USHUHUDA: Hivi ndivyo mafuta yanavyoibiwa Bandarini Dar...

Status
Not open for further replies.
Huo ni uongo uwezo wa meli kushusha KOJ ni meli isiyozidi Tani 35 KT na above that inashushia SPM au single mooring Point ambayo inashusha Diesel peke yake 70KT to 100KT mleta mada usidanganye watu KOJ haiwez kuhimili meli inayobeba Tani laki moja utakuwa umesimuliwa
Je hakuna huo ukwepaji wa kodi kwenye mafuta?

Hilo ndio swala la msingi
 
Halafu swala jingine inaonekana kuna vitu huvijui vizuri as per TBS requirement for Diesel au Gasoil inayotakiwa ni low sulpher 500 ppm na sio hiyo uliyoitaja na ilianza kutumika January 2015 before hapo tulikuwa tunatumia 50ppm. Mafuta yote yanayoingia nchini yanakuja kwa Bulk supply na kusimamiwa na PIC zamani sasa ni PBPA as government agency ambazo tangu waanze kuleta mafuta hakuna meli iliyoleta mafuta 150 KT haijawah kutokea na unatakiwa kufahamu delivery zinakuwa tano(sawa na meli nne mpka tano kulingana na mahitaji ya mwezi huo) kwa supply ya mwez mmoja meli za Gasoil au diesel 2 zenye uwezo wa kubeba 70 KT to 100 KT na hizi zote hushushia SPM ambayo ipo deep sea na KOJ hushusha Motor Spirit Premium/Unleaded petroleum/Petrol na Jet A1/IK na meli inayobeba Jet A1 huwa inakuwa Comb of Either petrol and Jet A1 au Gasoil & Jet A1 na meli hizo hazizidi kwa product zote 30KT to 38KT. As per shipping and supply contract.
si tumesema watu waache ushabiki na kupenda kuchafuana wafanye tafiti zaidi katika kupokea habari
 
Hivi kuna shule inayozidi hapa JF? MleMleta uzi ametuhabarisha hata kuzidi hizo Internet search zako, hivi ukiingia Google uka type wizi KOJ kama alivyodadavua mleta uzi utapata jibu? Acha kukariri na pia umesema kilichosemwa ni uongo, kuna bulky importers sasa tumekuambia tutajie wewe unaleta longo longo.
Oil com haagizi mafuta..wacheni porojo.
Mafuta tangu 2012 yanaagizwa kupitia PIC.
Hao hutoa tenda every quarter kuleta mafuta.
Sasa hivi kampuni inayoleta mafuta ni kampuni ya Nigeria .
Hakuna meli nyengine zinazokuja hapa kushusha .
Mmekaa kuleta fyoko fyoko tu...
 
hii nchi aisee ukiifuatilia unaweza ukadata
Yaani mkuu wee acha tu! Unaweza ukacease. Ila me naona hii vita inabidi wote tushiriki ili tutoke hapa tulipo. Me najiuliza hii habari inaweza kuwafikia walengwa? Hii issue inaweza kuwa na ukweli ndani yake!
 
Nikisoma habari kama hizi naumia sana,imagine mtu mmoja anapewa mil. 80 za kumfunga mdomo!!!!
Najuta kuzaliwa Tanzania,Nchi ya wachache!
Wengine ni vile tumejikuta tumeshazaliwa Tanzania,hakuna namna nyingine!
Usikate tamaa you have to push back.
 
Tanzania haipo salama kama kitengo kinahusika kuhujumu uchumi wa nchi nani atatusaidia sasa.
 
Mkuu Nyani Ngabu hebu njoo ushuhudie huku jinsi hii nchi ilivyooza,aisee kweli ilipaswa tuwe mbali sana kimaendeleo,inauma sana aisee,daaah
 
Wewe wala usijali sidhani kama Raisi Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa hawayajui hayo uliyoyaeleza wanayajua sana kwanza wanayajua kabla hata WM hajaenda hapo kwenye hiyo mitambo ya mafuta na ndiyo maana unaona hawakuweza kumdanganya ingawaje yeye WM siyo mtaalamu wa mambo ya mafuta, alikuwa na data zote na hata ukifwatilia maagizo aliyoyatoa siyo ya mtu ambaye hakuwa amejitayarisha na asiyejua alichokuwa anakifanya!

Hata ukiangalia huyo Masamaki uliyemtaja alishachomolewa zamani na ana kesi hivyo ninaweza kukutoa hofu wanajua kila kitu na ni swala la muda tu kwani lazima ujue kwamba wahalifu nao pia ni werevu hivyo ni lazima kwenda nao kwa umakini na mwisho wa siku sisi tunachotaka na fedha zetu ninakwambia kwa Magufuli kila jiwe litafunuliwa kama alivyosema Mzee Slaa, hao akina Oil Com, Lake Oil wote wako kwenye radar utasikia tu mda siyo mrefu!

Hivyo wewe chill na relax Raisi na Serikali yake wanafahamu yote hayo na zaidi kuna sababu kwa nini Maswi aliletwa halafu akaondolewa baada ya kumaliza kazi yake hivyo sasa kazi ndiyo imeanza na haponi mhalifu yoyote yule amini usiamini!
Hivi kweli Maswi pale alienda kufanya nini? Me mpaka leo sijapata jibu.
 
Tena wanaotoa taarifa kama hizi za muhimu za uhujumu uchumi,ni vyema wangepewa zawadi ikithibitika kuwa habari zao ni sahihi,daaaaaah,kweli nchi yetu ilipaswa iwe donor country
 
Hii nchi imeoza kuitibu hadi ipone lazima operation kubwa na madaktari bingwa (Watanzania na Viongozi wazalendo) watumike sio wale wanaojifunza kazi
 
Uzalendo kwanza, yaonyesha una taarifa njema kwa taifa hili. Embu nenda magogoni sema nahitaji kumuona JPM. Na kwamba una jibu/busha linalohitaji tiba mara moja.
 
Rais na Waziri wake mkuu watapata kazi sana kusafisha hii nchi,Ningewashauri kitu kimoja kama kweli wanataka kusafisha nchi hii na siyo "kuonekana wanasafisha" wakati ukweli hakuna kitu wanachofanya.

Wapo watu katika nchi hii wanazo taarifa za mifumo ya wizi katika sehemu mbalimbali jinsi inavyofanya kazi, either wao walishiriki na sasa hawapo kwenye hiyo mirija au wanashuhudia jinsi wizi unavyoendelea ingawa wao hawausiki. Rais angetengeneza utaratibu wa watu wema wenye taarifa ya madudu yanayofanyika katika taifa hili kupeleka hizo taarifa in details wakiwa wanajulikana au hawajulikani, iwe ni choice ya mtoa taarifa.

Nina uhakika wapo watu wangejitokeza kutoa hizo taarifa nikiwapo mimi.

Mimi nina uzoefu wa jinsi mafuta yanavyoibiwa bandarini:

Kwanza niweke wazi, mafuta hayaibiwi bandarini kwa kukadiria au sijui kwa sababu ya flow meters. Hakuna kitu kama hicho. Tena zile flow meter zilikuwa na capacity ndogo na zinaharibika mara kwa mara hivyo zikiharibika inabidi ku-bypass. Meli ikiwa inashusha mafuta inaweza kushusha kwa presha ya bar 16, zile flow meter zilikuwa hazihimili presha kubwa.

Mafuta yakishashushwa, kiwango cha mafuta kilichopokelewa kina pigiwa hesabu na ma-surveyor na wanatengeneza taarifa yao. Mchezo unaanzia hapo TRA, Mafuta yanayotakiwa kulipiwa ushuru ni ya local (yanayotumika humu nchini), na ya transit hayalipiwi ushuru. Sasa figure zinazoingizwa kwenye system ya TRA kwa ajili ya kulipiwa ushuru ndiyo hapo serikali inapoibiwa.

Na anayefanya mchezo huu ni afisa wa TRA kitengo cha mafuta akishirikiana na kampuni husika. Kuna makampuni ambayo yamekubuhu kwa mchezo huo. Makampuni ya watu binafsi yakiongozwa na yanayomilikiwa na waarabu. OILCOM ndio kinara, Lake oil, World oil, CAMEL Oil, etc.

Ipo mifano mingi ila natoa mmoja.

Kuna siku ilikuwa meli na mzigo mkubwa tu kana tani laki moja na nusu, Huo mzigo ulikuwa wa OILCOM. Kwenye Cargo manifesto ya meli ulikuwa umekuwa declared kama JET A1, (mafuta ya ndege) ya transit ya kwenda Zambia. Haya yana tax exemption.

Surveyor wa mzigo alikuwa kijana mmoja anaitwa ANDERSON kutoka Intertek. Akaenda kwenye meli akapima mzigo akaambiwa na wenye mzigo kuwa aandike kuwa ni JET A1 kwenye documents zake, ingawa mzigo ulikuwa ni diesel (GO), akaahidiwa dili ikishakamilika atapewa chake. Basi Anderson machale yakamcheza akaamua kutengeneza ducument set 2, moja akadiclare ule mzigo kuwa ni JET na nyingine kuwa ni GO.

Sasa kosa ambalo walilifanya hawakumuhusisha loading master wa pale manifold. Alipoambiwa afungue line ya kwenda oilcom, Yule mzee akafungua line ya JET ya kwenda OIL com. Sasa pale KOJ manifold kuna chujio za mafuta (Strainers) kwa ajili ya kila aina ya mafuta, na zina ukubwa tofauti kwaajili ya kuchuja mafuta. Mafuta yalipoanza kusukumwa, ile strainer ya JET ikaanza kupiga kelele yaani ikawa inapitisha mafuta kwa tabu.

Loading master akaamua kuangalia kwa nini inapiga kelele, akakuta mafuta yanayopita ni diesel tena ile diesel ya high sulphur (5000ppm). Akaita kwenye radio call, " We Anderson, hiyo mnayosukuma ni JET au DIESEL?", Hakuna mtu aliyejibu kenye radio, ikabidi pump za meli zizimwe washuke kwenye meli kwenda kuongea na loading master.

Sasa ile channel ya radio inayotumiwa kwa mawasiliano inasikiwa na watu wengi wakiwemo TRA, Usalama wa Taifa, Maofisa wa Bandari, n.k, baada ya kama nusu saa, watu zaidi ya 9 wakawa wamefika pale KOJ, wakiwemo maafisa wa usalama wa Taifa.

Kuona hivyo Underson akatoka na gari akakimbia, akamwacha Depot supervisor wa OILCOM, yule kijana wa oilcom ikabidi amtaarifu mzee ISLAM mwenyewe mwenye OILCOM kuwa kimesanuka. Ilikuwa ni Jumamosi, mzee Islam akaagiza watu wote walioenda kushuhudia ile saga waende OILcom, inavyosemekana kila mtu alipewa mil 80 cash palepale kwenye mifuko ya rambo. Na mzigo baadae ukashushwa kwenye line ya diesel.

Sasa ukiangalia wizi unaofanyika kwenye mafuta siyo wizi wa mafuta ila ni ukwepaji kodi, mafuta yanakuwa declared kama transit hayalipiwi ushuru ila yanauzwa local kwa bei ile ile. Na biashara hii ya kukwepa ushuru ilikuwa inasimamiwa na mwenyewe kamishna wa kodi ya forodha Bwana Masamaki.

Mafuta yakishaingiza kama transit yanatengenezewa document zote kuanzia za loading, Checkpoint zote za TRA, clearance ya Tunduma hadi upande wa pili wa boarder, na offloading documents na documents za ZRA(Zambia Revenue Authority). Na Bond clearance.

Hizi taarifa zote Usalama wa taifa wanazijua fika, kama Magufuli akitaka kusafisha, anatakiwa apate watu wa usalama wenye mtazamo kama wake. Laa sivyo, na wao watakuwa wanawashtua waalifu kwa meseji kama prof. Muhongo.

OIL COM ndio kinara.
Sasa naona Uzalendo wa Watanzania unarejea!
 
Je hakuna huo ukwepaji wa kodi kwenye mafuta?

Hilo ndio swala la msingi

Ndugu Belo ukwepaji upo na ukwepaji upo hasa kwenye declaration ambayo inahusisha mafuta ya Transit tu kwasababu process ya Cargo manifest ni ngumu kwa kitu alichokisema hapo juu mleta mada kwasababu manifest inafanywa na shipping agency (Sturrock) kwa kushirikiana na Supplier na kuwa lodged TRA na kampuni yenye mzigo yenyewe inapeleka Notice of Intention (NOI) to TRA kwahiyo udanganyifu unafanyika tu kwa kutoa Declaration ya kwamba mafuta yanapelekwa Transit(False declaration) na kwa mafuta ya Transit yoyote yale unapewa 30 days ya kuyapeleka to final destination since the day you receive Notice of Tax Liability from TRA(NOL). Kama siku hizo zikipita na mafuta hayajaenda unapewa demand note of tax from TRA na hiyo tu ndio mbinu mara nyingi hutumika kwa ukwepaji kwa watu kutengeneza document za uongo kuonyesha mafuta yalivuka boda na kwenda yalikotarajiwa kupelekwa. Mm nimekuwepo katika industry hii Oilcom haijawahi safirisha mzigo kwenda Zambia oilcom mafuta yake ya transit huwa yanaenda DRC kwa jinsi anavyo declare kwenye manifest filing so mleta mada amesimuliwa i can tell u. I work under company sometimes won the tender to supply white product(Petroleum) to Tanzania. Watu wanatakiwa kufanya research na kuacha kusikia story za kusimuliwa halaf anakuja kana kwamba ana uhakika
 
Hujui kitu..bwana unafata mkumbo tu.
Oil com sio ya mu asia wala haina uhusiano na mbunge.
Hii inaonesha vp unafata mkumbo tu.
Pump imeharibika na utaratibu wa zamani kupima ni bora zaidi.
Wewe unayejuankila kitu ndio jizi,mmeumbuka mnakuja hapa kutetea tetea bila mpango,mianya yenu imegundulika hamna pa kutokea,hakuna cha mkumbo....huu wizi upo na mmeumbuka!!Mwaka dume huu,hauzai mapacha wala njiti...Hoja si ya nani,hoja ni wizi...hilo lilikuwa ni swali kutaka kujua,na sio established facts
 
Nilishasema tena nchi hii inafisadiwa na waarabu wapemba na wachina na sio watanzania weusi kuna haja ya kutimua hii mijizi na wanapenda kuswali kweli sijui ni Mungu yupi wanamswalia
Mungu wa Kilaini na Gwajima !
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom