Utaratibu na gharama za kupata hatimiliki ya nyumba/kiwanja

Hapo blue sipo aware ila nahisi hati za kimila kama zipo applicable vijijini vile? upimaji shirikishi ni kuji-organize watu wote wenye majengo katika eneo husika na kuwafuatilia hawa watu ardhi nadhani kwa Kinyerezi itakuwa Ilala kama sijakosea au wizaeani kabisa maana kwa Dar even watu wa wizarani nao wanajihusisha na hii kitu. Sidhani kama kuna idadi maalumu kikubwa hata kama mpo kumi na kuendelea mnaweza kuanzisha move wengine watafuata

mkuu ahsante kwa majibu yaliyonyooka ,kuna hawa jamaa ni mawakala wa kusurvey wamemuwekea jirani yangu beacon huku hana hati pesa wamechukua laki 7 hii imekaaje mkuu
 
Halafu unapowekewa beacon katika kiwanja chako ni kuonesha kua upimaji umefikia hatua ambayo utapeli hamna, Au hata beacon zinachakachuliwa? I mean huwa zinatengenezwa wizarani? Au hata mtaani matapeli wanazitengeneza!
 
Becon mkuu huwa zina namba na alama zao wanazijua akija na ramani ya eneo hilo tu akishapata becon ya kiwanja kimoja atazipata zote (wanajua kabisa ukienda mita kadhaa upande flani utakuta becon), huwa wanaziweka wao mkuu though kuna ambazo unaweza kuweka wewe au mtu mwingine kwa ajili ya alama zako kwa kuwa wakati mwingine kiwanja chako kinaweza kikawa na becon 2 ambazo zina namba alafu wengine huongezea.
 
mkuu ahsante kwa majibu yaliyonyooka ,kuna hawa jamaa ni mawakala wa kusurvey wamemuwekea jirani yangu beacon huku hana hati pesa wamechukua laki 7 hii imekaaje mkuu

Kikubwa ni kuhakikisha una receipt ya serikali maana mjini wajanja ni wengi pia unatakiwa kujua hawa jamaa mpaka wao wa kazi ni upi maana labda wao wanaishia kupima alafu mwenye eneo anafuatilia issue ya hati maana watz wengi huwa ukipata offer au umelipia kiwanja unalidhika kumbe kuna hatua nyingine ya ziada ya kufuatilia hati
 
mkuu nakushukuru sana sana endelea kuwepo humu jamvini naamini wengine wataleta mada zao zinazohusiano na ardhi ,hutatasita kukutumia pale inapobidi ,umeonyesha uwezo kwenye masuala ya ardhi nikushukuru sana pia wana jf wote ,jamii forum ni kila kitu
 
Pamoja sana mkuu, hapa tunasaidiana na kushauriana mkuu based na yale yaliyotukuta wakati tunafuatilia haya mambo na ndio maana huwa ninashauri tusipende kumtumia mtu wa kati kwa mambo ya msingi kwa kuwa kwa kujaribu kwenda mwenyewe directly unapata practical experience ya kile unachokitafuta au unauliza before kwenda kama mdau alivyofanya na ndio maana wengine tulifuata hizo process nikajifunza kitu. Jaribu kufuatilia kwanza ukikwama ndio unaanza kutafuta njia mbadala.
 
Jodoki Kalimilo;

Mkuu kwanza samahani sana kwa kupotea kidogo, Asante sana kwa maelezo ya kina juu ya hili suala langu, ila niliambiwa huwa Letter of offer haitolewi mara 2, kinachofanyika ni kuauthorize transfer kwa kugonga mihuri kwenye mikataba na land forms, ikisha kuwa authorized na afisa ardhi watu wa database aka computer wanabadilisha jina kutoka kwa mmiliki wa kwanza na kuwa kwa jina lako, so kama utakuwa unalipa kodi ya pango la kiwanja litatokea jina lako!!

asante kwa mwongozo, inaonekana kuwa kila kitu kilishalipiwa na mmiliki wa kwanza mm ni kukomaa tu, ila watu wa Moro tunahududumiwa na Dsm, na pale nina conjugates ambao nadhani hawatanikwaza

asante sana na barikiwa mno!

JF daima dumu
 
Last edited by a moderator:
Kiresua;

Vizuri mkuu kila kitu kipo covered hiyo laki 3.5 wanataka kukupiga changa la macho, lakini kikubwa taratibu zote za manunuzi umefuata na jina lako lina appear hivyo hiyo ardhi ni mali yako komaa nao mdogomdogo huna haja ya kuwa na pressure nao
 
Last edited by a moderator:
Nilikuwa na kiwanja na nimeshaanza ujenzi huko Mbande,je naweza kupata hati ya kiwanja baada ya kujenga nyumba?
 
Jodoki Kalimilo;

Ndugu Jodoki, majibu yako yamenifurahisha sana, inaonyesha unaupeo mzuri katika mambo haya. Mimi niimestushwa sana na kupandishwa kwa gharama ya kodi ya kiwanja changu, maeneo ya Dar. Nimeanziasha thread huku about that. Katika thread hii swali langu kuu lilikuwa ni hili;

Je, hivi inawezekana kweli kodi ya kiwanja chenye ukubwa wa acre moja ikapande kutoka 90,500 (2011/12) mpaka 340,000 (2012/13) tshs? Hivi kodi za viwanja zimepanda au unataharifa zozote za mabadiliko haya?

Tafadhali naomba unisaidie kwa ufahamu wako.
Ni matumaini yangu kwamba mchango wako unaweza kuwasaidia na watu wengine.

Asante sana
 
Last edited by a moderator:
Nara;

Sipo aware sana ila nitafutalia maana hilo ongezeko ni kubwa pia sijui eneo hilo ni la biashara au vipi?
 
Last edited by a moderator:
Sipo aware sana ila nitafutalia maana hilo ongezeko ni kubwa pia sijui eneo hilo ni la biashara au vipi?

Asante for a quick answer. Eneo lenyewe pamoja na kwamba lina some business lakini current status yake bado haijabadilika from residential to commercial even though i have already applied for it. Kwa hiyo unaweza kusema ni residential.

I will appreciate to get ur opinion about this, tusijetukawa tunaibiwa!
 
Jamani kweli Jamii forums kama nikitaka kuorodhesha mambo niliyofanikiwa nilipaswa hata kuwapa shukrani walioanzisha website hii.

Sasa na mimi kaka nina shida na eneo nimenunua hivi karibuni. Eneo hilo limepakana na mahalai penye plan na pana mawe yakuonyesha pame pimwa , lakini mbele ambapo ni pangu hakuna plan. Nifanye nini nami ili niingizwe kwenye plan? Nilipoukuwa na nunua watu wa Serikali ya mtaa waliniambia wala usiwe na wasi wasi utapata na wewe.

NOMBA MSAADA JE NIANZIE WAPI?

Barikiwa kaka
 
Asante for a quick answer. Eneo lenyewe pamoja na kwamba lina some business lakini current status yake bado haijabadilika from residential to commercial even though i have already applied for it. Kwa hiyo unaweza kusema ni residential.

I will appreciate to get ur opinion about this, tusijetukawa tunaibiwa!

Ila kiukweli kodi za viwanja huwa si kubwa kiasi hicho vinginevyo watu wengi wangekuwa wamenyang'anywa maana navyojua mimi kosi ya kiwanja huwa around 11,000 to 25,000 sasa hapo nashindwa kuelewa. Na hiyo ukilipa unapewa receipt ya serikali ile ya rangi ya manjano na nembo ya taifa au just kulipa tu ili mradi kulipa.

Yaani hata hiyo 90,000 kwangu naona nyingi sana maana kama kodi ya jengo ni hiyo let say 90,000/= sasa kama umejenga nyumba ukaambiwa ulipe kodi ya majengo itakuaje hapo si utaambiwa ulipe laki 5 (si unajua tena kwa mwaka huwa unatakiwa ulipe kodi ya kiwanja na kodi ya majengo kama una jengo ambalo tayari limeezekwa na mara nyingi kodi ya majengo huwa ni kubwa kuliko ya kiwanja, in this case kama kodi ya kiwanja ni 350,000, hapo kodi ya jengo sijui itakuaje mdau)

Hapo kuna dalili ya kupigwa changa la macho mdau maana ardhi ni mali ya umma na serikali inaweza kuchukua muda wowote inapotaka na ndio maana inalipa fidia (kikubwa kama mode of payment ni ya kichina kichina hapo kuna walakini lakini kama unapewa receipt ya serikali ambayo inaonyesha kabisa kodi ya ardhi ya kiwanja namba flani hapo nadhani tunahitaji kuandamana
 
Mbwambo;

Ni mkoa gani huo mkuu maana sehemu nyingine unachotakiwa ni kuwaita watu wa ardhi na kuwaonyesha eneo lako na wao wataangalia master plan yao, hata kama kitakuwa hakijapimwa lakini watakuwa na plan inayoonyesha kama hilo ni eneo la makazi au vipi na ikitokea kwamba ni eneo la makazi basi utaangukia katika upimaji shirikishi ambao mara nyingi lazima kuwe na nyumba tayari zimejengwa (ndio inakuwa cheap) maana kinachofanyika ni mnapangwa kulingana na mipaka ya asili (barabara ambazo mmeziainisha wenyewe). Kama mfuko unaruhusu ndio hiyo unafanya utaratibu wa kupima mwenyewe kwa gharama zako ambayo ni gharama kubwa inaweza kuwa zaidi ya 3 million kupimisha eneo kama sikosei ambapo inapendeza kama una eneo ekari kadhaa.
 
Last edited by a moderator:
Kiresua;

Poa mdau ila hapo nilipo bold unaweza ulizia kuhusu hizi kodi za ardhi maana inaonekana kama kuna ambao wanaambiwa walipe kodi nyingi mfano ni mdau Nara ameibua issue nyingine muhimu kwa kuuliza swali ambalo kiukweli nimeona kama hiyo kodi ni kubwa sana, embu waulize kodi ya ardhi inakuaje ili kumsaidia Nara kama alivyouliza hapo chini;

Je, hivi inawezekana kweli kodi ya kiwanja chenye ukubwa wa acre moja ikapande kutoka 90,500 (2011/12) mpaka 340,000 (2012/13) tshs? Hivi kodi za viwanja zimepanda au unataharifa zozote za mabadiliko haya?
 
Jodoki Kalimilo;

Jamani yaani maelezo ni mazuri sana. Sasa na mimi ninashida naomba ushauri kwako mpendwa kaka wa JAmii forums.

Nimenunua mahali fulani mwezi jana nilipotafuta kujuwa kama kuna plan surveyor kasema hapo kwangu hakuna ila nyuma yake karibu na hapo plan ipo na watu wehapimiwa. Nikaamua tu kupanunua lakini nimenunua kwa kuandikishiana na Serikali ya mtaa ambao walikwena moaka kuona eneo husika na kisha kuandikishiana.

Sasa nifanye nini nami eneo langu lipate kuingizwa kwenye plan?

Asante kwa kunijibu na Mungu akubariki
 
Kaka asante sana kwa hii shule nzuri...hata mimi nimejua cha kufanya..du nilishaombwa laki2 kwa kazi kama hii.

JF idumu....tusiwekewe king'amuzi humu.

JF patamu jamani
 
Kaka asante sana kwa hii shule nzuri...hata mimi nimejua cha kufanya..du nilishaombwa laki2 kwa kazi kama hii.
JF idumu....tusiwekewe king'amuzi humu..JF patamu jamani

Poa mkuu wakiweka king'amuzi mbona ni balaa, JF acha idumu maana tunajifunza vitu vingi humu
 
Hati miliki iko ktk ngazi mbili; Offer inatolewa na Halmashauri ya wilaya au manispaa na Hati miliki inayotolewa na kamishna wa ardhi tu.
Hati inayotolewa na Wilaya/manispaa lengo lake ni kukuwezesha kupata Hati miliki yenywe. Watu wengine wanaweza kuitumia pia kupata mikopo kwa sababu kuna baadhi ya taasisi wanaziamini na tayari uwezekano wa kupoteza ardhi yako umeshakuwa mdogo.

Hati miliki ambayo inapaswa iwe ya miaka 33, 66 au 99 hutolewa na kamishna wa Ardh tu na mwenyewe uwezo wa kuifuta ni moja tu - Rais.
Hati miliki kwa sasa ni ngumu kupatikana kwa bei hiyo. Mara nyingi inakwenda mpaka mil 1 au zaidi. Hata hivyo, gharama kubwa ni za makampuni ya upimaji kuliko gharama halisi zinaenda serikalini.
Mwisho, ukipata hati yako ndani ya miezi 4 hadi 6 umejitahidi. Huwa ni ngumu sana. special case always zipo lakini huwa ni kwa watu wenye connections kubwa serikalini na ndio maana tunataka tubadilishe utawala wa nchi hii ili mambo yawe sawa kwa wote.
 
Back
Top Bottom