Ushauri wenu tafadhali, niko njia panda

Hapana sister me kwa mtazamo wangu naona kama umepata kamchepuko maaana hapo sioni tatizo kama kweli unampenda coz linarekebishika hilo kaa nae chini umwambie nini unataka afanye kama mwanaume anayejielewa sio kumuacha bila kuongea nae hapo utakuwa umefanya kosa

Ni vigumu kumbadili mtu life style yake.. Labda wampeleke JKT then akapige na JWTZ huko taaluma hyo wanayo.. Lakin kwa huyu dada mnajidanganya... Anajua urithi upo
 
Kunatofauti kubwa kati ya mvulana na mwanaume. Kukaaa home miaka yote hiyo bila sababu ya msingi ni uoga wa maisha. Ushauri wangu tafuta wa type yako.... Ndoa ni safari ndefu. Huyo mvulana achana naye maana inaonekana ana mind set za form six, na isitoshe hata kitanda hana


Tena wavulana wa hivi ukiishi nao jambo dogo tu anaenda kusema kwa mama yake, asipoangalia maamuzi yoteee ya familia yatakuwa yanafanyika kwa mama mkwe, atafute mwanaume tu, wavulana sio kabisa.
 
Tafuta ambaye unaona yupo perfect kwako. huyo mwenzio hana presha ya maisha. wewe wala usimlaumu wapo wanaompenda wa type hyo. mimi sioni kama ana kosa ila wewe ndo unia makosa kwa kuwa na mume tajiri au maskini ni uamuzi wako.
sijaelewa kosa langu hapo nilipi
 
Mwambie dukuduku lako lililo moyoni kuhusu penzi lenu kama ni mtu wa kubadilika na ana nia ya kuwa nawe kama mkewe basi atabadilika ukiona yupo yupo tu baada ya miezi miwili/mitatu hana mwelekeo chapa lapa uchakarike kivyako vyako.
 
Mwambie dukuduku lako lililo moyoni kuhusu penzi lenu kama ni mtu wa kubadilika na ana nia ya kuwa nawe kama mkewe basi atabadilika ukiona yupo yupo tu baada ya miezi miwili/mitatu hana mwelekeo chapa lapa uchakarike kivyako vyako.
Asante BAK,nimekuelewa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Habari wana Jamii Forum,

Mi ni binti niko kwenye mahusiano na kijana mmoja ambaye anafanya kazi mwaka wa nne huu kwenye ofisi fulani,
Elimu yake ni degree, kinachoniweka njia panda ni kwamba kwa miaka yote hiyo anaishi nyumbani kwao na yuko kwenye late 20's. Mimi nilipomaliza chuo sikupata kazi hivyo nilisota sana kitaani na tumemaliza mwaka mmoja wote ye akapata kazi mwaka huo huo.

Baada ya miaka mitatu ndio nimapata mtaji nikaanza kufanya biashara,ambapo naisapoti familia yangu 80% coz nimetoka familia ya chini sana. Pamoja na hayo mwezi ujao ntaanza kujitegemea,na hata mwaka haujaisha tangu nimepata hicho kimtaji,na simtegemei kwa chochote huyu mwanaume.

Napata mawazo naona kama huyu ni mtoto wa mama sababu kwao wako vizuri kiasi chake hakuna wanaomtegemea ila baado anakaa kwao. Mi naona sitaweza kuishi na mwanaume wa hivi kwa sababu ya nature ya maisha yangu na jinsi nnavyo hustle hard nafikiria kumuacha.

Sijui mnanishaurije

haya bhana, nashukuru kwa kuja kuntangaza. usipate tabu, kabla hujaniacha ghafla, ngoja nianze kukuacha mimi taratibu.
 
Kama mmeanza uhusiano January mwaka huu kimbia na viatu mkononi. Hayo mambo ya kutaka kubadilisha tabia mtoto wa mwanamke mwenzio sio kabisa. Hivi mama yake hajamfukuza hapo home? hehehe, aisee.
Mahusiano tumeanza January mwaka huu,ntajaribu kwa uwezo wangu kumshauri nione kama atabadilika
 
Back
Top Bottom