Sababu za ongezeko la vifo vingi kwa vijana wa nyakati hizi

GALOU

New Member
Jan 16, 2015
1
9
Kama Unafanya kazi SOMA hii
Utaokoa Maisha yako...🫡

Siku hizi kumekuwa na ongezeko la vifo vya ghafla kya vijana wengi (24-45).

Kwanini?

Kuna sababu nyingi lakini jambo la msingi tumepoteza dira ya maisha,

Focus kubwa ya vijana imekuwa kwenye mambo 2 makubwa:

1. Kusaka noti
2. Kuponda maisha

Zamani wazee wetu walidumu sana kutokana na lifestyle yao:

i. Kutafuta chakula kwa nguvu kubwa
ii. Kutembea na kukimbia umbali mrefu wakitafuta chakula (Mazoezi)
iii. Kula vyakula vya asili
iv. Kutokula kabisa bidhaa

SASA SISI TUMEGHUBIKWA NA AINA MPYA YA MAISHA:

1. Kutafuta na Kusahau Afya
Watu wamewekeza nguvu kubwa kwenye kutafuta maisha kuliko kawaida.
Sio kitu kibaya kufanya kazi kwa bidii.
Mimi mwenyewe nafanya kazi kwa muda mrefu sana.
Suala la msingi, unatunzaje afya yako?
Mind you, unaweza kutafuta sana pesa ukiwa kijana na kuja kuitafuta sana afya ukiwa mzee.

Mimi ninaamini kwenye yote 2.
TUTAFUTE PESA NA HUKU TUKITUNZA AFYA ZETU.

2. Kula Hovyo bila Kujali Afya
Watu wengi hasa wanaofanya kazi za maofisini,
Hawali kwa makusudi,
Wamejaza sukari, milo, maziwa feki, jam, mayonnaise, margarine na bidhaa zingine ofisini mwao.
Mikate ndio vyakula visivyokatika ofisini.
Wakitoka kwenda kula: wanakula kuku wa kisasa, soda, energy, na junk food kama zote.

Kwa kifupi kula kwa afya sio kipaumbele kabisa.

Ni huzuni sana.

3. Kutokufanya Mazoezi
Kufanya mazoezi peke yake kuna kuepusha na magonjwa mengi sana.
Sasa watu wanatumia magari kwenda kazini,
Wanaamka na kwenda job bila kufanya mazoezi,
Wakitaka kwenda lunch wanatumia usafiri,
Wakiwa ofisni wanatumia lift kupanda juu,
Kwa kifupi miili imelemewa na mafuta na nyama uzembe.
Kwa namna hii utapata kila aina na madhara na udhaifu.
Miili haitumikishwi kabisa na,

Mwanadamu anakuwa imara anapokuwa na rapsha rapsha na mambo yanayofanya mwili usikae kizembe.

4. Kukaa kwa Muda Mrefu
Mwili wa mwanadamu kimuundo unatakiwa kuwa umesimama zaidi kuliko kukaa.
Ndo maana kuna changamoto nyingi sana za magonjwa zitokanazo na kukaa kwa muda mrefu.
Mwili wa mwanadamu unatakiwa kuwa na balance nzuri ya kukaa na kusimama.
Sasa unakaa kwenye usafiri kwenda kazini,
Kazini muda wote umekaa,
Ukienda lunch umekaa,
Ukirudi nyumbani kwenye usafiri umekaa,
Nyumbani unakaa.
Unadhani bawasiri utaikwepaje hapa?
Unadhani low back pain utaikosaje hapa?
Lazima tu utawindwa na magonjwa kadha wa kadha.

5. Kutokuwa na Vifaa Bora vya Kufanyia Kazi
Kwa watu wanaokaa kwa muda mrefu wanatakiwa
kuwa na viti maalum na meza za kufanyia kazi.
Unatakiwa kuwa na adjustable table,
Meza unayoweza kuitumia ukiwa umekaa na
ukichoka ukabadilisha ikawa ndefu ukasimama.
Na ukafanya kazi ukiwa umesimama.
Wapo wengi wana meza hizi lakini hawazitumii kikamilifu.
Kaka yangu @MalemboLE anayo hii meza na huwa anajitahidi kuitumia kikamilifu. Tujifunze.

Haya je tunatumia viti gani?
Watu wengi hawatumii vitu bora,
Vinavyoruhusu kukaa kwa muda mrefu ukiwa kwenye pozi sahihi.

Hivi ni baadhi tu ya vifaa vya muhimu zaidi kwa,
Utendaji kazi bora na kulinda afya zetu.

6. Stress za Mapenzi
Kumekuwa na chipuko kubwa la soy boys na simps kwa vijana wengi.
Wenye pesa na wasio na pesa. Mapenzi yanawanyanyasa.
Wenye pesa wanadhani wanastaihili kupendwa kwa sababu wanazo, huzuni!
Wasionazo wanadhani wanastahili kupendwa kwa sababu wanajipendekeza kupitiliza. Dah!
Wote ni maumivu tu.
Ku-survive mapenzi kwa dhama hizi unakuwa ujuzi adimu.
Unahitaji kujifunza kubalance shobo za mapenzi.
Lazima ujifunze kutokuwa simp na soy boy.

Wanawake watakupenda na kukuheshimu ukionesha:
..Unayejali, linda, fikisha kunako, tunza, ongoza.
LAKINI, lazima uwe na:
..Sauti
..Mamlaka
..Uongozi
..Usiyetabirika
..Usiyekubali ujinga
HAYA YOTE UNATAKIWA KUBALANCE SHOBO.

7. Kutokufanya Kazi Unayopenda
Watu wengi wamekuwa na kawaida ya kufanya kazi zinazowaingizia pesa,
Bila kujali wanapenda au la.
Sibishi, kwa mazingira yetu wengi wanakuwa hawana uchaguzi na kuishia,
Kufanya kazi wasizozipenda ili tu mkono uende kinywani.
Tatizo ni kuwa haya maisha yana stress nyingi sana kuliko furaha ukiwa kazini.

Hawa ndio watu wanachukia zaidi Jumatatu na kufurahisi kila Ijumaa.
Maisha yao yote wanawaza kumaliza kazi na kuanza wikendi.
Ikifika Jumapili wanaanza mawazo kuwaza blue Monday.
Tofauti ni kuwa ukifanya kazi unayoipenda sana,
Unakuwa hujui tofauti ya kazi na kupumzika.
Unatamani kufanya kazi muda wote maana ni sehemu ya maisha yako.

Ukiweza, jitafute, wafanyie kazi kwa muda ukijitafuta - Siku moja amka ukiwa unaenda kufanya kazi unayopenda kutoka moyoni.

Na sio kukaa kwenye kazi unalaani kila siku,
Na maisha ya kazi yanachukua muda wetu mwingi wa hapa duniani.

Furaha yako imebaki kwenye kupokea mshahara tu.

You can do better.
Work on yourself more than you work on your job,
...Jim Rohn.

Bonus:
8. Kukosa balance ya maisha
9. Kunywa pombe na kupati kupitiliza

MADHARA YA LIFESTYLE HII:
i. Kuugua mara kwa mara

ii. Kuwa umechoka muda wote

iii. Kukosa hamu ya chakula

iv. Kunenepa bila mpango

v. Kuotesha vitambi uchwara

vi. Bawasiri kushamiri

vii. Low back pain kuzidi

viii. Magonjwa ya moyo

ix. Kuongezeka kwa pressure na kisukari

x. Upungufu wa nguvu za kiume

xi. Kukosa furaha na maisha

xii. Stress zisizoisha

xiii. Na mengine mengi

NINI KIFANYIKE?

FIX maisha yako:

1. Kula vizuri

2. Fanya mazoezi (3-7 kwa wiki)

3. Kuwa mtu wa movements – Tumikisha mwili

4. Tumia vifaa bora kazini

5. Ondoa sukari, jam, margarine, mikate na bidhaa zote ofisini

6. Ongeza muda wa kutembea kwa miguu

7. Jifunze ku-survive mapenzi

8. Fanya unachopenda au penda unachofanya

9. Paki gari mbali na utembee

10. Ukiwa karibu na kazini nenda kwa miguu

11. Usitumie lift kupanda majengo

12. Ukiwa karibu na kazini nenda kwa miguu

13. Punguza kupati i.e pombe

Nakuamini sana kuliko unavyojiamini,
You brother
Millambo, R.
 
Asante kwa kutukumbusha , mtindo wa maisha inaua vijana wengi sana now days.
 
.....vijana show off zmeizidi + kupenda masifa [like]....kila linalokupata unakimbilia kwnye mitandao,wahuni wanakuchoro tu na kukuachua husda na vijicho...

But kifo ni haki...
 
Mada nzuri, ningependa kuongezea jambo

1_ Matumizi ya Usafiri (Bodaboda) kama kijana unaejielewa jitahidi kuepuka hiii kama unataka uishi Maisha marefu.

2_Matumizi ya Sukari kupita kiasi acha.

3_Kutotulia nyumbani ukatuliza hilo komwe kama huna cha maana cha kufanya huko mitaani (Jinsi unavyozurura ndio jinsi unavyopishana na kifo/mtoa roho) jitahidi kama hauna shughul ya msingi baki nyumbani. Mfno ni wakati wa COVID.. kama utatulia home haikupati ila ukiwa mzururaji lazim ipite na ww.

4_Kataa Ndoa.
 
Taarifa yako inatofautiana na data za NBS ambazo zinatuambia life expectancy imeongezeka toka miaka 45 mpaka kwenye miaka 54 ivi...
 
Back
Top Bottom