Za leo ndu wapendwa, mimi nimeolewa na mda wa mwaka na nusu sasa. Hapo nyuma niliwahi kuwa na boyfriend tuliye kaa naye kwa mda wa miaka mitatu hivi. Huyu X-bf alikujakufahamu kuwa niliolewa na akafanya juhudi sana kutafuta no. yangu ya simu mpya. Ss huwa ananipigiaaga na kutunimia messages za mapenzi. Nimemkataza lakini haonyeshi kunielewa kabisa, mpaka sasa nimeamua kukaa kimya ila ndo kama vile amezidisha kutuma sasa. Kwa ajili ya kujiweka in a safe position, nilimwambia hata mume wangu lakini hakusema kitu alibakia kunyamaza tuu. Sasa naombeni msaada katika hili swala maana linanikera sana sana. Nifanye nini?