Usiwe king'ang'anizi...soma alama za nyakati!!

Kwani ndoa kazi yake ni nini kama sio kutafuta furaha na maliwazo???Kama ndoa inampa mtu kinyume cha anachohitaji na dalili za mabadiliko hamna ni bora kuikimbia kabla mtu hajachanganyikiwa kwa msongo wa mawazo.Maana ikishatokea hivyo hutokua faida kwenye hiyo ndoa wala hiyo ndoa haitakua faida kwako!!!!


LAKINI LIZZY - SUPPOSE MMEJENGA NYUMBA WOTE - MNAISHI PAMOJA - HALAFU ANAANZA VISA - YAANI UTOKE UMWACHE AKAE KWA RAHA ZAKE NA AMLETE MWINGINE NYUMBANI KWAKO??? SOMETIMES NDIO MAANA INAKUWA NGUMU - IMAGINE UNAENDA KUPANGA???

MIE NAONA AFADHALI KAMA ANAFANYA VISA NA KWA VILE KAKUCHOKA - ATOKE YEYE ............ UNAWEZA KUSEMA MUUZE MGAWANE - SUPPOSE ANAKATAA????

KUNA FACTORS NYINGI SANA ZA KUANGALIA

hayo ni mawazo yangu tu
 
Ndo maana kuna sheria na mahakama mpendwa..Yatima!Kama nyumba ni mali yenu na imeandikishwa kisheria itauzwa mgawane au mmoja amlipe mwingine shea yake alafu yeye anabaki na nyumba!Tatizo ni kwamba wapo wengi wanaokuta mwanaume ameshajenga kwahiyo yeye anahamia tu..hapo hata wakati mwingine mwanaume anadiriki kumwambia mwanamke atulie maana yupo kwake!Nwyz ndo maana kila siku tunaimbiwa tujitume!Ukiwa na vijicent vyako unaondoka na kutengeneza maisha yako!
 
LAKINI LIZZY - SUPPOSE MMEJENGA NYUMBA WOTE - MNAISHI PAMOJA - HALAFU ANAANZA VISA - YAANI UTOKE UMWACHE AKAE KWA RAHA ZAKE NA AMLETE MWINGINE NYUMBANI KWAKO??? SOMETIMES NDIO MAANA INAKUWA NGUMU - IMAGINE UNAENDA KUPANGA???

MIE NAONA AFADHALI KAMA ANAFANYA VISA NA KWA VILE KAKUCHOKA - ATOKE YEYE ............ UNAWEZA KUSEMA MUUZE MGAWANE - SUPPOSE ANAKATAA?
Alafu usisahau kwamba kuna wanaume wasio na aibu anaweza kukuletea mwanamke humo humo ndani!
 
Kuna wakati unaweza kumkuta mtu yupo kwenye mahusiano yenye kila aina ya karaha na unyanyasaji lakini bado yupo tu na wala hafikirii kuondoka.Unakuta mtu anatukanwa...anapigwa...anadharauliwa...yani kwa ujumla anaonyeshwa kila dalili za kuchokwa ama kutotakwa tena lakini anaamua kufa kibudi.Uvumilivu ni muhimu kwenye mahusiano...ila pia inabidi tujifunze kusoma alama za nyakati.Kuna vitu ambavyo mwenzi wako akianza kuvifanya tena kwa kuvirudia rudia unatakiwa ujue kwamba hapa sitakikani tena na utafute jinsi ya kujitoa.Ndio maana wahenga walisema ''akufukuzae hakwambii ondoka.'' Mara nyingi mtu atakufanyia visa akijua kwamba ukivichoka utaondoka mwenyewe...kumbe kuna wale wenzangu na mie wanaoamini na kujipa moyo wa mabadiliko hata pasipo na moyo...unavumilia manyanyaso ukijua kesho itakua bora ya jana alafu matokeo yake jana inageuka bora ya leo pale unapovunjwa moyo kabisa.

Na hii ni zaidi kwa sisi kina dada!!Jamani embu tujifunze kusema inatosha na tuache kua ving'ang'anizi.Jiamini kwamba ulivyompata huyo ndivyo ambavyo utampata mwingine.Usiishi kwa mateso kwa wasiwasi wa kutokupendwa tena kwasababu hujui kuna kizuri gani kinakusubiria huko nje ila hakiwezi kujitokeza bila wewe kuweka hiyo nafasi wazi!Hamna mtu anaestahili kulala akilia kila siku au kutokua na furaha kwasababu ya binadamu mwenzake.Ukiona mtu hakufai achana nae...usimpe mtu mwingine nafasi ya kucontroll maisha yako ....hiyo ni kazi yako.Ukitaka furaha itafute....ukikereka na kuchoka huzuni ikimbie!!!

Usisubiri kuvunjwa moyo uokote vipande....ondoka na moyo wako mzima ukatafute atakaeupa furaha na amani!!

So does not matter how much it pains (time heals) ni bora uondoke mapema na kujijenga mwenyewe.., because you should never depend on someone else for your happiness you must be a King/Queen to your own castle so its true "If he cant learn to love you, you should leave him" sababu life is too short and the time you spend na huzuni with someone can be spent better with someone else who know your value.., and they are a lot people out there who will value you more hata kama hakuna ni bora kukaa peke yako kuliko na mzigo wa matatizo........BY J!!


wanaish kwa mazoea awaish kwa kusoma nyakat
 
Tukutane pale chini ya mwembe kabla hujanikaribisha ghetto kwako na kuninunulia simu mpya niachane na mChina!
hehehe CPU akiwa hayupo unakuwa unaongea kijitu kizima kweli wewe. halaf leo nimemind kuchunwa kweli. mwaga menu dada. yaani hapa mambo ya fedha ni kama kuleft click mouse tu
 
hehehe CPU akiwa hayupo unakuwa unaongea kijitu kizima kweli wewe. halaf leo nimemind kuchunwa kweli. mwaga menu dada. yaani hapa mambo ya fedha ni kama kuleft click mouse tu

Ahh una pesa gani na wewe?Walio nazo hawaulizi unataka kiasi gani...wanatoa tu!Alafu mwache Sipiyu!
 
Ahh una pesa gani na wewe?Walio nazo hawaulizi unataka kiasi gani...wanatoa tu!Alafu mwache Sipiyu!
nikiamua kuzuia share yangu kwa serikali nina hakika viwango vya mishahara TZ vitashuka. jarib kuwa karib sana na mimi kwa mafanikio yako ya baadae.
 
Wanavumilia eti Lizzy,labda atabadilika. Wanakufa kisabuni.
 
nikiamua kuzuia share yangu kwa serikali nina hakika viwango vya mishahara TZ vitashuka. jarib kuwa karib sana na mimi kwa mafanikio yako ya baadae.
Mafanikio ya baadae nnayo mimi wewe!Au unataka ukininyanyasa na mimi nivumilie kwasababu wewe ndo unanipa kula?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom