka,,sio benki zinakuwepo hakuna wanaochukua mkopo,zisije zikafilisika buree wakati mimi nipo.

kupigia msumali zaidi suala la kuwa SELFISHLESS,nataka watu wengine wajue hizi habari,si unajua watanzania wengi tu maskini wa habari..nadhani umenipata hapo..

ukweli ni kwamba naendelea kusubiri maoni ya wakuu wengine ili kufanya maamuzi yenye akili zaidi,yaaaah ninaamini ukijenga msingi wako katika utajiri wa mawazo mazuri,nyumba yako itakuwa nzuri sana na hata kudumu sana,

note kuna maeneo KIDDING na mengine SERIOUS.

asante sana mkuu kwa kautani kazuri.
 
Kukodi GPS nsa mtu wa kukusomea coordinate na kupata barua inayoonyesha kama eneo linafaa kupimwa or not ni Tshs. 50,000 (Hii ni kwa mtu aliyenifanyia mimi)

Gharama za upimaji (kwa mtu aliyenifanyia mimi) ni Tshs. 900,000( gharama inaweza kubadilika according to surveyor utakayempata)

Gharama nyingine ndogondogo ambazo hazizidi Tshs. 200,000 mpaka kupata hati

So, ukitaka kupata hati, kuanzia kupima mpaka kuwa na hati uwe na si chini ya Tshs. 1,000,000.

Vingunguti wanaruhusu leseni za makazi na gongo la mboto pia. Kupata leseni za makazi ni rahisi zaidi na haichukui muda kama hati na gharama yake pia ni ndogo. Vingunguti na Gongo la mboto zipo manispaa ya ilala, ukitaka kupata leseni ya makazi nenda ofisi za manispaa ya ilala kitewngo cha lesen i za makazi.

Ofisi zipo karibu na ofisi za jiji.

Gharama ya kupata
kwanza unastahili shukurani sana kwa msaada wa kimawazo ulioutoa,,nyumba moja iko vingunguti maeneo ya spenko na nyingine iko gongo la mboto karibu na pugu,,je maeneo hayo yanapata hati ya makazi?? naomba pia unifafanulie kuhusu GPS na UTM cordinate..

halafu gharama zake zinakuwaje kwa zote mbili yaani HATI MILIKI na HATI MAKAZI,

asante sana mkuu kituko
 
MARANDU 2010.
swali lako ni too general, lakini kama unataka kupata hati ya nyumba yako ambayo ipo katika maeneo ambayao hayajapimwa, kitaalamu tunayaita "maeneo ya mazagazaga" ama slums na siyo squatter kama watu wengi wanavyosema.mambo ya msingi ili upate hati ni kama ifuatavyo
1. eneo lako inatakiwa liandaliwe TP drawing "town planning drawing" 1,200,00
2.lipimwe "surveyed" 2,000,000
3.ulipie gharama zifuatazo
-fees for preparation of certificate of occupancy 10,000
-Registration fees 5000
-stamp duty 3000

baada ya hapo unatakiwa uwe na nyaraka zifuatazo ambazo manispaa yako watakupatia wakati wa kukumilikisha kiwanja
-land form no 19 inalipiwa 5000
-barua inayoelezea historia ya kiwanja
-acknoledgement letter kwa ajili ya malipo ya serikali uliyolipia
-berth certificate au kitambulisho cha uraia

ukikamilisha mambo hayo afisa ardhi mteule wa manispaa yako ataandaa rasimu ya hati na kuiwasilisha kwa kamishna, kamishna ataisaini na hatimae atagonga mhuri wa moto kama ipo sahihi, then itawasilishwa kwa msajili kwa ajili ya kuisajili hiyo hati

kaka upo ukikwama nitumie Email kwanzamen@yahoo.com
 
GPS na UTM ni vifupi katika fani za Jiografia na Surveying (Upimaji). Kwa kifupi maana yake mtoa maelezo ni kwamba ueleze kiutalamu wa upimaji hiyo sehemu iko wapi - au umpate Surveyor akakupimie kwa kutumia hiyo GPS.
 
Mada naona imekuja muda muafaka, Asanteni wadau.

Nina mchakato wa kuchukua kakiwanja maeneo ya Kisarawe (Kibong'wa), nasikia panapimwa huko. hati miliki nitapata (NINA UHAKIKA!)

Kwa anayepafahamu huko Kibong'wa;

Naweza kukopa pesa toka BANK kwa kumiliki kiwanja TU bila jengo wala nini? Na ni Bank gani naweza kupata mkopo wa aina hiyo na ni MAXIMUM amount ya mkopo ni kiasi gani?

Mi' niko machakani huku Mtwara (lakini panachangamka!).

Kibong'wa sipajui lakini kuna rafiki yangu wa KUFA na KUZIKANA alinistua kuwa atanisaidia kufuatilia kiwanja ili nami nipate huko Kisarawe.

Naomba mnisaidie majibu.
 
wana JF,

Natumai mu wazima. Naombeni msaada wenu wenye kufahamu utaratibu gharama za kupima kiwanja chenye ukubwa wa ekari tatu.

kuna jamaa nilikuwa nina deal naye mwanzoni, lakini nikashindwa baada ya kunitajia bei za juu mno. Mara ya kwanza nilipompeleka kuchukua coordinates za kiwanja nilimlipa Tsh. 80,000 taslim.

Baada ya hapo aliniambia sehemu ndogo ya kiwanja ilishafanyiwa pre-survey, but sehemu kubwa ipo nje ya mchoro. Na hivyo marekebisho ya mchoro yatagharimu Tsh. 400,000.

Baada ya hapo alinitajia gharama zingine ambazo sizikumbuki, lakini jumla ya mchakato wote ilikuwa inagharimu Tsh. 3,100,000/= ( milioni tatu laki moja).

Je, kwa mwenye kufahamu process kiasi hicho ni halali?
 
wanajf kwa msaada wa wengi naomba kujua utaratibu wa kupata hati ya nyumba,

nilinunua kiwanja zamani yapita miaka mitano sasa, hata mkataba wa mauziano haupo, nimeshajenga nyumba nimeweka mpangaji. maeneo ya mbezi ya kimara (km 1 toka morogoro road)

nikitaka kupata hati ya nyumba naazia wap na gharama zake ni kiasi ghani na inachukuwa muda ghani kupatikana



wenu

J kwa J
 
J kwa J

nadhani itakuwa sahihi ukisema unahitaji hati ya kiwanja, certificate of occupancy (Tittle Deed)

vinginevyo labda unahitaji hati ya makazi

please advice and clarify
 
J kwa J

nadhani itakuwa sahihi ukisema unahitaji hati ya kiwanja, certificate of occupancy (Tittle Deed)

vinginevyo labda unahitaji hati ya makazi

please advice and clarify

mkuu nilijieleza sana ungenipatia maelezo tu
(kilikuwa kiwanja sasa nimeshajenga hapo nyumba natakiwa nipate nini kama mmiliki halali wa hiyo nyumba)
 
Back
Top Bottom