Uso kwa uso na mke wa rafiki yangu gesti

Tabia ya wanaume kuchepuka naichukia sana...na ikija kwa mwanamke napo siipendi.

Sasa wewe kwanini haujamjibu kama hautaki kuongea kiutu uzima. Inaonekana nawe unataka kuonja...kwani ungemwambia nitasema au sitasema angefika huko? Subiria basi uone msg zenu zinabambwa ndio utajua tamaa mbaya...mjibu kuwa hautasema na mmalize maana na wewe utakamatwa tu arobaini yako ikifika.

wala asijaribu kumjibu kwa msg, amfuate nyumbani kwake, kumuonyesha heshima, amkabidhi pesa na kutamka, mimi sikuhukumu wala sintotamka, jiheshimu...only that,,, coz akianza na msg,,,,anaweza mgeuzia kibao kuwa jamaa alikuwa anamtaka na akahakikisha kauvunja urafiki wenu then aendelee kuchepuka.....
 
Mudishie pesa yake
mwambie huwezi kutembea nae
na mwambie unamuomba ajirekebishe ikitokea tena unaweza shindwa kukaa nayo moyoni....
but kwa kuwa wote ni watu wazima.....kila mtu atazame yake

You are the best man ever and your contributions which you have made here i wish it remain memories to many forever!
 
1.aisee mrudishie pesa zake
2.muheshimu kama shemeji yako,hivyo basi huwezi tembea naye.
3.mwambie hutamwambia rafiki yako ambaye ni mume wake
4.mwambie asirudie tena
5.nawewe acha uzinzi
 
Dah., ama kweli nyani halioni.....,,.,
wewe ni mwanaume kweli.?
 
Malizana naye kiutu uzima ili uwe silence daima mkutane tena hapo mlipokutana ili moyo wake uwe na amani.
Kula mzigo acha ubwege ww. Kamata fursa tekeleza wajibu uzembe haufai.msikilize anachotaka la sivyo atakuchukia mtakuwa maadui daima, na usiendelee kumuumiza moyo pia hapo ndio mwanzo wakupata pesa zisizo na risiti.
 
Kama angekuwa yeye amekuona na mchepuko wako ila wake hujamuona nadhani vice versa is true
 
Pesa rudisha, ila usijaribu kumalizana kama anavyotaka yeye eti mutenge muda....jaribu kumwambia ajirekebishe
 
Hahaha hahaha, mpeni ushauri
shauri nasema
vaswaili vanasena nyani oni kundule
yeye naacha Mke yake jumbani
nakimbilia chepuko,
kule nakuta mke ya rafiki chepuka
sasa natamani kotekote
goja nayeye firigisa iko siku kitu yake ya tigo
 
Husika na heading hapo juu,

Wakuu weekend iliyopita nilimuaga mke wangu kuwa nina semina nje ya Dar kikazi maana hiyo ndo huwa mbinu yangu ya kwenda kwenye dhambi zangu kwa siku tatu nne.

Nilikua nime import mchepuko wangu kutoka arusha so nika check in kwenye hotel moja Bagamoyo tukajipumzisha hapo alhamisi,Ijumaa, Jumamosi, jumapili asubuhi tuka check out.

Wakati nafunga mlango wa room nashtuka kumuona mke wa rafiki yangu akitoka chumba mkabala na changu akiongozana na zee moja hivi nao wakifunga chumba chao, shemeji alitetemeka na kupata mshtuko mkubwa hadi yule mzee kumuuliza kuna nini?

Mchepuko wangu ulishatangulia kwenye gari nikamsalimia shemeji nikamwambia mimi ndio na check out nilikua semina ya siku tatu ndo imeisha, akaitikia kwa kichwa tu, nikapiga hatua za haraka kwenda kwenye Gari ili asiuone mchepuko wangu ambao ulishatangulia kwenye gari.

Jumatatu akanipigia simu mwenyewe akaniambia shemeji naomba unifichie siri sitarudia tena. Nikamwambia naomba tuongee baadae kwa sasa nipo busy.

Mchana wake akanitumia meseji inasomeka hivi "" Shem naomba kama vipi tafuta sehemu nije tumalizane kiutu uzima and you stay silence forever "" naomba unijibu i can't afford to loose this marriage

Wakuu nipo njia panda, ingawa mimi ni mzinzi na sina utakatifu lakini siwezi kutembea na mke wa rafiki yangu kipenzi tulieshibana miaka nenda miaka Rudi na nilishawahi kukaa kwake sana wakati sijapata kazi yeye alianza kuja Dar es salaam kabla yangu.

Kwa sasa huyu jamaa yupo mkoani kikazi alihamishiwa huko mke alishindwa kumfuata kwa yeye mwenyewe ana kazi hapa Dar.Jana kanitumia M-PESA laki tano ikisindikizwa na msg kuwa vipi shemeji lile suala letu umeamuaje ukimya wako unaniumiza sikujibu kitu.

Wakuu naomba muongozo wenu. Kweli nisimwambie rafiki yangu kuhusu uzinzi wa mkewe? Na mimi ndio nimepewa jukumu la kumuangalizia familia yake kwa mambo mbali mbali kwa kuwa yupo mbali.

Nawasikiliza wakuu
Wewe Mzinzi na yeye mzinzi, sasa hapo unaumia kitu gani? Muonye asirudie tena na wewe baki njia kuu.Acha kuchepuka.
 
Mtafune tu maana inaonekana hamtofautiani, wewe na yeye ni kama pipa na mfuniko.
 
Wewe unatakaje?????? wewe mwenyewe mzinzi alafu unamtishia mwenzio, MWAMBIE yameisha ajirekebishe na wewe jirekebishe, nyie ndio wanaume mnafia gesti mnatupa wakati mgumu wa kulilia maiti, maana mwanake anabaki kulia kwa aibu badala yakulia kwa uchungu. umenikera.
Unahasira??
Msamehe basi.
 
Back
Top Bottom