Usijitie kitanzi!

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,026
Hivi utafanyaje?umeishi na mkeo ktk ndoa,mkajaliwa kupata watoto watatu.Siku moja bahati mbaya unapata ajali na kuumia sana sehemu za mgongoni.Daktari anakucheki na kugundua huwezi kuzaa tena maishani kutokana na spinal chord kudhurika.Siku moja unagombana na mkeo,kwa hasira katikati ya ugomvi anakupa ukweli watoto wote watatu si wako,ali cheat na kuzaa na wanaume wengine,utafanyaje?
 
Hufanyi kitu....
 
Nashindwa kuconnect hii story kuumia na kuzaa watoto wote si wako??

Hebu niweke sawa kidogo hapo. Shida iko wapi??
 
Hii story imekaaje, Jamaa amekaa na Mkewe miaka 10 na baadaye anapata ajali, Ninavyoielewa ni kwamba inaonyesha hao Watoto walizaliwa kabla ya Jamaa hajapata ajali.
 
Unajua mtoto si lazima umzae ndo umwite wako
kwa mimi binafsi naona hal watoto ni wake
Sababu ye ndo kawatunza..

Kwa kweli itamuuuma sana
lakini ukiangalia kwenye big picture hakuna la kufanya
maji yamesha mwagika..
Life goes on my dear..
 
Nashindwa kuconnect hii story kuumia na kuzaa watoto wote si wako??

Hebu niweke sawa kidogo hapo. Shida iko wapi??
okay ni kwamba kipindi jamaa yuko safi kiafya,wife ali cheat akazaa watoto wote nje ya ndoa.
 
Shukuru walau una watoto wanaitwa kwa jina lako, hasa ukizingatia mambo yameshakuwa mambo. Chukulia kakudanganya tu hao ni watoto wako, kwa sababu kwanza wewe ndo unawalea.

Ila kwa kweli dunia ina mambo sio wanawake sio wanaume. Heri tu aliyemfanya Bwana Mungu kuwa tumaini lake!!!!
 
LD upo sawa
pia kumbuka wale watoto toka wamezaliwa wanajua baba yao ndie yule. kwa hiyo itachukua muda mrefu hao watoto kuona kwamba yule sio baba yao na inawezekana wasimtambue huyo anayeitwa biological father. aendeleza upendo aliokuwa nao kwa hao watoto wala asionyeshe kuna lolote linalotaka kutengana nao. na watoto watampenda sana huyo baba na kumtunza hadi mwisho wa maisha yake.
 
aaaaghh kumbe kuzaaa tu m nkajua shughuli hawezi piga hao ndo ingekua noma...........................
 
Hivi utafanyaje?umeishi na mkeo ktk ndoa,mkajaliwa kupata watoto watatu.Siku moja bahati mbaya unapata ajali na kuumia sana sehemu za mgongoni.Daktari anakucheki na kugundua huwezi kuzaa tena maishani kutokana na spinal chord kudhurika.Siku moja unagombana na mkeo,kwa hasira katikati ya ugomvi anakupa ukweli watoto wote watatu si wako,ali cheat na kuzaa na wanaume wengine,utafanyaje?

Itakubidi uwe mdogo sana kwa mkeo asije kutoa siri na wewe uwapende zaidi hao watoto. Hata hivyo ni lazima ujue baba zao wa ukweli ili ujue kama ni ndugu zako au rafiki zako. Usikipe kisasi, utakufa kabla hujamaliza
 
story ina utindio wa ubongo... Mwanzo, kati na mwisho no connection...
 
Kama ni mimi nitawachukua watoto tukafanye vipimo.
Inawezekana ameongea kwa hasira.
Sa zingine tunatoa kauli mbaya sababu ya hasira tu. Ikipoa unajutia.
 
Hii story imekaaje, Jamaa amekaa na Mkewe miaka 10 na baadaye anapata ajali, Ninavyoielewa ni kwamba inaonyesha hao Watoto walizaliwa kabla ya Jamaa hajapata ajali.

Yaani anataka kukwambia kwamba huyo kaka hana mtoto na bahati mbaya ndio ameumia na hata weza kuzaa tena, maana bila hiyo ajali huenda na yeye angetafuta mpango wa kando azae nao, ndio anakuuliza ukiwa wewe utafanyaje?
 
Back
Top Bottom