Ushauri wenu tafadhali, niko njia panda

afrique

JF-Expert Member
Jun 28, 2012
509
135
Habari wana Jamii Forum,

Mi ni binti niko kwenye mahusiano na kijana mmoja ambaye anafanya kazi mwaka wa nne huu kwenye ofisi fulani,
Elimu yake ni degree, kinachoniweka njia panda ni kwamba kwa miaka yote hiyo anaishi nyumbani kwao na yuko kwenye late 20's. Mimi nilipomaliza chuo sikupata kazi hivyo nilisota sana kitaani na tumemaliza mwaka mmoja wote ye akapata kazi mwaka huo huo.

Baada ya miaka mitatu ndio nimapata mtaji nikaanza kufanya biashara,ambapo naisapoti familia yangu 80% coz nimetoka familia ya chini sana. Pamoja na hayo mwezi ujao ntaanza kujitegemea,na hata mwaka haujaisha tangu nimepata hicho kimtaji,na simtegemei kwa chochote huyu mwanaume.

Napata mawazo naona kama huyu ni mtoto wa mama sababu kwao wako vizuri kiasi chake hakuna wanaomtegemea ila baado anakaa kwao. Mi naona sitaweza kuishi na mwanaume wa hivi kwa sababu ya nature ya maisha yangu na jinsi nnavyo hustle hard nafikiria kumuacha.

Sijui mnanishaurije
 
mmmmmh wanaume wenye kupenda kuwa tegemez hivyo kwa wazazi wakw hata akiwa na kazi ni balaa, hapendi kufikir , aishiwe asiiahiwe msosi utapikwa akikuoa huyo jiandae kulea famili na ukimuudhi , akitaka fanya jambo lolote anamuuliza mama
 
Katika miaka yake hiyo minne ndani ya ajira kuna kitu chochote cha maana ambacho amekifanya cha maendeleo???
Huyo kijana anaonekana bado hajajitambua sawasawa...
Huyo ni mtoto wa kiume na sio mwanaume!
 
Ulishaongea naye kuhusu hilo kabla ya kuja kuomba ushauri hapa? hata hivyo mwenye maamuzi ya mwisho ni wewe mwenyewe.
 
aiseee kuna rafiki yangu tulitafautiana sababu ya tabii hii ya kuwa hom dependant, yan hata vocha basi simu nyumbani, tulimaliza chuo miaka 2 anafanya kazi yupo kwao, nikaona huyu kiazi......
wanadeka kweli, sijui ni last born, sijui kabila....
hebu ni pm kabila la jamaa nione isihekuwa kabila moja na huyu ninae muongelea.... sitak kuanzisha ugomvi hapa
 
Kunatofauti kubwa kati ya mvulana na mwanaume. Kukaaa home miaka yote hiyo bila sababu ya msingi ni uoga wa maisha. Ushauri wangu tafuta wa type yako.... Ndoa ni safari ndefu. Huyo mvulana achana naye maana inaonekana ana mind set za form six, na isitoshe hata kitanda hana
 
Katika miaka yake hiyo minne ndani ya ajira kuna kitu chochote cha maana ambacho amekifanya cha maendeleo???
Huyo kijana anaonekana bado hajajitambua sawasawa...
Huyo ni mtoto wa kiume na sio mwanaume!
Hajafanya investment yoyote ile,anaofanya nao kazi walio chini yake wana maisha mazuri tu na maendeleo wanayo
 
aiseee kuna rafiki yangu tulitafautiana sababu ya tabii hii ya kuwa hom dependant, yan hata vocha basi simu nyumbani, tulimaliza chuo miaka 2 anafanya kazi yupo kwao, nikaona huyu kiazi......
wanadeka kweli, sijui ni last born, sijui kabila....
hebu ni pm kabila la jamaa nione isihekuwa kabila moja na huyu ninae muongelea.... sitak kuanzisha ugomvi hapa

Naona unataka kuanza kutongoza kijanja:confused:
 
Kunatofauti kubwa kati ya mvulana na mwanaume. Kukaaa home miaka yote hiyo bila sababu ya msingi ni uoga wa maisha. Ushauri wangu tafuta wa type yako.... Ndoa ni safari ndefu. Huyo mvulana achana naye maana inaonekana ana mind set za form six, na isitoshe hata kitanda hana
asante kwa ushauri,noted
 
Binti km unaitajii kua mfanyakazi kwao wa kuingalia family just endelea nae.....!!!! Ila ungeachana nae utafute yule anaejua Ku hangaika,
 
Ulishaongea naye kuhusu hilo kabla ya kuja kuomba ushauri hapa? hata hivyo mwenye maamuzi ya mwisho ni wewe mwenyewe.

Sijaongea naye ila soon ntaongea naye nimwambie kabisa kua siwez
 
Dada hata hivyo mm naona unachelewa Huo ni mzigo kwako kwa maisha ya sasa yanaitaji ambae ni mpambanaji hapo anakazi je ikitokea kasimamishwa ghafla? Automatically atarudi kunyonya kwa mama yake achana nae bado ananuka maziwa huyo Sio size yako hata kumuuliza usimuulize.
 
Honestly huwa sipendi kushauri mtu kuvunja uhusiano bila kujua black and white ya side B coz there is a time to regret for a wrong decision.
Unahisi kuna sababu za kutosha kueleweka kwa nini anakaa kwao todate?????
 
Dada hata hivyo mm naona unachelewa Huo ni mzigo kwako kwa maisha ya sasa yanaitaji ambae ni mpambanaji hapo anakazi je ikitokea kasimamishwa ghafla? Automatically atarudi kunyonya kwa mama yake achiana nae bado ananuka maziwa huyo Sio size yako hata kumuuliza usimuulize.

kuna rafiki naye aliolewa na mwanaume ambaye alikua type hii,no investment no what,akasimamishwa kazi ghafla,yaaani huezi kuelewa maisha yao yalivyomagumu sa hivi ,hata kodi ya chumba kimojawanaume hawez kulipa,mwanamke anatoka sa 12 asibuhi anamuacha mwanaume anavuta shuka hadi sa 6 mchana
 
Dada hata hivyo mm naona unachelewa Huo ni mzigo kwako kwa maisha ya sasa yanaitaji ambae ni mpambanaji hapo anakazi je ikitokea kasimamishwa ghafla? Automatically atarudi kunyonya kwa mama yake achana nae bado ananuka maziwa huyo Sio size yako hata kumuuliza usimuulize.
ntaongea naye ajue msimamo wangu,na ikitokea tofauti kidogo anasema namtaftia sababu,so nataka ajue sababu kabisa
 
Back
Top Bottom