USHUHUDA: Hivi ndivyo mafuta yanavyoibiwa Bandarini Dar...

Status
Not open for further replies.
Nchi hii ina wenyewe wengine ni wasindikizaji tu.No patriotism kwa viongozi na wafanyakazi wa umma.
 
Mkuu sio wafanyakazi wa umma tu, hata wasio wafanyakazi wa umma wanahusika tena sana, hizo kampuni utakuta zina watumishi wengi tu watanzania , lakini wanashiriki kuiumiza nchi yao
 
Aisee kumbe watu wanapiga pesa kila nyanja ndani ya hii nchi dah. Cha zaidi no kumuombea my. Raid awe na moyo huo huo Wa kusafisha nchi yetu.
Taarifa muhimu kama hizi anapaswa atumiwe kwenye personal email yake bhaas.
 
Hii nchi unaweza ukajikuta unaishia kufanya kazi ya kufukuza watu na kuteua wengine, unafujuza unateua na mwisho unaamua kuirudisha nchi kwa wakoloni waiendeshe.

Haitakua mara ya kwanza kuchukua TX. Tukiwahi kuwa na nwanadheria mkuu nadhani kutoka Ghana. Pia Tume ya Keenja (Tume ya Jiji la Dar es Salaam) ilikua na mtaalamu wa mipango miji toka Ghana na ilikua na mafanikio makubwa sana.
 
Asante bwana Fuhrer kwa kutupasha haya tuliyokua hatuyajui. Ninachokuomba jiangalie sana,hawa jamaa wana jeuri yapesa wasije wakakunyamazisha milele. Bwana Mungu akulinde na amlinde mtumbua majipu mkuu. Amen
 
Nchi hii imeliwa na wajanja aisee...mpaka inatisha. Hatukatai investment...hatukatai wafanyabiashara...ila dhuluma kwa watu maskini hakuna sehemu inakubalika. Tulipe kodi watu wanyonge wafurahie kuwepo kwenye nchi yao ya Tanzania
 
Ndugu Bopwe napenda kukusahihisha kwamba TIPER hupelekwa mzigo ambao ni Financial Hold haujalipiwa kwa supplier (either by Cash or LC yenye payment terms ya 60 days) na kama mzigo umelipiwa unakuwa pump direct to the terminal/depot ya Oil Market Company. Ushuru wa importation kila kampuni inalipa on DAP basis ambapo wanalipa kwa Arrival Quantity na sio Shoretank Quantity received. Kuhusu swala la meter what i knw zile meter haiwez kuhimili pumping pressure rate za meli e.g 100-150MT/hour(KOJ) na 250MT/hour (SPM) na pia wakati mwingine zinaingiza hewa na kuendelea kusoma so zinahitaji calibration kila wakati na uwezo wa kuzitengeneza ndio huwa inakuwa shughuli cha Muhim Government watafute meter bora ambazo hazipitish hewa na pia ziweze kuhimili pumping pressure bar ya meli ili zisiweze kuharibika mara kwa mara na kuweza kutimia njia ya by pass na kuwa na watu waadilifu bandarini hapo tutakusanya kodi ipasavyo.

Mkuu kuna kitu sijakuelewa vizuri: Flowmeters zinaingizaje hewa, ungesema kuna air leakages kwenye mabomba yanayo nyonya mafuta kutoka melini kwenda kwenye pressure pumps hivyo kufanya pump isukume mafuta yaliyo changanyikana na hewa -ugesema hivyo hapo ningekuelewa.

Kitu kingine kinacho shangaza kidogo - unataka kusema wataalamu walio funga flowmeters hawana experience ya kununua flowmeters zenye uwezo wa kuhimili flow rate zote under the sun!!!

Mwisho linapokuja suala la ku calibrate measuring Instruments hilo linategemea flowmeters zina fanyakazi/tumika mara ngapi kwa mwaka kama ni mara chache basi na frequency za kufanyiwa calibration zinapungua accordingly, kwa hiyo wakati mwingine tusijaribu ku invent excuses za kulea uzembe - kwa kutoa visingizio mbali mbali, nayasema haya kwa nia njema tu namely ya kujenga.
 
nikupongeze sana mleta mada lakini sidhani kama rais hajui hili au waziri mkuu hajui. mpaka wewe umezipata hizi hata wao sina shaka kwamba wanazo. nadhani bado ni mapema mno kuweka sawa kila kitu.rai yangu kila mtu asimame kwenye nafasi yake kwa haki
huku tukiendelea na maombi kwa imani zetu Mungu hataacha kutukumbuka sisi tulionyong'oshwa ili hali si wanyonge. lakini tukumbike tuu kuiishi haki.
 
Rais na Waziri wake mkuu watapata kazi sana kusafisha hii nchi,Ningewashauri kitu kimoja kama kweli wanataka kusafisha nchi hii na siyo "kuonekana wanasafisha" wakati ukweli hakuna kitu wanachofanya.

Wapo watu katika nchi hii wanazo taarifa za mifumo ya wizi katika sehemu mbalimbali jinsi inavyofanya kazi, either wao walishiriki na sasa hawapo kwenye hiyo mirija au wanashuhudia jinsi wizi unavyoendelea ingawa wao hawausiki. Rais angetengeneza utaratibu wa watu wema wenye taarifa ya madudu yanayofanyika katika taifa hili kupeleka hizo taarifa in details wakiwa wanajulikana au hawajulikani, iwe ni choice ya mtoa taarifa.

Nina uhakika wapo watu wangejitokeza kutoa hizo taarifa nikiwapo mimi.

Mimi nina uzoefu wa jinsi mafuta yanavyoibiwa bandarini:

Kwanza niweke wazi, mafuta hayaibiwi bandarini kwa kukadiria au sijui kwa sababu ya flow meters. Hakuna kitu kama hicho. Tena zile flow meter zilikuwa na capacity ndogo na zinaharibika mara kwa mara hivyo zikiharibika inabidi ku-bypass. Meli ikiwa inashusha mafuta inaweza kushusha kwa presha ya bar 16, zile flow meter zilikuwa hazihimili presha kubwa.

Mafuta yakishashushwa, kiwango cha mafuta kilichopokelewa kina pigiwa hesabu na ma-surveyor na wanatengeneza taarifa yao. Mchezo unaanzia hapo TRA, Mafuta yanayotakiwa kulipiwa ushuru ni ya local (yanayotumika humu nchini), na ya transit hayalipiwi ushuru. Sasa figure zinazoingizwa kwenye system ya TRA kwa ajili ya kulipiwa ushuru ndiyo hapo serikali inapoibiwa.

Na anayefanya mchezo huu ni afisa wa TRA kitengo cha mafuta akishirikiana na kampuni husika. Kuna makampuni ambayo yamekubuhu kwa mchezo huo. Makampuni ya watu binafsi yakiongozwa na yanayomilikiwa na waarabu. OILCOM ndio kinara, Lake oil, World oil, CAMEL Oil, etc.

Ipo mifano mingi ila natoa mmoja.

Kuna siku ilikuwa meli na mzigo mkubwa tu kana tani laki moja na nusu, Huo mzigo ulikuwa wa OILCOM. Kwenye Cargo manifesto ya meli ulikuwa umekuwa declared kama JET A1, (mafuta ya ndege) ya transit ya kwenda Zambia. Haya yana tax exemption.

Surveyor wa mzigo alikuwa kijana mmoja anaitwa ANDERSON kutoka Intertek. Akaenda kwenye meli akapima mzigo akaambiwa na wenye mzigo kuwa aandike kuwa ni JET A1 kwenye documents zake, ingawa mzigo ulikuwa ni diesel (GO), akaahidiwa dili ikishakamilika atapewa chake. Basi Anderson machale yakamcheza akaamua kutengeneza ducument set 2, moja akadiclare ule mzigo kuwa ni JET na nyingine kuwa ni GO.

Sasa kosa ambalo walilifanya hawakumuhusisha loading master wa pale manifold. Alipoambiwa afungue line ya kwenda oilcom, Yule mzee akafungua line ya JET ya kwenda OIL com. Sasa pale KOJ manifold kuna chujio za mafuta (Strainers) kwa ajili ya kila aina ya mafuta, na zina ukubwa tofauti kwaajili ya kuchuja mafuta. Mafuta yalipoanza kusukumwa, ile strainer ya JET ikaanza kupiga kelele yaani ikawa inapitisha mafuta kwa tabu.

Loading master akaamua kuangalia kwa nini inapiga kelele, akakuta mafuta yanayopita ni diesel tena ile diesel ya high sulphur (5000ppm). Akaita kwenye radio call, " We Anderson, hiyo mnayosukuma ni JET au DIESEL?", Hakuna mtu aliyejibu kenye radio, ikabidi pump za meli zizimwe washuke kwenye meli kwenda kuongea na loading master.

Sasa ile channel ya radio inayotumiwa kwa mawasiliano inasikiwa na watu wengi wakiwemo TRA, Usalama wa Taifa, Maofisa wa Bandari, n.k, baada ya kama nusu saa, watu zaidi ya 9 wakawa wamefika pale KOJ, wakiwemo maafisa wa usalama wa Taifa.

Kuona hivyo Underson akatoka na gari akakimbia, akamwacha Depot supervisor wa OILCOM, yule kijana wa oilcom ikabidi amtaarifu mzee ISLAM mwenyewe mwenye OILCOM kuwa kimesanuka. Ilikuwa ni Jumamosi, mzee Islam akaagiza watu wote walioenda kushuhudia ile saga waende OILcom, inavyosemekana kila mtu alipewa mil 80 cash palepale kwenye mifuko ya rambo. Na mzigo baadae ukashushwa kwenye line ya diesel.

Sasa ukiangalia wizi unaofanyika kwenye mafuta siyo wizi wa mafuta ila ni ukwepaji kodi, mafuta yanakuwa declared kama transit hayalipiwi ushuru ila yanauzwa local kwa bei ile ile. Na biashara hii ya kukwepa ushuru ilikuwa inasimamiwa na mwenyewe kamishna wa kodi ya forodha Bwana Masamaki.

Mafuta yakishaingiza kama transit yanatengenezewa document zote kuanzia za loading, Checkpoint zote za TRA, clearance ya Tunduma hadi upande wa pili wa boarder, na offloading documents na documents za ZRA(Zambia Revenue Authority). Na Bond clearance.

Hizi taarifa zote Usalama wa taifa wanazijua fika, kama Magufuli akitaka kusafisha, anatakiwa apate watu wa usalama wenye mtazamo kama wake. Laa sivyo, na wao watakuwa wanawashtua waalifu kwa meseji kama prof. Muhongo.

OIL COM ndio kinara.

Yesu.wangu,............................kwani mkuu ameshalala...................... kesho ongea mkuu..............
 
Hivi nini kilitokea kwa yule mzabuni aliyepewa tenda ya kuagiza mafuta yote yanayoingizwa nchini? Kwangu mimi Oil com au any local retailer siwezi kumruhusu aseme anafanya export ta mafuta unless nina record yake ya mauzo nje ya nchi
 
Shamba la bibi,hata watumbuaji wenyewe mi naona bado ni ngonjera zinachezwa,unamtoa mtu mmoja au watatu,halafu system yote bado unaiacha!!!.
 
Mkuu nionavyo mimi TPA,TRA na wafanya biashara ya kuingiza mafuta nchini wana network ya wizi/udanganifu wa hali ya juu, haya mambo ya kusimamisha/fukuza kazi mtu mmoja mmoja hayatufikisha popote, mambo yatakuwa yanajirudia rudia miaka nenda rudi.

Sasa nini kifanyike: Wafanyakazi wote wa TPA wanaohusika na chain ya masuala ya ingizwaji wa meli za mafuta Bandarini, upakuaji wa mafuta kwenda kwenye matanki nk wote wahamishwe na kupelekwa kufanya kazi Bandari za Mwanza, Kigoma, Musoma na Bukoba - tusifanye makosa ya kuwabakiza Bandari ya Dar, zoezi hilo liwakumbe vile vile wafanya kazi wa TRA nao wahamishiwe Mikoani.

Mwisho Serikali (TPDC) ndiyo ipewe majukumu ya kuagiza mafuta in bulky kama walivyo kuwa wanafanya miaka ya nyuma waende mbali zaidi wakarabati Oil Refinery ya Kigamboni itisaidie ku-refine Crude Oil kama ilivyo kuwa Zamani - Baba wa Taifa alikuwa anaona mbali sana.

Tatizo lilikuja kuhibuka baada viongozi waliomrithi Kambarage kudanganywa na wafanya biashara wakubwa wa mafuta tukajikuta tunaua kiwanda chetu cha Kigamboni, baadae Serikali ikajitoa katika Biashara ya kuagiza mafuta chini - mimi kitendo hicho nilichukulia kama ni hujuma za makusudi, haingii akilini kwamba Viongozi hao walikuwa hawajui umuhimu Wa Serikali kusimamia masuala yote nishati ya mafuta. Dk.Magufuli afanye hima ku reverse upuuzi huu wote,saa hizi tusingekuwa tunazungumzia masuala ya ku bypass flowmeters, mabomba yaliyo fungwa kinyemela kwenye manifold, kufungwa kwa kiwanda cha ku-refine mafuta huko Kigamboni.
 
habari kama hizi watu wawe nazo makini. ..kuna mbinu nyingi sana zinatumika kuchafuana
Inawezekana mkuu, lakini kila tip ni muhimu kuifuatilia, ufanyike uchunguzi wa kina then kama niuzushi we loose nothing. Better to be safe than sorry. Kila tip ni muhimu ikafanyiwa kazi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom