Habari wadau
Nina imani humu kuna wataalamu wa sheria za ardhi. Na pia wapo watu wenye uzoefu na mgogoro wa ardhi kama huu wa baba yangu mdogo.
Mwaka 1988 baba yangu mdogo alinunua kiwanja maeneo ya yombo vituka kutoka manispaa ya temeke.
Alilipia malipo yote yaliyohitajika. Na kupewa hati ya kiwanja chake (certificate of occupancy)
Wakati anajipanga kuanza ujenzi mnamo mwaka 1990 akaamua kwenda kwenye kiwanja chake akawa amepanda miti ya miembe.
Akaendelea kulipia kodi za serikali za ardhi.
Mwaka 1994 baba mdogo alipata na kesi ya mauaji... alipigana na mtu kazini kwake bahati mbaya huyo mtu alifariki.
Kesi ikapelekwa mahakamani ikasikilizwa mwishoni kabisa baba mdogo akahukumiwa kufungwa miaka 30. Hivyo akapelekwa gerezani kutumikia hukumu yake.
Mwaka jana december baba mdogo akafanikiwa kutolewa jela. Na kurudi uraiani.
Baada ya kurudi uraiani. Akatuambia ndugu tumsaidie kujenga kwenye kiwanja chake hata chumba kimoja ili apate pa kuishi amalizie maisha yake. Wazo likapita.
Akaenda kwenye kiwanja chake ili aandae mazingira ya ujenzi. Shida kubwa alipofika kwenye kiwanja chake kakuta kuna familia inaishi.
Imejenga chumba na sebule. Na inadai hapo ni kwao wamerithi kutoka kwa baba yao. Ambaye ameshafariki toka mwaka 2013.
Wakamuitia Mjumbe na viongozi wa kata kudai baba mdogo anataka awazulumu kiwanja chao.
Baba mdogo akaeleza stori nzima ilivyokuwa na akatoa na documents za kiwanja chake alizopewa na manispaa ya temeke miaka ya 90. Akatoa hati ya kiwanja certificate of occupancy. Na document ingine aliyopewa wakati ana register imeandikwa certificate of title. Watu kuzicheki zile documents kweli ni halali.
Ile familia iliyokuwa inaishi yenyewe haina document yeyote ya kiwanja zaidi ya muhtasari wa kikao cha familia wakati wa mirathi.
Wanadai hapo ni kwao ila hawajui marehemu baba yao hati zake aliweka wapi. Hivyo hawana hati.
Mjumbe na watu wa kata wamemshauri baba mdogo aende mahakamani.
Maana wao hawamjui. Ila hiyo familia wanaijuia kwa miaka mingi inaishi hapo na hata majirani wote wanatambua kama ndio wamiliki wa hapo.
Na wakasema sheria inammilikisha kiwanja mtu mwingine. Kama ikitokea mmiliki hujakiendeleza kiwanja chako kwa miaka mingi.
Hivyo baba mdogo hana haki maana yeye ndie aliefanya ujinga wa kutoendeleza kiwanja chake mapema. Ama kuwaambia ndugu zake wakiendeleze kwa niaba yake wakati yupo jela
Naombeni msaada wa ushauri wataalamu wa ardhi. Je, mahakamani baba mdogo atatoboa kweli?