Utaratibu na gharama za kupata hatimiliki ya nyumba/kiwanja

Habari wana JamiiFrm.
Naombeni msaada,mimi ni mkazi wa Arusha,nina kiwanja changu chenye vyumba vyangu ila wakati wa kununua nilimtumia mchumba wangu akailipie kiwanja kwa jina lake.
Nataka nikiwekee hati miliki ya kiwanja hicho na nyumba yake.
Naomba mwenyekujua anijuze njia ya kufanya na Garama ya kutimiza lengo hilo.
NAMALIZIA KWA KUWASHUKURU,
ASANTENI
Nawakilisha kwenu kwa msaada.

Pole sana mleta mada hii.Nianze kwa kusema kuwa wewe na mchumba wako hamkuwa na makubaliano ya kisheria kuweza wewe kumwamini na kununua kiwanja ambachao mlikubaliana kiandkikwe jina la mchumba wako.Kwa ufupi wewe huna haki juu ya kiwanja hicho.Mwenye haki ni mchumba ni wako.Wachumba hawatambuliki kisheria kama wana ndoa,zaidi itajulikana kama ni marafiki wa kawaida.

Kama nilivyosema awali wewe huna haki na kiwanja hicho isipokuwa kilichopo hapa ni wewe na mchumba wako kuaminana,ambapo huwezi kupata nguvu ya kisheria endapo mchumba wako akaamua kujimilikisha na kukutoa nje ya umiliki unaosema.Huna ushadi kuthibitisha kama kweli wewe ulitoa hela kununua kiwanja hicho.

Pili hujaeleza kwa kipindi hiki kama unaishi na mchumba wako kama mume na mke.Kama mmekwisha kuoana ama kwa sheria za mila au kwa sheria ya ndoa ya mwaka 1971.Basi unapashwa kukubaliana na mkeo (kama ni wanandoa) juu ya jambo hili na namna ya kuliweke.Jambo linawezekana na ni rahisi sana kufikia muafaka na hivyo kupata aidha umiliki wa pamoja(mume na mke) au umiliki wako binafsi(mume)
Sheria ya ardhi iko wazi kabisa ,tatizo ni urasimu wa watendaji wetu,nashauri kwanza uwe na hati ya mauziano ya kiwanja hicho,pili upate muhtasari wa serikali ya kijiji au mtaa,tatu eneo lako lipimwe (watu wa ardhi au wanaotambulika kisheria) na kukewa bicons ili liweze kuingizwa katika ramani ya mji.Baada ya mambo haya kukamilika,utapata offer ya kiwanja ambayo kama mtakuwa mmekubaliana na mchumba wako/mke itakuwa kwa majina ya wote wawili au jina lako pekee.

Offer hiyo itakuwa na masharti fulani ikiwa ni pamoja na kuliendeleza eneo hilo,kitu ambacho wewe umekifanya tayari.

Kama offer utakuwa nayo,basi utapewa aidha faili lako kutoka ofisi za ardhi ili uende nalo au litatumwa Moshi ambako offer hiyo itasajiliwa na Kamishina wa Ardhi kanda,na baaada ya siku kama tatu hadi wiki moja utapata Title Deed unayoitaka. Kumbuka Moshi hakuana ushuru au kitu cha kulipia, ni bure. Kila kitu utakuwa umelipia katika ofisi za Ardhi kabla ya kwenda Moshi.

Aidha mchakato huu wote unahitaji hela hasa hasa katika upimaji wa eneo lako.Kama utaona gharama ni kubwa jaribu kutafuta marafiki wenye uhitaji wa kupimiwa maeneo yao walio karibu na wewe ili muweze kuchangia gharama hizo. Hivyo jiandae kwa gharama hizo.
 
wana Jamii,

Nimenunua kuwanja mahali, nimeshakamilisha taratinu zote za kubadilisha jina... sasa nataka kupata hati. Nimesikia huwa ni bure lakn kuna gharama kidogo. Nimeongea na maafisa ardhi wa sehemu husika wakaniambia natakiwa kulipa lak 350, sasa nataka mweneye kujua proper channel, nisije nikaingia mkenge na maafisa wetu wanaofanya ofisi zao ni duka
 
Zina risiti? Manake aridhi napo naona wamejazana watu kibao sijui wanafanya nini kazi utapeli tu, hata kakitu kadogo utasikia sio chini ya laki, na kazi ya siku inaweza chukua miezi au zaidi ya mwaka. Aridhi kwenye Manispaa na Wizarani ni zaidi ya janga la kitaifa!
 
Umesema umekamilisha zoezi la kubadilisha jina (swali langu ulichobadilisha jina ni nini mkuu, letter offer au nini?). Kwa uzoefu tu maafisa wa ardhi hawahusiki na kutoa hati, anaehusika kutoa hati ni kamishina wa ardhi. Labda ungenijibu swali langu hapo kwenye blue pia nijue upo mikoani au upo Dar (maana Dar kuna complication sana kutokana na wizara ya ardhi kujiingiza kwenye kuuza viwanja kama ilivyo Dodoma inavyofanya CDA mwisho wa siku katika hii mikoa miwili kuna mgongano wa kimaslahi na manispaa husika zinazopaswa kuuza)
 
Wizara inatakiwa kuratibu tu kwani ardhi ni mali ya manispaa kuanzia kulipa fidia, kupima mpaka kuuza, sasa kwa Dar kwa kuwa wizara ipo hapo wamejipa majukumu ambayo sio yao na ndio mwanzo wa matatizo.
 
Umesema umekamilisha zoezi la kubadilisha jina (swali langu ulichobadilisha jina ni nini mkuu, letter offer au nini?). Kwa uzoefu tu maafisa wa ardhi hawahusiki na kutoa hati, anaehusika kutoa hati ni kamishina wa ardhi. Labda ungenijibu swali langu hapo kwenye blue pia nijue upo mikoani au upo Dar (maana Dar kuna complication sana kutokana na wizara ya ardhi kujiingiza kwenye kuuza viwanja kama ilivyo Dodoma inavyofanya CDA mwisho wa siku katika hii mikoa miwili kuna mgongano wa kimaslahi na manispaa husika zinazopaswa kuuza)

Asante kwa quick reply Mkuu, niko Morogoro.. nilichobadili jina ni Letter of Offer (kwa hiyo nikilipa kodi inakuja kwa jina langu sio la muuzaji
 
Asante kwa quick reply Mkuu, niko Morogoro.. nilichobadili jina ni Letter of Offer (kwa hiyo nikilipa kodi inakuja kwa jina langu sio la muuzaji

Kama umepata letter of offer maana yake kwamba hapo ofisi ya ardhi ya manispaa wanaandaa file mbili ambazo zote zinafanana yaani moja copy yako na nyingine nadhani itabaki kwa upande wa serikali imeandikwa CERTIFICATE OF OCCUPACY (Under section 29), THE LAND ACT, 1999 (NO. 4 OF 1999) ambazo watakupa uzipeleke kwa mwanasheria kuthibitisha kwamba wewe umekubali terms and condition kisha unarudisha manispaa ambao watazipeleka (au unapeleka mwenyewe) ofisi ya Kamashina wa ardhi ambapo utalipa stamp duty sh. 500 (mia tano ambayo hata hivyo itakuwa tayari imelipwa wakati kiwanja kinanunuliwa kama inavyoonekana hapo chini) kisha unaandikishwa kwenye daftari na kupewa siku maalumu ya kurudi kuona kama hiyo CERTIFICATE OF OCCUPANCY (ndio hati yenyewe) kama imesainiwa na kamishina wa ardhi pia inabandikwa na ramani ndogo ya viwanja vilivyopo eneo lako of which cha kwako kinawekewa alama nyekundu plus namba ya hati, ukubwa na vitu kama hivyo. Kama ikishasainiwa tu unapewa hati yako kabisa na unasepa zako

hiyo laki 350,000 hapo ni utata kwani gharama ya kiwanja hicho ime-include mambo mengi, embu check letter of offer yako uone jinsi mchanganuo wa gharama ya kiwanja kama ilivyo kwa mnunuzi wa kwanza, ukicheck utaona kuna

- Premium (hiyo ndio gharama ya kiwanja wanakuwa wameweka amount
- Fees for certificate of occupancy ambayo ni 3000 ila hata kama imepanda haiwezi kuwa juu sana (hii ilikuwa 2006)
- Registration fees ni 2106
- Survey fees 24,570
- Deed Plan fees 6,000
- Stamp duty on Certificate and Duplicate 1,000
- Land rent ya mwaka ambao amenunua kiwanja 11,000 (baada ya hapo kila July mhusika unakwenda kulipa
Hivyo ukijumlisha zote kuanzia premium mpaka hizo gharama nilizokuonyesha unapata gharama halisi ya kiwanja na ipo indicated kwenye letter of offer. Let say, kama gharama ya kiwanja ni milion moja (ambayo ndio imeandikwa premium kwenye letter of offer) maana yake gharama ya kiwanja jumlisha hizo cost ndogondogo.

Ukisoma hivyo vigharama utagundua kila kitu kilishalipiwa na mnunuzi wa kwanza ambapo kimsingi kilichofanyika ni kubadili jina tu condition zingine zinabaki vilevile, so hati ni bure in this case unless taratibu ziwe zimebadilika, gharama ambayo utaingia ni hiyo ya mwanasheria ambayo ukienda utalipa labda mwekundu anagonga mhuri na kupiga sahihi na wewe unapiga sahihi mbele yake.

Tafuta ofisi ya kamishina wa ardhi, huwa zipo kikanda upate taratibu, sasa kwa Morogoro sijui watakuwa na ofisi hapo au mtakuwa mnahudumiwa na Dar ili upate mwongozo maana watu wa idara ya ardhi sio
 
Alhamdulilah na Leo nimejifunza jambo jipya kupitia JF. Asante sana wadau,

Sent from my Nokia 8310 using Tapatalk
 
Pamoja na maelezo Mazuri yaliyotolewa na Jodoki, lakini hizo longo longo za njoo kesho, ukifika kesho unaambiwa uje wiki ijayo utakazokutana nazo huko ofisi ya msajili wa hati utaona bora utoe rushwa ili upate hiyo hati mapema , kwahiyo kimsingi haitakuwa bure.
 
mkuu jodoki narudi kwako kwa ushauri zaidi nimeuziwa kiwanja na mndengereko fulani maeneo ya kimanzichana ,nikamlipa jumla ya sh.4m mbele ya mwandishi wa umma ,mkataba nilionao ni huu wa mwandishi wa umma ,nahitaji hati wapi pa kuanzia na wapi pa kuishia .
 
Ni kweli mkuu hapo bolded ila kinachotakiwa ni uvumilivu tu kwani mtu akikuomba rushwa unampotezea tu kwani hati ni haki yako pia hata kama ataleta urasimu lakini mwisho wa siku ataachia kwani ukiwa na letter of offer na kiwanja unalipia kila mwaka hicho ni mali yako ila hati yenyewe ni ya kisheria zaidi hata wakikaa nayo watajiju yaani ni sawa na umemaliza chuo alafu ukapewa Transcript (hii nachukulia mfano wa letter of offer) alafu baada ya muda unafuatilia cheti (hii ndio kama mfano wa hati sasa na kwa msingi huo hata mtu akubanie kukupa hati mwisho wa siku lazima atoe. Hata kama kuombwa rushwa sio hiyo laki 3.5 sana sana labda aseme alfu 30 ili achakachue uonekane umefuatilia siku nyingi kumbe una haraka zako kwani hicho ni kiwanja chako hata afanye nini hati lazima atoe , ingekuwa kwa wazee wa ardhi unataka kiwanja hapo kama kawaida yao wangetaka zaidi ya laki 3 but since tayari una offer yaani kama una shughuli zako unaendelea ukipata nafasi unakwenda kucheck hati yako hakuna haja ya kujipelekesha. Kwa Mwanza ukifika unakutana na notice board ya majina ambayo hati zao tayari na kama hujakuta unaingia ofisi husika kuulizia kulikoni (ni zoezi la kama miezi 2 mpaka 3 unapata hati yako.
 
mkuu jodoki narudi kwako kwa ushauri zaidi nimeuziwa kiwanja na mndengereko fulani maeneo ya kimanzichana ,nikamlipa jumla ya sh.4m mbele ya mwandishi wa umma ,mkataba nilionao ni huu wa mwandishi wa umma ,nahitaji hati wapi pa kuanzia na wapi pa kuishia .

Tatizo mkoa wa Pwani, A town na Dar ardhi ipo mikononi mwa watu ili mradi usinunue ardhi katika hifadhi ya barabara na maeneo kama ya jeshi, tofauti na mikoa mingine kunakuwa na master plan ya mji mzima hata kama maeneo mengine ardhi haijapimwa lakini bado kwenye master plan inaonyesha hayo ni maeneo ya makazi au viwanda hivyo yanakuwepo tu pindi wakipata hela ya fidia wanakuja kuwapa wahusika wenye maeneo na kupima viwanja kwa ajili ya kuuza. Ila hata kama hawajaja kulipa fidia unachofanya ni kumuita mtu wa manispaa / jiji ili ujue kama eneo hilo ni la makazi ya watu kisha hatua inayofuata ni kupimisha hilo eneo (kuna gharama hapa tena kwa huko walivyo wasanii ndio usiseme, ila sehemu nyingi kupima eneo 3m) kama huna hela za kupimisha na master plan inaonyesha ni eneo la makazi unachofanya ni kujenga kisha kinachofanyika ni upimaji shirikishi.

Kwa Dar sasa 75% ya jiji ni unplanned hivyo kila mtu anajenga tu anavyotaka na watu wa ardhi wanafanya kazi kwa mazoea hivyo ni kwenda hivyo hivyo tu ili mradi tunafika na ndio maana kwa kutambua hilo ikabidi waje na leseni ya makazi. (kwahiyo process ni kama nilivyoelezea hapo juu though kwa kanda ya mashariki kidogo utaratibu wa ardhi upo complicated kidogo maana hata mie nina kaeneo kangu maeneo ya Kimara temboni mambo ni yale yale watu wanajijengea tu kikubwa kuna muhuri mwenyekiti wa mtaa na shahidi mjumbe, though angalau mwaka juzi walitoa namba kwenye hivyo viwanja tulivyonunua kienyeji wakasema wanapeleka wizarani but no response.)
 
Mkuu Jodoki nakushukuru sana kwa ufafanuzi mzuri hivyo sasa nimejua nini cha kufanya na kwa muda gani ili kupata hati.

Poa mkuu ila hakuna consistency kati ya mkoa mmoja na mwingine, ila nunua maeneo as much as you can kikubwa ni kuhakikisha hayo maeneo ni kwa ajili ya makazi (unachotakiwa ni kuwasiliana tu na watu wa ardhi wakusaidie kuangalia master plan ya mji maana unaweza nunua eneo limetengwa kwa ajili ya jeshi)
 
Mkuu asante kwa majibu mazuri,
Mimi nina kiwanja hapa Dar. Maeneo ni karibu na kinyerez ambako kumepimwa aka mradi. Hapo kwangu hapaja pimwa.
Kuna kajamaa fulani ka ardhi kananiambia pale kwangu supa. Mchoro upo ila unahitaji urekebishwe kidogo, sijui kivipi. Lakini ishu ni hivi, kuna mzee alikua na mashmba yake halafu yeye akayakata katika mfumo wa viwanja standard halafu anauza.
Sasa haka kajamaa ka ardhi cjakaelewa kanamaanisha nini kuhusu kurekebisha mchoro. Yaaani nakaita kajamaa coz nakaogopa na nakaona kananuka rushwa. Hata kakinieleza jambo linaingia sikio hili linatokea sikio lingine.
Je wewe unaonaje maelezo ya haka kajamaa?!
Na je nikitaka nishughulikie kila kitu nipate hati kwa haraka (within 6months) nijiandae total shs ngapi? (+kifutajasho kwa wanaonishghulikia)!
Ni kweli siku hizi hakuna mambo ya kupata offer, ni unapata hati moja kwa moja?
 
Tripo9;

Kinachorekebishwa I think ni kiwanja na si mchoro kwa kuwa mchoro tayari umeonyesha miundombinu ya mbalimbali kama barabara n.k

Kinachofanyika ni kukinyoosha tu kwa kuweka becon ili iendane na mchoro wa eneo zima though kinaweza kikamegwa kidogo ili kuonyesha barabara au kisimegwe kabisa kama waliouza / uongozi wa eneo waliweka barabara za asili ambazo watu wa ardhi huzifuata kikubwa ni makubaliano na wananchi na kama zitakuwa zimekaa fresh.

Hapo kama umejenga tayari nadhani utaangukia katika upimaji shirikishi ambapo wakazi wa eneo moja wanajikusanya kwa pamoja na kulipa kiasi flani cha fedha kuchangia zoezi la upatikani wa hati (sidhani kama inazidi laki 2 mwenye data atatupa ila mnakuwa kikundi wakija kupima wanakuja kupima eneo kubwa vinginevyo kama una hela zako ndio hiyo 3m)
 
Last edited by a moderator:
Jodoki Kalimilo;

nashukuru mkuu kwa majibu mazuri swali la nyongeza ,je una fahamu chochote h=kuhusu hizi hati za kimila zinatolewaje na wapi pa kuanzia .swali la pili ,upimaji shirikishi nimeupenda zaidi ni nyumba ngapi zinatakiwa ili tuweze kumuita afisa ardhi kwa ajili ya upimaji .
 
Hapo blue sipo aware ila nahisi hati za kimila kama zipo applicable vijijini vile? upimaji shirikishi ni kuji-organize watu wote wenye majengo katika eneo husika na kuwafuatilia hawa watu ardhi nadhani kwa Kinyerezi itakuwa Ilala kama sijakosea au wizaeani kabisa maana kwa Dar even watu wa wizarani nao wanajihusisha na hii kitu. Sidhani kama kuna idadi maalumu kikubwa hata kama mpo kumi na kuendelea mnaweza kuanzisha move wengine watafuata
 
Back
Top Bottom