USHUHUDA: Hivi ndivyo mafuta yanavyoibiwa Bandarini Dar...

Status
Not open for further replies.
Sikiliza bwana usituone sisi wapuuzi kama wameweza kuzima flow meter kwa miaka mitano itashindikaa hao kuleta huo mzigo na kufanya figisu figisu hii taarifa ifanyiwe kazi kama na wewe ni sehemu ya wizi jiandae Magufuli atakufunga

STORI YA KUTUNGA BWANA ..
Hivi kuna shule inayozidi hapa JF? MleMleta uzi ametuhabarisha hata kuzidi hizo Internet search zako, hivi ukiingia Google uka type wizi KOJ kama alivyodadavua mleta uzi utapata jibu? Acha kukariri na pia umesema kilichosemwa ni uongo, kuna bulky importers sasa tumekuambia tutajie wewe unaleta longo longo.
asiejua maana hambiwi ..muache tuu
 
habari kama hizi watu wawe nazo makini. ..kuna mbinu nyingi sana zinatumika kuchafuana
Huyo mtoa taarifa hamchafui mtu. Kaeleza ukweli kabisa tena kwa uchache sana. Huyo bwana anastahili pongezi kubwa. Kaeleza ukweli mtupu. Mbona mimi namjua mwizi mmoja na Mali zake zote. Anatisha. Waweza sema Ana ubia na mungu. Kaka Acha tu
 
Aisee hivi Jakaya amepewa ukuu wa UDSM kwa kipi ?? Kuna kila sababu ya kubadilisha sheria inayokataza Rais wa Nchi asifunguliwe mashtaka ,huyo alitakiwa awepo kwenye house of arrest mpaka tunapo ongea hivi sasa,kama Magufuli dhamira yake ni ya dhati aanze na kufuta hiyo sheria then anyonge watu kama kumi hivi ndio mambo mengine yaendelee ,vinginevyo anampigia mbuzi gitaa
Kama wewe hujakosea popote kua wa kwanza kuendekeza mswada
 
Umeandika siku ya deal kulikua na meli ya Oil com(Uongo oil com hawaleti meli siku hizi) halafu unasema huu mzigo umekua declared kama Jet1 ..ati hiya yana Tax excemption ! Kwa Diesel ya transit ina lipa ushuru..wacha ujinga wewe kama huna kitu wacha choyo piga kazi upate..chuki kwa waarabu haikufikishi mahali utakufa na kijiba bure.
Na inshangaza watu humu waingia kichwa kichwa kila kinacho andikwa humu..watu wajabu kabisa
Unaandika kama vile mwarabu au muhindi utakuwa ndio jipu HILI
 
Rais na Waziri wake mkuu watapata kazi sana kusafisha hii nchi,Ningewashauri kitu kimoja kama kweli wanataka kusafisha nchi hii na siyo "kuonekana wanasafisha" wakati ukweli hakuna kitu wanachofanya.

Wapo watu katika nchi hii wanazo taarifa za mifumo ya wizi katika sehemu mbalimbali jinsi inavyofanya kazi, either wao walishiriki na sasa hawapo kwenye hiyo mirija au wanashuhudia jinsi wizi unavyoendelea ingawa wao hawausiki. Rais angetengeneza utaratibu wa watu wema wenye taarifa ya madudu yanayofanyika katika taifa hili kupeleka hizo taarifa in details wakiwa wanajulikana au hawajulikani, iwe ni choice ya mtoa taarifa.

Nina uhakika wapo watu wangejitokeza kutoa hizo taarifa nikiwapo mimi.

Mimi nina uzoefu wa jinsi mafuta yanavyoibiwa bandarini:

Kwanza niweke wazi, mafuta hayaibiwi bandarini kwa kukadiria au sijui kwa sababu ya flow meters. Hakuna kitu kama hicho. Tena zile flow meter zilikuwa na capacity ndogo na zinaharibika mara kwa mara hivyo zikiharibika inabidi ku-bypass. Meli ikiwa inashusha mafuta inaweza kushusha kwa presha ya bar 16, zile flow meter zilikuwa hazihimili presha kubwa.

Mafuta yakishashushwa, kiwango cha mafuta kilichopokelewa kina pigiwa hesabu na ma-surveyor na wanatengeneza taarifa yao. Mchezo unaanzia hapo TRA, Mafuta yanayotakiwa kulipiwa ushuru ni ya local (yanayotumika humu nchini), na ya transit hayalipiwi ushuru. Sasa figure zinazoingizwa kwenye system ya TRA kwa ajili ya kulipiwa ushuru ndiyo hapo serikali inapoibiwa.

Na anayefanya mchezo huu ni afisa wa TRA kitengo cha mafuta akishirikiana na kampuni husika. Kuna makampuni ambayo yamekubuhu kwa mchezo huo. Makampuni ya watu binafsi yakiongozwa na yanayomilikiwa na waarabu. OILCOM ndio kinara, Lake oil, World oil, CAMEL Oil, etc.

Ipo mifano mingi ila natoa mmoja.

Kuna siku ilikuwa meli na mzigo mkubwa tu kana tani laki moja na nusu, Huo mzigo ulikuwa wa OILCOM. Kwenye Cargo manifesto ya meli ulikuwa umekuwa declared kama JET A1, (mafuta ya ndege) ya transit ya kwenda Zambia. Haya yana tax exemption.

Surveyor wa mzigo alikuwa kijana mmoja anaitwa ANDERSON kutoka Intertek. Akaenda kwenye meli akapima mzigo akaambiwa na wenye mzigo kuwa aandike kuwa ni JET A1 kwenye documents zake, ingawa mzigo ulikuwa ni diesel (GO), akaahidiwa dili ikishakamilika atapewa chake. Basi Anderson machale yakamcheza akaamua kutengeneza ducument set 2, moja akadiclare ule mzigo kuwa ni JET na nyingine kuwa ni GO.

Sasa kosa ambalo walilifanya hawakumuhusisha loading master wa pale manifold. Alipoambiwa afungue line ya kwenda oilcom, Yule mzee akafungua line ya JET ya kwenda OIL com. Sasa pale KOJ manifold kuna chujio za mafuta (Strainers) kwa ajili ya kila aina ya mafuta, na zina ukubwa tofauti kwaajili ya kuchuja mafuta. Mafuta yalipoanza kusukumwa, ile strainer ya JET ikaanza kupiga kelele yaani ikawa inapitisha mafuta kwa tabu.

Loading master akaamua kuangalia kwa nini inapiga kelele, akakuta mafuta yanayopita ni diesel tena ile diesel ya high sulphur (5000ppm). Akaita kwenye radio call, " We Anderson, hiyo mnayosukuma ni JET au DIESEL?", Hakuna mtu aliyejibu kenye radio, ikabidi pump za meli zizimwe washuke kwenye meli kwenda kuongea na loading master.

Sasa ile channel ya radio inayotumiwa kwa mawasiliano inasikiwa na watu wengi wakiwemo TRA, Usalama wa Taifa, Maofisa wa Bandari, n.k, baada ya kama nusu saa, watu zaidi ya 9 wakawa wamefika pale KOJ, wakiwemo maafisa wa usalama wa Taifa.

Kuona hivyo Underson akatoka na gari akakimbia, akamwacha Depot supervisor wa OILCOM, yule kijana wa oilcom ikabidi amtaarifu mzee ISLAM mwenyewe mwenye OILCOM kuwa kimesanuka. Ilikuwa ni Jumamosi, mzee Islam akaagiza watu wote walioenda kushuhudia ile saga waende OILcom, inavyosemekana kila mtu alipewa mil 80 cash palepale kwenye mifuko ya rambo. Na mzigo baadae ukashushwa kwenye line ya diesel.

Sasa ukiangalia wizi unaofanyika kwenye mafuta siyo wizi wa mafuta ila ni ukwepaji kodi, mafuta yanakuwa declared kama transit hayalipiwi ushuru ila yanauzwa local kwa bei ile ile. Na biashara hii ya kukwepa ushuru ilikuwa inasimamiwa na mwenyewe kamishna wa kodi ya forodha Bwana Masamaki.

Mafuta yakishaingiza kama transit yanatengenezewa document zote kuanzia za loading, Checkpoint zote za TRA, clearance ya Tunduma hadi upande wa pili wa boarder, na offloading documents na documents za ZRA(Zambia Revenue Authority). Na Bond clearance.

Hizi taarifa zote Usalama wa taifa wanazijua fika, kama Magufuli akitaka kusafisha, anatakiwa apate watu wa usalama wenye mtazamo kama wake. Laa sivyo, na wao watakuwa wanawashtua waalifu kwa meseji kama prof. Muhongo.

OIL COM ndio kinara.


Mie hii thread imenichosha hapa tu
 
Huo ni uongo uwezo wa meli kushusha KOJ ni meli isiyozidi Tani 35 KT na above that inashushia SPM au single mooring Point ambayo inashusha Diesel peke yake 70KT to 100KT mleta mada usidanganye watu KOJ haiwez kuhimili meli inayobeba Tani laki moja utakuwa umesimuliwa
 
Halafu swala jingine inaonekana kuna vitu huvijui vizuri as per TBS requirement for Diesel au Gasoil inayotakiwa ni low sulpher 500 ppm na sio hiyo uliyoitaja na ilianza kutumika January 2015 before hapo tulikuwa tunatumia 50ppm. Mafuta yote yanayoingia nchini yanakuja kwa Bulk supply na kusimamiwa na PIC zamani sasa ni PBPA as government agency ambazo tangu waanze kuleta mafuta hakuna meli iliyoleta mafuta 150 KT haijawah kutokea na unatakiwa kufahamu delivery zinakuwa tano(sawa na meli nne mpka tano kulingana na mahitaji ya mwezi huo) kwa supply ya mwez mmoja meli za Gasoil au diesel 2 zenye uwezo wa kubeba 70 KT to 100 KT na hizi zote hushushia SPM ambayo ipo deep sea na KOJ hushusha Motor Spirit Premium/Unleaded petroleum/Petrol na Jet A1/IK na meli inayobeba Jet A1 huwa inakuwa Comb of Either petrol and Jet A1 au Gasoil & Jet A1 na meli hizo hazizidi kwa product zote 30KT to 38KT. As per shipping and supply contract.
 
Nashauri kuwe na jukwaa la WHISTLE BLOWING, kwa ajili ya wale wazalendo walio ktk mfumo na wanaona madudu yakifanywa ila hawana pa kuanzia, wadondoshe nondo humu, NINA uhakika Magufuli habari zitamfikia tu. Jf ni zaidi


Mimi nina ushahidi bila chenga kuwa taarifa za uhakika zikimfikia Mheshimiwa Magufuli huwa anazifanyia kazi; mradi habari hizo ziwe zimefanyiwa kazi vizuri na ni za kweli!!
 
....watu zaidi ya 9 wakawa wamefika pale KOJ, wakiwemo maafisa wa usalama wa Taifa.... mzee Islam akaagiza watu wote walioenda kushuhudia ile saga waende OILcom, inavyosemekana kila mtu alipewa mil 80 cash palepale kwenye mifuko ya rambo. Na mzigo baadae ukashushwa kwenye line ya diesel.

Hukumalizia story. Sasa, kama na wewe ulikuwa shuhuda kama unavyosema, ilikuwaje hukualikwa kwenda kupewa mil 80 kama mashuhuda wenzako?
 
Mungu tusaidie,kama Kuna watu WA usalama fanyieni kazi taarifa hii.
mkuu wakati umesoma hapo na umeambiwa hao watu 9 nawana usalama nao walikuwepo wote wakalambishwa mlungula na wakapiga kimya hapa unawaomba wana usalama wapii??

hii serikali kila mahali hakufai na mijizi ishajiwekea watu wao ili wawe wanapata kila kitu watakacho ndani ya nchi.hii na wamejiimalishia ulinzi vya kutosha pia
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom