Rafiki yangu amezaa na mke wa mtu

King Jody

JF-Expert Member
Oct 8, 2022
1,002
1,830
Habari zenu waungwana,
Rafiki yangu anaomba ushauri, Kwa kifupi ilitokea akawa na mahusiano na mke wa mtu, kwa maelezo yake anasema Mara ya kwanza Kushiriki tendo mwanamke alinasa ujauzito.

Baada ya mwanamke kujifungua mtoto mzuri wa kike ikawa jamaa anaulizia maendeleo ya mtoto anapewa ushirikiano kama kawaida, Wakati huo Mume wa huyo mwanamke hajui kama mtoto si wake,

Jamaa alimwambia mwanamke kwa kuwa imetokea wamezaa ili kuepusha hatari kwake na kwa mtoto wapunguze kuwasiliana na wavunje mahusiano abaki na jambo moja tu la kumhudumia mtoto japo kwa siri,

mwanamke akamwambia jamaa kama anahitaji kuendelea kupata taarifa za mtoto basi waendelee na mahusiano, mwanamke hataki habari ya kuvunja mahusiano, Jamaa anakiri ni kweli alifanya kosa kubwa na hata nafsi yake inamsuta. Mshaurini huyu jamaa yangu kwani yuko njia panda.
 
Pole!

Sasa mpaka huu mkasa unaletwa hapa, maana wewe na huyo jamaa yako mmeona kuna tatizo, na tatizo lenyewe amezaa na mke wa mtu na wote mnakiri hivyo.

Sasa mnataka ushauri wa kazi gani ikiwa nyote watatu mke, jamaa, na wewe mnahisi siyo sawa?

Hapa mnataka majibu gani?

Anyway, kitanda hakizai haramu, kisheria mtoto siyo wa jamaa bali ni wa mwenye mke.

Huyo mwanamke atumie nafasi yake kama mama kwamba ajuaye baba wa mtoto ni yeye, na hivyo ampe mumewe mtoto na mtoto atambulishwe kwa baba mlezi.

Siku zote ndiyo maana baba huitwa Baba Mlezi na Mama ni mzazi.

Kama jamaa kapanda mbegu shamba si lake basi mazao si yake; kama ana kiherehere lolote limkute; mke wa mtu sumu!
 
achukue panga, shoka na bunduki kama anayo aende kwa mwenye mke akaombe samahani, jamaa akimsamehe basi atakuwa amepata msamaha pia mbele za Mwenyezi Mungu.

Unamdhini mke wa mwenzio huku ukijua kabisa na kujiona shababi, hii sio sawa.

Tukae mbali sana na huu uhuni wazee, sio sawa kutembea na mke wa mwenzio huku ukijua kabisa ni mke wa watu.
 
Habari zenu waungwana,
Rafiki yangu anaomba ushauri, Kwa kifupi ilitokea akawa na mahusiano na mke wa mtu, kwa maelezo yake anasema Mara ya kwanza Kushiriki tendo mwanamke alinasa ujauzito.

Baada ya mwanamke kujifungua mtoto mzuri wa kike ikawa jamaa anaulizia maendeleo ya mtoto anapewa ushirikiano kama kawaida, Wakati huo Mume wa huyo mwanamke hajui kama mtoto si wake,

Jamaa alimwambia mwanamke kwa kuwa imetokea wamezaa ili kuepusha hatari kwake na kwa mtoto wapunguze kuwasiliana na wavunje mahusiano abaki na jambo moja tu la kumhudumia mtoto japo kwa siri,

mwanamke akamwambia jamaa kama anahitaji kuendelea kupata taarifa za mtoto basi waendelee na mahusiano, mwanamke hataki habari ya kuvunja mahusiano, Jamaa anakiri ni kweli alifanya kosa kubwa na hata nafsi yake inamsuta. Mshaurini huyu jamaa yangu kwani yuko njia panda.
We umejuaje mtoto ni mzuri,,,ni wewe ila pole mkuu pambania ulichopanda tumia akili,,,,,Akili Mungu aliyokupa inakutosha kuyakabili mazingira yote.....wala huhitaji akili toka nje man....
 
Kwanza huyo mwanamke ni malaya

Cha kufanya akapime DNA kwanza kisiri, kama malaya hataki amwache mumewe aendelee kutunza mtoto

Wanawake malaya matapeli sana

Anaweza akawa anahudumia mtoto kumbe hata mtoto si wake wala wa sio wa mume wake huyo malaya, utakuta ni mtoto wa mwanaume mwingine kabisa

Kumfanya malaya kuwa mke ni changamoto sana na haiwezikani
 
Yeye anataka taarifa za mtoto bila kutuma kibunda,

Ahakikishe anatuma 150,000/- hadi 300,000 kwa mwezi atapewa taarifa za mtoto
 
Habari zenu waungwana,
Rafiki yangu anaomba ushauri, Kwa kifupi ilitokea akawa na mahusiano na mke wa mtu, kwa maelezo yake anasema Mara ya kwanza Kushiriki tendo mwanamke alinasa ujauzito.

Baada ya mwanamke kujifungua mtoto mzuri wa kike ikawa jamaa anaulizia maendeleo ya mtoto anapewa ushirikiano kama kawaida, Wakati huo Mume wa huyo mwanamke hajui kama mtoto si wake,

Jamaa alimwambia mwanamke kwa kuwa imetokea wamezaa ili kuepusha hatari kwake na kwa mtoto wapunguze kuwasiliana na wavunje mahusiano abaki na jambo moja tu la kumhudumia mtoto japo kwa siri,

mwanamke akamwambia jamaa kama anahitaji kuendelea kupata taarifa za mtoto basi waendelee na mahusiano, mwanamke hataki habari ya kuvunja mahusiano, Jamaa anakiri ni kweli alifanya kosa kubwa na hata nafsi yake inamsuta. Mshaurini huyu jamaa yangu kwani yuko njia panda.
wambie wafungw ndoa
 
We umejuaje mtoto ni mzuri,,,ni wewe ila pole mkuu pambania ulichopanda tumia akili,,,,,Akili Mungu aliyokupa inakutosha kuyakabili mazingira yote.....wala huhitaji akili toka nje man....
Nimeona picha mwamba
 
Yeye anatak taarfa za mtoto bila kutuma kibunda ,

Ahakikishe anatuma 150,000/- hadi 300,000 kwa mwez atapew taarfa za mtoto
Mwanamke ni mfanya biashara anajiweza kiuchumu, ye amnachotaka waendelee na mahusiano ya kimapenzi, only that
 
Back
Top Bottom