Utaratibu na gharama za kupata hatimiliki ya nyumba/kiwanja

Kama upo kata ya Saranga kimara ambayo nadhani inaishia kwa msuguri, Kimara B yote kwasasa kunaupimaji shirikishi.

nenda manispaa Kinonondoni mipango miji kaangalie survey plan na upewe namba ulipie ili wakupimie bei zao ni 290,000 kwa sqm maixmum 300, 340,000 kwa sqm mpaka 400, 440,000 kwa sqm chini ya 1000, na 790,000 kwa sqm zaidi ya 1000 mpaka 1500.

Mimi nimefuatilia kama wiki mbili zilizopita wameanza november 2011. Namba na ramani pia zinapatikana Kimara amtangini serikali za mitaa ni mradi wa muda ukipita utpata usumbufu .
 
mkuu nilijieleza sana ungenipatia maelezo tu
(kilikuwa kiwanja sasa nimeshajenga hapo nyumba natakiwa nipate nini kama mmiliki halali wa hiyo nyumba)

hicho bado ni kiwanja ambacho kina nyumba (property), hata kama una nyumba umiliki unaotambulika kisheria ni hati ya kiwanja

hivyo ninakushauri uanze na kutafuta nyaraka ya mauzianno na aliyekuuzia, halafu upate hati ya utambulisho wa ununuzi ya serikali ya mtaa/kijiji/kitongoji, then utaomba muhtasari kwa ajili ya maombi ya kupima ili uweze kufanya maombi ya kumilikishwa, then utatafuta surveyor atafanya upimaji na kuwakilisha maombi yako ardhi, angalizo ni kwamba sehemu hii iwe haipo katika maeneo yaliyopangwa kufanyiwa mipango miji,

ukifanikiwa utapewa letter of offer then you will proceed into tittle deed
 
Mkuu
Nenda serikali ya mtaa wanakupa mkataba unaoonyesha kwamba unamiliki kihalali eneo (hatua ya kwanza)

Mtafute survey afanye survey eneo lako na akupe survey document (hatua ya pili)

Nenda manispaa ya kinondoni wanakupa forms kuomba hati ya kiwanja ambazo utazipitisha serikali ya mtaa pia (hatua ya tatu)

Ukishamaliza hayo unarudisha the whole documents kwa bwana ardhi wa wilaya unasubiri hati yako

(ni vizuri ukafanyiwa na wataalamu wa ardhi)..
 
Kwanza hakikisha documents za mauziano ya kiwanja hapo awali toka kwa mmiliki wa awali unazo. Tatizo wengi wetu hufanya mauziano ya kienyeji bila kupitia vyombo husika ili kuweka kumbukumbu za kisheria. maofisa wa Idara ya ardhi mara nyingi hutaka hati za mauziano kama mmiliki wa awali alikuwa mwingine, na hata kama ulinunua kiwanja kipya basi hati ziwepo ili kurahisisha zoezi la kuratibu umiliki wa kiwanja chako na kupata hati ya makazi.

Kabla hujaenda mbali kama wengi walivyodokeza hapo juu, mwenyekiti wa serikali ya mtaa ni hatua ya awali ambayo katu huwezi kuruka kihunzi hicho. Huyo anayo ramani na taarafa zote za mipango miji kama eneo lako ni la makazi au la. Na huyo ndiye atakayekupa maelekezo ya hatua za kufuata. Ukiamua kumruka huyo mwenyekiti wa serikali za mtaa utakapofika huko juu utarudishwa tu hadi kwake na kuanza upya. Usihangaike nenda kwa huyo na atakupa ushirikiano na kukusaidia nini ufanye na hatua gani za kuanza.

Angalisho: Ununuzi wa viwanja ni muhimu kuuziana kwa documents ambazo zinakuwa zimethibitishwa na vyombo vya sheria na hasa nchini mwetu ni bora akutumia mahakama. Ukifanya hivyo utakuwa umeepuka migogoro kadhaa ambayo huwakumba watu kutokana na utata wa umiliki.
 
Wazee mimi nimepata hati miliki kirahisi sana huko wilayami nilitumia 2,000,000
ambapo tsh 1000000 nilinunua kiwanja na nikamwezesha mtumishi mmoja 1,000,000 nikapata hati yangu ndani ya siku 21.
 
Naomba ushauri kujua jinsi ya kufanya kupata hati ya kiwanja(Na siyo offer letter). N apia nomba kujua hatua za kufuata kupata hati ya Nyumba.

Nashukuru kwa kuendelea kunielimisha na Mungu awabariki.
 
hati ya kuwanja certificate of occupancy (tittle deed) ndiyo doc unayotakiwa kuwa nayo, hiyo hati ya nyumba siifahamu , nyumba ni property iliyopo kwenye land .

document ya nyumba ni certificate of occupancy (tittle deed)

labda wadau wengine kama wao wanafahamu tofauti
 
Mkuu nadhani unaulizia title deed! Hauwezi kupata title bila kua na offer,kwanza nenda halmashauri usika waambie kwamba unataka kupimisha kiwanja,watakuja na gps watachukua cordinates then watakuja kukupimia then utataomba upewe offer ya title deed kwa kuapply wakishakupa offer then utaenda kulipia utapata title deed(ambayo ndio hati ya kiwanja),nyumba haina hati si unaweza ukavunja na ukajenga ghorofa hata kumi kwenye block hiyo hiyo!
 
Mkuu! Bila shaka umekuja vema kbs!

Lakini Mi ckujuaga kama nyumba haina hati. Nashukuru kwa kutujuza hili kwn wengine tulikuwa giza bado.
 
Mkuu nadhani unaulizia title deed! Hauwezi kupata title bila kua na offer,kwanza nenda halmashauri usika waambie kwamba unataka kupimisha kiwanja,watakuja na gps watachukua cordinates then watakuja kukupimia then utataomba upewe offer ya title deed kwa kuapply wakishakupa offer then utaenda kulipia utapata title deed(ambayo ndio hati ya kiwanja),nyumba haina hati si unaweza ukavunja na ukajenga ghorofa hata kumi kwenye block hiyo hiyo!

Kaka,
Yaani umejibu kwa ufasaha sana sana na hata sisi wengine tuilikuwa hatuelewi tofauti hizo na maana halisi ya Title deed na offer.
Sasa ninaelewa nitaanza wapi na mimi kisha nimejuwa niandae na kapesa kakulipia ili nipate Title dee.
Barikiwa mkuu kwa ufasaha wa maelezo yako:A S 465:
 
King Kong III Majibu yako ni sahihi kabisa, lakini vipi kuhusu rushwa hadi ufanikiwe maanake nasikia ni kimbembe kweli kwenye kufanikisha mchakato huo!
 
Mbona kupata hati kwa Tanzania ni usumbufu sana halafu ni ghrama sana. Tangu nilipie nina miaka kama minne hivi napigwa chenga kila nikienda. Kuna wakati faili langu lilipotea mwaka mzima alionekani. Naomba kama ndiyo hali halisi au nasungushwa ili nitoe kitu kidogo.
 
King Kong III Majibu yako ni sahihi kabisa, lakini vipi kuhusu rushwa hadi ufanikiwe maanake nasikia ni kimbembe kweli kwenye kufanikisha mchakato huo!

Kwa kweli tatizo la rushwa ni kubwa sana sana, hasa pale Makao Makuu ya Wizara ya Ardhi.
Nilidhani Prof. Tibaijuka angefanya hili ni tatizo la kwanza la kuwatatulia Watanzania. Ameshindwa.

Pale Wizara ya Ardhi wafanyakazi wote, kutoka Messenger hadi Mkurugenzi, wameanzisha makampuni yao ndani ya Wizara (syndicate). Mara ya mwisho nakumbuka walikuwa wanatoza si chini ya shillingi Milioni Mbili kwa mtu biafsi ili faili lako la Title Deed litembee kutoka ofisi moja hadi nyingine pale pale wizarani. Zile Computer zimewekwa kama mapambo tu. Shughuli hiyo inafanywa Kimafia kwani unaambiwa tu weka pesa kwenye bahasha na kabiddi kwa messenger pale ground floor. Ukishakabidhi tu wanakutaarifu baada ya dakika zisizozidi tano kuwa mzigo wameupata.

Nimengeandika sana lakini naona kichefuchefu na Wizara ya Ardhi. Inawezekana kabisa tukafukuza wale wafnyakazi wote na kuajiri dara la saba na wakafanyaka kazi nzuri kuliko wanayofanya hao waliopo.

Mungu Ibariki Tanzania!
 
Kuna hili tatizo jingine,
Watu wananunua vawanja kwa wengine na serikali ya kijiji inaridhia.
Mtu unakwenda ardhi kupima update title, serikali kuu inasema ni Barabara, hapa inakuaje?
Serikali zinajichanganya??
 
Habari zenu GT

i hope everyone yupo powa kabsa. Kwa yeyote hapa jamvini mwenye ufahamu wa mambo ya kupima kiwanja na mchakato mzima wa kupata hati naomba msaada wake wa ushauri na mawazo. Mimi nina kiwanja changu kipo maeneo ya Goba, Wilaya ya kinondoni, DSM. Ni kiwanja chenye ukubwa wa takribani sq. meter 2,100. Naomba kama kuna mtu anayejua anisaidie kujua mchakato mzima na gharama, pia ushauri wake na mawazo yake yatakuwa highly appreciated. kwa sasa nipo nje ya nchi, ningekuwa bongo, ningeenda kwenye ofc za manispaa kuulizia huo mchakato.
 
Habari wana JamiiFrm.
Naombeni msaada,mimi ni mkazi wa Arusha,nina kiwanja changu chenye vyumba vyangu ila wakati wa kununua nilimtumia mchumba wangu akailipie kiwanja kwa jina lake.
Nataka nikiwekee hati miliki ya kiwanja hicho na nyumba yake.
Naomba mwenyekujua anijuze njia ya kufanya na Garama ya kutimiza lengo hilo.
NAMALIZIA KWA KUWASHUKURU,
ASANTENI
Nawakilisha kwenu kwa msaada.
 
Kama ni eneo ambalo halijapimwa utahitaji kwanza lipimwe na registered surveyors. watafute KILI SURVEYORS ambao ofisi zao kuu ziko Moshi lakini pia wana branch yao Arusha. Namba yao ni 0754-276324 mie walinisaidia kupima mpaka kupata HATI kamili lakini gharama zao kwa kiwanja kimoja ina cost mpaka mil moja hadi kupata HATI
 
Thanks bro

Back
Top Bottom