Utafanya nini ukikuta picha, video au jambo lako la aibu limevuja mtandaoni?

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
Salaam ndugu zangu,

Katika harakati zetu za maisha tunakutana na tunafanya mambo mengi sana. Kuna baadhi ya matukio tunayoyafanya tunatamani yajulikane na mengine tunatamani yabaki kuwa siri.

Kutokana na kukua kwa teknolojia kwa sasa ni rahisi baadhi ya matukio yetu ya faragha kunaswa kwenye vifaa vya kidijitaji au taarifa zetu za siri kuvuja na kuenea mitandaoni.

Katika jamii yetu tumeshuhudia sisi wenyewe au watu wetu wa karibu wakiwa wahanga wa siri au taarifa zao za aibu kuvuja mtandaoni. Baadhi ya ndugu zetu au watu mashuhuri walichukua maamuzi magumu ya kujitenga na jamii zao au kujitoa uhai wakidhani ndiyo suluhu la tatizo hilo.

Je, ushawahi jiuliza utachukua uamuzi gani ikitokea umekutana na picha, video au taarifa zako za aibu zimesambaa mtandaoni?

Karibu tujadili

 
Vipi ikitokea umetegeshewa kamera bila kujua na ukakutana na picha au video zako mtandaoni. Utafanyaje?

Mbaka unakuwa target wa kurekodiwa tayari kuna mazingira mabaya umetengeneza. Tembea na pisi/masela wanaojielewa, nenda lodge za uhakika achana na lodge za elfu30. Piga show show hata ikitokea kwa bahati mbaya imevuja upate dili Brazzers au PH 🤣
 
Mpaka kufikia kujirekodi ina maanisha dhamira yako hasa ni hadhira. Sasa mtaka hadhira hachagui wahudhuriaji.

Ila ikitokea ikavuja, siri kubwa ni kutopaniki. Mara nyingi itakuwa ni issue kubwa siku mbili tatu baada ya hapo maisha yanaendelea.

Na wale watakaojifanya wakali sana katika hilo jambo elewa ndio waovu wakuu.
 
1. Kwanza usiruhusu mtu yeyote awe mke au mume au mpenzi arecord video mkiwa faragha.

2. Ikitokea kuna video inayokuhusu, kwanza usichangie chochote (nyamaza kimya) waseme wenyewe.

3. Angalia kama mtandao husika wanaweza kuifuta.

4. Angalia kama ipo namna ya kumjua muhusika na kumpeleka kwenye vyomba vya sheria kimya kimya

Muhimu;
Usichangie wala usikubali kuhojiwa na mtu yeyote (labda awe Polisi kwa ajili ya ushahidi) tofauti na hapo kataa kwani hao ndio watazidi kuitangaza
 
Me nitapasua simu
Umenikumbusha enzi zile za Facebook ndiyo inaanza Anza Miaka hiyo.

Kuna jamaa akamwambia demu wake aliyemtongoza huko fb amtumie picha yake ya mbususu,bibie kwa ushamba badala ya kutuma messenger akaweka profile ili mwamba aione. Baada ya kuweka mbususu profile picha kwa kujiamini akamtext jamaa tayari nimeshakutumia,jamaa akauliza iko wapi mbona siioni!? Dada wa watu akajibu angalia kwenye fb yangu.

Jamaa akakuta likitumbua alilotumiwa limejaa kwenye profile na watu wanatiririka kulaani "sasa ndiyo ujinga gani huu". Akamrudia demu wake "bibie futa haraka hiyo picha umeweka sehemu siyo, watu wanaona"

Wenge la demu badala ya kufuta picha si akalog out kwa kudhani ndiyo hataonekana. Mitandao hi hii tumetoka nayo mbali Sana.
 
Back
Top Bottom