Utapeli Kariakoo: Kuna tofauti kubwa sana kati ya kusoma na kuwa na akili nyingi. Kuna watu waliishia darasa la saba (7) tu kwa sababu ya umasikini

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
S.hikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu Watanzania;

Kuna tofauti kubwa sana kati ya kusoma na kuwa na akili nyingi. Kuna watu waliishia darasa la (7) tu kwa sababu ya umasikini wa nyumbani kwao wakashindwa kuendelea na masomo.

Kuna watu hawajasoma sana (unakuta mtu ameishia darasa la saba tu mwaka 1991) ila wana akili sana hata ukikutana nao mtaani katika maisha ya kila siku.

Namna wanavyopangilia kazi zao au hata ratiba zao za kila siku, unajua kabisa huyu mwamba aliishia darasa la 7 kwa sababu ya umasikini tu na kama angesoma sana angekuwa mtu mmoja hatari kweli kweli.

Wewe jenga picha wale wezi wa pale kariakoo wanakuibia mfukoni bila hata wewe kujua kama kuna mkono umeingia ndani ya mfuko wako wa suruali na kuchukua pesa yako ya dagaa. Zile ni akili nyingi sana sema tu zimeelekezwa pahala pasipo stahili.

KISA KIDOGO CHA MIMI KUUZIWA KIPANDE CHA SABUNI KWA 20,000/= NIKIDHANIA NI SIMU
===========
Nikiwa kidato cha 6 miaka hiyo ya 2000 na kitu, niliwahi kuuziwa kipande kidogo cha sabuni nikidhani kuwa ni simu.

Nilikuwa ninatoka Tabata Segerea nyumbani mama yangu mkubwa nilienda kumtembelea siku ya ijumaa jioni sasa nikawa ninarudi jumapili mchana ili nifanye maandalizi ya usafi wa nguo kwa ajili ya shule kesho yake ambayo ni Jumatatu.

Baada ya kushuka kutoka katika daladala pale mtaa wa Kongo akatokea jamaa mmoja rika langu akiwa ameshika simu aina ya nokia zile za jeneza za zamani akawa ananioneshea kwa ukaribu basi mimi nikaichukua ile simu nikaikagua vema kisha nikamuuliza bei gani, yeye akasema ni 20,000/=. Nikasema kimoyomoyo poa ngoja nichukue hii ngoma ili na mimi nikatambe huko mitaani.

Alafu hiyo pesa yenyewe sasa ndio nilikuwa nimepewa kama pocket money ya mwezi mzima na huyo mama yangu mkubwa.

Yule jamaa rika langu kabisa akaniambia mwamba njoo huku hapo barabarani sana, basi mimi nikaenda, akanipa tena simu nikaikagua kwa mara ya pili, simu ipo sawa haina tatizo.

Sawa. Basi mwamba akaichukua simu akaiweka katika bahasha fulani hivi ya kaki kisha na mimi nikampa pesa yake 20,000/= huyo nikaondoka.

Kabla sijaenda mbali, baada ya kupanda daladala za kwenda home kwetu kurasini huku Dar, nikaona ngoja nifungue bahasha nitoe simu yangu walau nicheze hata game la nyoka niji-keep busy, halooooo!

Nilikutana na kipande cha sabuni ya kodrai hahahahahaaaaa size ile ile kama simu ya Nokia ya jeneza (3310) kikiwa kinaniangalia tu. Kwa kweli roho iliniuma sana.

Ukizingatia 20,000/= ni pesa nyingi sana kwa miaka ile alafu mimi bado mwanafunzi sina majukumu mengi.

Basi sikuwa na jinsi zaidi ya kuvumilia hasira nilizokuwa nazo na nilipofika home nikafua nguo zangu kwa kutumia sabuni ya kipande ya 20,000/= hahahahaa.
===========

Kuna watu wenye akili nyingi lakini hawajasoma sana hususan huko vijijini. Unakuta mwanakijiji yeye hawajawahi kuwa na njaa bomani kwake.

Miaka yote anavuna mahindi mengi, anafuga ng'ombe wake vizuri na anasomesha watoto kwa kuuza maziwa tu mpaka watoto wanamaliza form six. Siku akiamua kukuandikia barua, huo muandiko wake utadhani labda ni mwalimu wa secondary.

Kuna watu hawajasoma sana ila wana akili nyingi kweli. Je, ulishawahi kukutana nao (mbali na wizi) katika maisha yako?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO. MUNGU IBARIKI NCHI YANGU.
 
Mimi niliuziwa kipande cha sabuni pia.,
kisa kinaendana na chako.

Ila kisa fulani naweza nikasema ni experience tu ndio inawafanya waonekane kuwa ni wataalam wa kuwaibia watu, muda mwengine hutumia sayansi kidogo.

mfano ubongo wa mwanaume hauwezi kutafsiri mambo mawili kwa wakati mmoja, wanawake wanaweza ila si zaidi ya vitu vitatu.

wanachezaje na hii saikolojia?
Siku 1 nipo mitaa ya Tandika, nipo nimeweka wallet mfuko wa nyuma, si unajua tena Tandika foleni ya watu kupishana kwa tabu..baasi mbele yangu alikuwepo mzee fulani hivi napishana nae akajigongesha kwangu huku akiugulia maumivu kuwa nimemuumiza basi kanishika bega ananitingisha sina hili wala lile akili yangu namhurumia yule mzee na kumpa pole na kumwambia samahani ni bahati mbaya watu ni wengi...kumbe kile kitendo cha kunitingisha, akili yangu anaifanya iwaze jambo moja, huku mfuko wa nyuma naibiwa sina habari maskini. Nilivyomuacha kwenda mbele kidogo najipapasa hamna kitu, nilicheka sana maana nilipata funzo, japo hazikuwa pesa nyingi sana.

Mwizi anaweza akakupiga kofi la uso, na akakunyang'anya simu yako au mkoba (kwa wadada) maana akili yako itasikiliza kofi ukija stuka kashasepa...

Akili zetu haziwezi tafsiri mambo mawil kwa wakati mmoja, wezi wengi ndio hutumia hii mbinu.
 
Na ule wa dirishani unaupa asilimia ngapi?

Kuna siku nilikua nimepanga ku-download windows sasa nikakumbuka offer ya ya usiki kutoka halotel yenye unlimited data

Majira ya usiku kama saa tisa hivi hapo speed imechanganya inaenda mpaka 5mbps ikanibidi nilale.

nikamuachia usukani brother yangu aendelee ku monitor si unajua sometimes network na servers zinazingua unakuta dowload files zina stop kwaiyo hapo itakubidi uwe karibu u-resume

Nilikua nime connect internet kwenye pc kupitia simu kwa njia ya wireless halafu ile simu nilikua nimeichomeka chaji kupitia usb port ya pc nikawa nimeiweka juu ya keybord, na pia kulikua na kisimu cha keypad cha tecno kilikua nacho nimekiweka hapo hapo kwenye keyboard

Nikajikuta nimestuka majira ya saa 11, kucheki internet signal naona alama ya ❌ Kuangalia pale kwenye keybord ya laptop sioni simu, naona usb cable inabembea chini bila simu

Nikaanza kuitafuta huku nikiwaza pengine itakua ilianguka chini lakini sikuweza kuipata. Hapo nikapata wazo la kuchukua simu ile ndogo ili niipige niskie itapoitia niichukue kiulaini, nashangaa nayo simu ndogo haipo.

Ikabidi nimuamshe bro tusaidiane maana ishu ishakua heavy, katika harakati za kutafuta tukafunua pazia tukaona kuna tobo kwenye wavu

Distance ya kutoka dirishani mpaka mezani ambapo tuliweka pc ilikua ni umbali wa futi 9 au kumi, na hapo ndipo nilipoamini kua hii kumkwepa mwizi ni ngumu.
 
Back
Top Bottom