USHUHUDA: Hivi ndivyo mafuta yanavyoibiwa Bandarini Dar...

Status
Not open for further replies.
KIJANA RUDI SHULE KWANZA..FANYA RESEARCH ..KAMA KITU HUJUI HUNA HAKI YA KUJADILI
Shule niliyonayo inanitosha,sitaki shule yenu ya wizi wa mafuta ya Transit halafu mnayapeleka Kibaha na Misugusugu,hata Mh Rais jana kasema,Dsm to Kibaha zimejaa sheli kibao za kuibia mafuta ya Transit...Ebooo!!!Wezi wakubwa nyie
 
Wakuu wa idara ,vitengo,wizara magufuli hatanii na yule yuko serious ,rekebisheni ama mtafukuzwa woooote
 
Hebu tusaidie huyo bulky importer mmoja wapo ni nani?

Hizi tender ni za kila mwezi ambazo hutangazwa na Petroleum Importation Coordinator Ltd (PICL) na supplier wana Bid then the lowest bidder anashinda supply since 2012. Mifano ya kampuni zilizowahi kushinda ni Augusta Energy SA (Geneva), Addax Energy SA(Geneva) Gapco Tanzania Ltd (Tanzania), Gapco Kenya Ltd (Kenya), Sahara Energy(UAE) na ENOC (UAE). Hiyo ni mifano tu na kwa mfano kuna meli ina itwa Ridgeburry John ilikataliwa kushusha december na TBS kwa sababu ya kutokidhi viwango ambapo ilikuwa imebeba Petrol na wamereplace that cargo mwezi February kwa Meli inaitwa MISENO. Utafiti ni muhimu kabla ya kuleta mada hapa.
 
Hi stori ina walakini sana. Ni stori ya kusadikika zaidi.
Sasa hivi Hizi kampuni hazileti meli za mafuta.
Utaratibu unaotumika ni kuwa kila quarter kuna bulk importer mmoja ambaye analeta mafuta. Sio oil com wala world oil au babake yoyote anae agiza mafuta kutoka nje.
Utaratibu uliopo ni kuwa bulk impoerter analeta mafuta na yanashushwa yote kwenye deport ya tipper.
Huyu anaye shunda tenda ndie anaelipa ushuru kwa mafuta yote ysnayo ingia.
Na tangu utaratibu huu kutumika hakuna local company ilo shinda tenda hii..
Makampuni ya ndani yananua mafuta kutoka muagizaji mafuta ambayo yameshalipiwa ushuru wa kuingiza wao hawahusiki na hizo taratibu za kubadilisha Jet na diesel.
Utaratibu huu ndio ulowezesha EWURA kuweza kuweka bei ya mafuta kwa mlaji kwa sababu wote hawa wananunua bei ile ile kutoka kwa bulk importer...serikali inachukua chake yakkingia tu.
Hivyo ni uongo wa mchana kusema kuna meli imeagizwa na oil com au babako nani...
Hizi ni chuki kwa warabu kwa sababu ndio umetanguliza hayo.
Na world wenyewe ni wwswahili walo amka wachapa kazi.
Mafuta yanayo enda nje ya nchi huagizwa na nchi husika na makampuni ya hapa hushughulika na usafirishaji tu.
Hivyo stori sijui alikua ashushe meli diesel lakini imeandikwa jet 1 ni yauongo.

Kama kuna ulaji katika mita basi mchezo anacheza bulk importer ..usiootoshe watu kwa sababu za chuki binafsi

Ndugu Bopwe napenda kukusahihisha kwamba TIPER hupelekwa mzigo ambao ni Financial Hold haujalipiwa kwa supplier (either by Cash or LC yenye payment terms ya 60 days) na kama mzigo umelipiwa unakuwa pump direct to the terminal/depot ya Oil Market Company. Ushuru wa importation kila kampuni inalipa on DAP basis ambapo wanalipa kwa Arrival Quantity na sio Shoretank Quantity received. Kuhusu swala la meter what i knw zile meter haiwez kuhimili pumping pressure rate za meli e.g 100-150MT/hour(KOJ) na 250MT/hour (SPM) na pia wakati mwingine zinaingiza hewa na kuendelea kusoma so zinahitaji calibration kila wakati na uwezo wa kuzitengeneza ndio huwa inakuwa shughuli cha Muhim Government watafute meter bora ambazo hazipitish hewa na pia ziweze kuhimili pumping pressure bar ya meli ili zisiweze kuharibika mara kwa mara na kuweza kutimia njia ya by pass na kuwa na watu waadilifu bandarini hapo tutakusanya kodi ipasavyo.
 
Hile sheria ya kuwalinda watoa taarifa za ualifu inahusika , platform kama hizi jamii forum zitumike kuweka uozo wazi na kusaidia serikali kufahamu maovu. Big up mtoa mada hakika umelitendea haki taifa lako tuko nyuma yako.
 
Kama wewe hujakosea popote kua wa kwanza kuendekeza mswada

Hapa ndipo napo pata tabu na watanzania ,waliotunga sheria za kunyonga walikua hawajui kama wao nao pia wanakosea ???

Mimi niko tayari kwenda mbele zaidi maana naona marais wanakwepa kusaini ,wapeleke muswada na muweka saini wa awe raisi au yeyote atakaye taka kujitolea kuweka saini kwa niaba ya raisi ,Mimi nitamsaidia kuweka saini hao watu kumi wa mwanzo kama mfano
 
Kilichonifanya nicheke ni sentensi ya mwisho kuwa unawastua wahalifu kwa sms kama Pro.Muhongo!
 
Kikwete angenyimwa ukuu wa UDSM mita za kupima mafuta zingefanya kazi !? .......... fankuroo !
Lowasa alikua sahihi sana
Elimu
Elimu
Elimu
Umesoma post aliyo ni quote huyo mwenzio ??? Hebu na wewe jiongeze
 
Rais na Waziri wake mkuu watapata kazi sana kusafisha hii nchi,Ningewashauri kitu kimoja kama kweli wanataka kusafisha nchi hii na siyo "kuonekana wanasafisha" wakati ukweli hakuna kitu wanachofanya.

Wapo watu katika nchi hii wanazo taarifa za mifumo ya wizi katika sehemu mbalimbali jinsi inavyofanya kazi, either wao walishiriki na sasa hawapo kwenye hiyo mirija au wanashuhudia jinsi wizi unavyoendelea ingawa wao hawausiki. Rais angetengeneza utaratibu wa watu wema wenye taarifa ya madudu yanayofanyika katika taifa hili kupeleka hizo taarifa in details wakiwa wanajulikana au hawajulikani, iwe ni choice ya mtoa taarifa.

Nina uhakika wapo watu wangejitokeza kutoa hizo taarifa nikiwapo mimi.

Mimi nina uzoefu wa jinsi mafuta yanavyoibiwa bandarini:

Kwanza niweke wazi, mafuta hayaibiwi bandarini kwa kukadiria au sijui kwa sababu ya flow meters. Hakuna kitu kama hicho. Tena zile flow meter zilikuwa na capacity ndogo na zinaharibika mara kwa mara hivyo zikiharibika inabidi ku-bypass. Meli ikiwa inashusha mafuta inaweza kushusha kwa presha ya bar 16, zile flow meter zilikuwa hazihimili presha kubwa.

Mafuta yakishashushwa, kiwango cha mafuta kilichopokelewa kina pigiwa hesabu na ma-surveyor na wanatengeneza taarifa yao. Mchezo unaanzia hapo TRA, Mafuta yanayotakiwa kulipiwa ushuru ni ya local (yanayotumika humu nchini), na ya transit hayalipiwi ushuru. Sasa figure zinazoingizwa kwenye system ya TRA kwa ajili ya kulipiwa ushuru ndiyo hapo serikali inapoibiwa.

Na anayefanya mchezo huu ni afisa wa TRA kitengo cha mafuta akishirikiana na kampuni husika. Kuna makampuni ambayo yamekubuhu kwa mchezo huo. Makampuni ya watu binafsi yakiongozwa na yanayomilikiwa na waarabu. OILCOM ndio kinara, Lake oil, World oil, CAMEL Oil, etc.

Ipo mifano mingi ila natoa mmoja.

Kuna siku ilikuwa meli na mzigo mkubwa tu kana tani laki moja na nusu, Huo mzigo ulikuwa wa OILCOM. Kwenye Cargo manifesto ya meli ulikuwa umekuwa declared kama JET A1, (mafuta ya ndege) ya transit ya kwenda Zambia. Haya yana tax exemption.

Surveyor wa mzigo alikuwa kijana mmoja anaitwa ANDERSON kutoka Intertek. Akaenda kwenye meli akapima mzigo akaambiwa na wenye mzigo kuwa aandike kuwa ni JET A1 kwenye documents zake, ingawa mzigo ulikuwa ni diesel (GO), akaahidiwa dili ikishakamilika atapewa chake. Basi Anderson machale yakamcheza akaamua kutengeneza ducument set 2, moja akadiclare ule mzigo kuwa ni JET na nyingine kuwa ni GO.

Sasa kosa ambalo walilifanya hawakumuhusisha loading master wa pale manifold. Alipoambiwa afungue line ya kwenda oilcom, Yule mzee akafungua line ya JET ya kwenda OIL com. Sasa pale KOJ manifold kuna chujio za mafuta (Strainers) kwa ajili ya kila aina ya mafuta, na zina ukubwa tofauti kwaajili ya kuchuja mafuta. Mafuta yalipoanza kusukumwa, ile strainer ya JET ikaanza kupiga kelele yaani ikawa inapitisha mafuta kwa tabu.

Loading master akaamua kuangalia kwa nini inapiga kelele, akakuta mafuta yanayopita ni diesel tena ile diesel ya high sulphur (5000ppm). Akaita kwenye radio call, " We Anderson, hiyo mnayosukuma ni JET au DIESEL?", Hakuna mtu aliyejibu kenye radio, ikabidi pump za meli zizimwe washuke kwenye meli kwenda kuongea na loading master.

Sasa ile channel ya radio inayotumiwa kwa mawasiliano inasikiwa na watu wengi wakiwemo TRA, Usalama wa Taifa, Maofisa wa Bandari, n.k, baada ya kama nusu saa, watu zaidi ya 9 wakawa wamefika pale KOJ, wakiwemo maafisa wa usalama wa Taifa.

Kuona hivyo Underson akatoka na gari akakimbia, akamwacha Depot supervisor wa OILCOM, yule kijana wa oilcom ikabidi amtaarifu mzee ISLAM mwenyewe mwenye OILCOM kuwa kimesanuka. Ilikuwa ni Jumamosi, mzee Islam akaagiza watu wote walioenda kushuhudia ile saga waende OILcom, inavyosemekana kila mtu alipewa mil 80 cash palepale kwenye mifuko ya rambo. Na mzigo baadae ukashushwa kwenye line ya diesel.

Sasa ukiangalia wizi unaofanyika kwenye mafuta siyo wizi wa mafuta ila ni ukwepaji kodi, mafuta yanakuwa declared kama transit hayalipiwi ushuru ila yanauzwa local kwa bei ile ile. Na biashara hii ya kukwepa ushuru ilikuwa inasimamiwa na mwenyewe kamishna wa kodi ya forodha Bwana Masamaki.

Mafuta yakishaingiza kama transit yanatengenezewa document zote kuanzia za loading, Checkpoint zote za TRA, clearance ya Tunduma hadi upande wa pili wa boarder, na offloading documents na documents za ZRA(Zambia Revenue Authority). Na Bond clearance.

Hizi taarifa zote Usalama wa taifa wanazijua fika, kama Magufuli akitaka kusafisha, anatakiwa apate watu wa usalama wenye mtazamo kama wake. Laa sivyo, na wao watakuwa wanawashtua waalifu kwa meseji kama prof. Muhongo.

OIL COM ndio kinara.
Ulikua wapi siku zote
 
Wewe jamaa na yule alitoa uzi wa utitiri wa vituo bara bara ya mlandizi mpo vizuri sana ingawaje yule wa kwanza alipingwa sana na hao majambazi na kumkebehi na Ewura nao wanahusika kama wanatoa milion 80 hawawezi kushindwa kuwalipa 10elfu watu kadhaa kupinga watu wanapoibua uozo nimenunua mafuta yasiolipwa kodi miaka zaidi ya mitano ??
 
Vyombo Vipo Imara Kwasasa Ni Kutoa Taarifa Sahihi Kazi Ifanyike Na Matokeo Watu Watayaona Haraka
 
Ndugu Fanya mpango upate makala katika magazeti yetu uanike mambo haya. Nadhani yata wafikia wengi, watanzania wajue kinacho wamaliza na kuwabakisha katika maisha duni
 
....naona majanga mengi sana Tanzania.Kwa kuanzia,hiyo TISS ni ya wapiga dili tu na ndio maana hata wale twiga walipandishwa ndege KIA.Halafu hao hao TISS ndio wanaohusika kwa kiwango kikubwa kuweka viongozi wa nchi hii madarakani.!!
Kama Magufuli kweli ana nia ya dhati,naona aanze na hao TISS,aisafishe hiyo idara yote tuanze upya,kwa sababu imeshathibitika ni idara ya wezi,inayowalinda wezi na kuendelea kulisababishia hasara taifa.
Baada ya hapo ndio akasafishe huko bandarini,naamini itakuwa ni kazi nyepesi sana km ataifanya hiyo ya kwanza,which i highly douby if he will..sioni ni kwa jinsi gani unaweza kumfukuza aliesaidia kukuweka madarakani,na km atashindwa,basi tutaendelea kulalamika kila siku.
 
Ndugu Fanya mpango upate makala katika magazeti yetu uanike mambo haya. Nadhani yata wafikia wengi, watanzania wajue kinacho wamaliza na kuwabakisha katika maisha duni
Mkuu watu wamagazeti huja huku JF na kuiba post na kuzichapisha wao bila hata kuwacredit wahusika.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom