Utafiti mpya wa kisayansi wa Covid19 – Msaada mkubwa wa kujikinga na kuzuia maambukizi kwa wengine

Dr Mathew Togolani Mndeme

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
201
808
Watafiti wa vyuo vikuu na taasisi kadhaa za utafiti wa magonjwa ya mlipuko nchini Marekani, wamechapisha utafiti mpya wa kimaabara unaotoa mwanga mkubwa wa namna virusi wa Covid19 wanavyasambaa na kuambukizwa kutoka mtu mmoja hadi mwingine (UKO HAPA). Kwa kuwa sio kila mtu anasoma machapisho ya kisayansi, ninaomba nijaribu kutoa ufupisho wa matokeo ya utafiti huu na tafsiri yake ya namna yanatusaidia katika kupambana na mlipuko wa Covid19.

Kwa kuanzia, ili kuelewa utafiti huu, chukulia unapuliza Doom (spray) kuua wadudu au unapuliza spray ya kuleta harufu nzuri kwenye chumba/nyumba (air refresher). Tunapopuliza spray hizi hutoa matone madogomadogo kama ya maji yanayobaki hewani au kwenye uso wa kitu ulichopulizia kwa muda kufanya kazi kusudiwa (kuua wadudu au kuleta harufu nzuri). Kwa lugha ya kikoloni matone haya huitwa “Aerosols” ila kwa malengo ya ufafanuzi huu sisi tuite tu kizaramo kwamba ni matone.

Mtu anapokohoa au kupiga chafya matone (mate, makohozi au kamasi) hubaki ama hewani au kwenye kitu yalipoangukia kwa muda na kua chanzo cha maambukizi ya Covid19. Utafiti huu mpya umegundua yafuatayo kuhusu uwezo wa virusi wanasababisha Covid19 kuendelea kuwa hai na ambukizi pale matoke yanapokua hewani (aerosol transmission) au yanapoangukia kwenye uso wa kitu (surface/fomite transmission):
  • Matone ya Covid19 yakiwa ndani ya nyumba (closed doors), virusi hao wanabaki hewani wakiwa hai na ambukizi kwa hadi masaa 3.
  • Matone yakiangukia kwenye kitu cha plastiski (polypropylene) au chuma (stainless steel), virusi wanakua hai na ambukizi kwa hadi masaa 72 (siku 3).
  • Matone yakiangukia kwenye kitu kilichotengenezwa kwa mbao (cardboard), virusi wanakua hai na ambukizi hadi masaa 24 (siku moja).
  • Matone yakiangukia kwenye kitu kilichotengenezwa kwa shaba (copper) virusi wanakua hai na uwezo wa kuambukiza kwa hadi masaa 4.
  • Popote matone yanapokuwepo, virusi wa Covid19 hawafi mara moja kama vile mtu anapokata roho muda unapofika. Virusi hawa hukata roho kwa mfumo unajulikana kisayansi kama “half-life decay” (sina neno la kizaramo). Ila kwa kifupi, wanakufa nusunusu au wanaoza hadi wanapoangamia kabisa. Kwa mfano, kwenye uso wa plastiki virusi wanakufa au kaoza nusunusu kila baada ya masaa 6 dakika 48 (half-life time is 6.8 hours) hadi siku ya 3 kukamilika fungu la mwisho la virusi wanakua wamekufa.
Nini maana ya half-life decay (kufa/kuoza nusunusu)?
Ukitaka kuelewa dhana ya kufa nusunusu chukulia virusi wa Covid19 ni chungwa. Sasa chukua chungwa kaa nalo kwa masaa 6 dakika 48 kisha likate nusu. Tupa nusu moja (imekufa/ imeoza) ubaki na moja (hai). Baada ya muda mwingine kama huohuo ile nusu hai uikate tena nusu (unabaki na robo hai) kisha tupa robo nyingine (imekufa/imeoza). Endelea hivyohivyo hadi kipande cha mwisho ushindwe kabisa kukikata kwa uwembamba wake na hivyo kukitupa. Ukifikia hatua hiyo utakua umefikisha siku 3 (yaani virusi wote wamekufa).

Nini tafsiri ya utafiti huu na unatusidiaje kupambana Covid19
  1. Utafiti huu unatupa mwanga zaidi kuhusu maambukizi ya Covid19 na kutueleza ni kwa nini unaambukiza kwa haraka. Pia unatueleza ni kwa nini imekua vigumu kudhibiti maambukizi ya Covid19. Kwa mfano, tukipanda basi pale Kimara Mwisho tunaelekea posta, kisha kukawa na mtu ambaye ana Covid19 bila kujijua akakohoa au kupiga chafya (mara moja tu), basi kuna uwezekano mkubwa watu wengi watagongana na matone hata wale watakaopanda baadaye pale Ubungo au Manzese. Ikitokea hilo wanaweza kuambukizwa (usitishike ni mfano tu). Pia watakaoshika viti, chuma au eneo lolote la basi ambapo matoke yamedondokea, wataondoka na virusi mikononi na watakapojishika usoni basi watakua wamewakaribisha kupia kinywa, macho au puani.

    Hivyo basi, utafiti huu unatuonesha kwa nini ni muhim sana mtu mwenye Covid19 anapokua karibu na watu wengine avae mask. Pia, kwa kuwa hatufahamiani nani anao, basi ni vema tunapoongea tuwe na umbali wa kadiri ili matone yanayotoka mtu anapoongea (na wengine kama mimi huwa yanatoka kwelikweli) yasikufikie.

    Kwenye hili, niwasisitize vongozi wetu wanapokua wanaongea na vyombo vya habari wakiambatana na timu yao ya wataalamu na viongozi wenzao, wasikaribiane sana. Hadi sasa viongozi wa nchi kadhaa waliokua ndio wasemaji wakuu wa ugonjwa huu, wameathirika na wengine wamelala mauti na huenda waliambukizwa kwa njia hii.

  2. Utafiti huu unaendelea kuthibitisha ni kwa nini kujitenga (social distancing and isolation) kwa mtu aliyeathirika ni njia muhimu sana ya kudhibiti maambukizi kwa wengine. Sio tu kwamba baada ya siku 7 hadi 14 atakua kapona kama hana hali mbaya ya kutibiwa hospitali, bali chumba au nyumba atakayokua amejitenga haitakua na virusi kwa kuwa muda wao wa kuendelea kuwa hai utakua umeshapita kwa kifo cha kinusunusu.

  3. Utafiti huu unaendelea kutukumbusha umuhim wa kutoshikashika maeneo yoyote ambayo watu wengine wanashika kama vile milango ya nyumba na magari, chooni, ngazi, viti, reli za kwenye ngazi, nk. Hii ni ngumu sana kuepuka lakini inapowezekana jitahidi usishike maana huenda kuna kafungu ka vikorona ndio kwanza vimekufa robo tatu vimebaki robo moja na utaondoka nao.

  4. Utafiti huu unatusisitiza umuhim wa kujitahidi kunawa mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka kila unaposhika mahali wanaposhika watu wengine au kutumia kitu ambacho kimetumiwa na watu wengine. Baada ya kunawa jitahidi kujifuta na tissue na kuitupa au kutumia taulo safi ambayo una hakika ni wewe mwenyewe unaishika. Ikishindikana usijifute baada ya kunawa (hata kwa nguo ulizovaa). Kung'uta mikono iache ikauke.
Mwisho
Ninaomba unisamehe kwa lugha ya kizaramo isiyo rasmi niliyotumia hapa. Ni ngumu sana kutafisiri maandiko ya kisayansi yaliyo katika lugha ya kikoloni kwenda kwenye lugha ya kizaramo na ukaeleweka hasa unapokua kwenye kiwewe cha korona. Bado ninajifunza.

Imeandikwa na Mathew Mndeme (mmtogolani@gmail.com)
Mwanasayansi/Mtafiti wa mifumo ya digitali kwenye ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza
 
"Kufa Nusu Nusu" kunahitaji ufafanuzi zaidi kuliko ulivyotolewa ili kueleweke vizuri.

Badala ya kutumia mfano wa chungwa, heri ungetumia vitu vinavyohesabika, kama mbuzi, kuku, ng'ombe, n.k.

Hebu jaribu na kuku. Watu wengi hufuga kuku, na mara nyingi kuku hao hupata magonjwa pia, ingawaje hawafi kwa pamoja kama huko kwa "kufa nusu nusu"

Kumbuka, corona ni 'particle' (vipande?) vyenye umbile dogo sana, sijaangalia, lakini nadhani ni chini ya 'micrometer' moja, wao wako kwenye 'nanoparticle' (nanometer).

Kwa hiyo ki-'spray' kimoja tu, ambacho nacho ni kidogo kabisa, kama 'micron' hivi, kinauwezo wa kubeba hao corona maelfu.

Basi tuchukulie, hicho ki'spray' (kitone) kimoja tu kiwe na corona 100 (hesabu kama kuku mia moja).

Anzia hapa kujua maana ya "kufa nusunusu"

Tuseme hili tone (spray), kule kutoka tu mwilini mwa mgonjwa kwa kupiga chafya, liwe limeangukia kwenye meza ya mbao, ambayo mleta mada hapo juu, kabainisha kwamba uhai wa hawa corona huchukua msaa (?) - naona mfano huu mwandishi hakuutolea half-life yake.
Basi tuchukue ule wa 'plastiki' ambao ni masaa sita na dakika 48:

Maana ya hii ni kwamba, lile tone lenye corona 100 (kuku 100); likishatimiza masaa 6:48 corona watakaokuwa wamekufa wakati huo watakuwa 50, waliobaki hai 50. Hawa hamsini ambao bado wapo hai, kama mazingira yanaruhusu, wataendelea kuambukiza.

Baada ya masaa mengine 6:48, kati ya wale 50 waliosalia, kati yao 25 watakuwa wamekufa tayari, lakini bado wapo 25 wapo hai, na wanaweza kuambukiza baada ya masaa 13:na ushee tokea tone litue pale kwenye ile plastiki..
Baada ya masaa mengine 6:48, kati ya wale 25, corona 12 bado watakuwa na uhai - hii ni baada ya masaa takribani 19 - 20 tokea lile tone la mwanzo litue.

Baada ya masaa mengine 6:48, wale corona 12 waliosalia, sas hivi ni corona 6 tu ndio bado wapo hai na wanaweza kuambukiza.

Tayari ni zaidi ya masaa 26 tokea yule mgonjwa alipopiga chafya na tone lenye corona 100 kutua kwenye plastiki. Sasa hivi waliosalia hai ni wangapi baada ya masaa 6:48 zifuatazo?---------------?

Lakini kumbuka: hali ya lile tone haiwezi kuendelea kuwa na mazingira rafiki kwa uhai wa hao corona watakaokuwa wamesalia kwenye ngazi mbali mbali za "kufa kwao nusu nusu"

Ule unyevunyevu tu wa lile tone utakuwa umepungua kama sio kuisha kabisa. Ujoto, mionzi ya jua, n.k. vyote vitachangia kuua hawa corona na kuacha huo mfumo wa "kufa nusu nusu."

Kwa hiyo unaweza kukuta huku "kufa nusu nusu" kukaweza kuchukua mizunguko miwili au mitatu tu kumwezesha corona kuendelea kuwa hatari.

Kuna mengine humo aliyoandika mwandishi yanahitaji kurekebishwa, lakini hili ndilo la mhimu sasa hivi kueleza hiyo "kufa nusunusu"
 
Corona virus anayo "half life!??!"--- huyo bila shaka siyo kiumbe hai bali ni package ya chemikali ndiyo maana it undergoes the half life.
Ndiyo, hata kama sio kiumbe hai kama tujuavyo maana ya kuwa hai.
Huyu ni 'particcle' ambaye kiuhalisi ni 'protein' chenye uwezo wa kusababisha ugonjwa.

Kama 'protein' huathiriwa na kemikali na vitu mbalimbali, kama mionzi na kuharibu umbile lake na kusababisha kuondoa uwezo wake wa kusababisha magonjwa.

Chukulia mfano wa 'protein' (casein) iliyomo kwenye maziwa, hii inaweza kuathiriwa na kupoteza umbo lake na "kujikunata" (coagulate).

Au ulishawahi chemsha yai?
 
Hivi mkuu kwa mujibu wa utafiti huu huoni kuna haja kwa mtu asiyeambukizwa kuvaa respirator/mask ili kujikinga na aerosols kutoka kwa potentially infected person? Au unaunga mkono kauli ya yule Mama aliyesema waopaswa kuvaa maski ni walioambukizwa tu?

Je kwa mujibu wa utafiti ni umbali gani salama mtu akae kutoka kwenye "hot spot"?
 
Vipi kuhusu virusi vya corona vikidondokea keyboard za ATM zetu kwa siku si itakuwa majanga tuombe sana Mungu atuepushe na janga hili.

Eneo lolote linaloshikwa na zaidi ya mtu mmoja (pamoja na ATM) ni hatarishi kwa maambukizi. Na ndio mana dhana ya kukumbuka kunawa mikono mara kwa mara na kutojishika usoni inasisitizwa sana. Viko vitu vingi sana tunashika ambavyo sio rahisi kukumbuka vimeshikwa na wengine.

Kwa mfano, unakwenda supermarket/sokoni karibu kila unachokinunua (ili ukawe na akiba wakati wa mlipuko) kuna mtu/watu wamekishika na hujui hali zao. Hivyo una hatari ya kupeleka mlipuko nyumbani kupitia vitu unavyodhani ni vya kukusaidia kwa mlipuko. Dawa? Jilazimishe kukumbuka kunawa mikono kwa sabuni mara kwa mara na kutojishika usoni. Hakuna njia ya mkato.

Lakini zaidi ya yote hayo, ni kujikumbusha pia kuwa uoga dhidi ya Covid19 umekuzwa na HOFU kuliko uhalisia. Wasiwasi/panic ya kupata Covid19 imekuzwa kuliko ugonjwa wenyewe. Kama huna matatizo mengine ya kiafya (health conditions), huna haja ya kutembea na hofu ya Covid19 na kuogopa kila kinachokuzunguka.

Jiongeze kujikinga lakini maisha yaendelee bila hofu ya kujiona umezungukwa na kifo. Covid19 ni binamu yake na virusi wengine wengi ambao tuko nayo kila siku yanayoathiri mfumo wa kupua (respiratory system) kama vile mafua ya misimu na hatuogopi kufa. Haifikii ukali wa mjomba wake (Ebola) wala mashangazi kama malaria na kipindupindu.
 
Kalamu1,
Asante Kalamu1 kwa maelezo ya ziada na ufafanuzi. Lengo langu la kutumia chungwa ni kupata mfano mrahisi kabisa kumwelesha mtu yoyote ambaye anajisikia kizunguzungu anaposikia kauli za namba, hesabu, biotech na binamu zao.

Pia nitashukuru ukirebisha mengine uliyoona yana shida nami nijifunze zaidi. Na bila shaka utafanya hivyo baada ya kusoma publication niliyoitafsiri.
 
Hivi mkuu kwa mujibu wa utafiti huu huoni kuna haja kwa mtu asiyeambukizwa kuvaa respirator/mask ili kujikinga na aerosols kutoka kwa potentially infected person? Au unaunga mkono kauli ya yule Mama aliyesema waopaswa kuvaa maski ni walioambukizwa tu?

Je kwa mujibu wa utafiti ni umbali gani salama mtu akae kutoka kwenye "hot spot"?

Nikuulize swali jepesi. Covid19 ana kiherehere cha kutuvamia kupitia macho, pua na mdogo. Ukivaa mask kufunika mdomo na pua, je macho yanafunikwa na nini dhidi ya aersols ambazo ni ndogo sana na huzioni kwa macho? Huo usafi wa mask utauzingatiaje muda wote maana sio kifaa cha kuvaa kwa muda mrefu?

Jibu ni lilelile kwamba masks hazina msaada wowote kumkinga mtu kama wewe sio tabibu unayehudumia wagonjwa wa Covid19. Matabibu huzivaa pamoja na vifaa vingine vinavyofunika macho na sehemu nyingine za mwili.

Umbali unaoshauriwa kumkinga mtu iwapo anayeongea naye ameathirika ni wowote unaoweza kuwa salama lakini sio chini ya mita 2 au futi 6.
 
Nimesikia wapo wengi walioambukizwa ugonjwa huu lakini ni asymptomatic yani hawana zile dalili za mgonjwa wa Corona, na hawa ndio uaminika kuusambaza ugonjwa huu bila wao kufahamu na kuufanya uwe mgumu kudhibitika. Sasa maswali yangu ni haya.

Je, watu wote huonyesha dalili sawa au zinazofanana? na Je, inachukua muda gani tangu mtu kuambukizwa hadi kuonyesha dalili za ugonjwa?

Na ,Je, ni sehemu gani ya mwili hawa hukaa wakiisha muingia mtu, mapafu, kinywani, au hupenya kwenye blood system?

Mwisho nimesikia na kuona Trump akitangaza kwamba Chloroquine inatibu, je unaweza kutusaidia mechanism ya chloroquine kutibu virus wakati tunafahamu inatibu parasite wa malaria?
 
Kwenye half life kitu hakiwezi kubaki kilekile. Hubadilika na kuwa kitu kingine chenye asili nyingine.
 
Back
Top Bottom