Mama mkwe kamtorosha Mke wangu, nifanye nini niko njia panda

Pleasepast

JF-Expert Member
May 30, 2023
325
454
Habarini za usiku wapendwa

Naomba kwa wenye ufahamu na mambo haya wanijuze nifanye nini kwasababu niko njia panda iko hivi mke wangu tulikosana kidogo akaenda kwao amekaa wiki mbili nimeenda kwa lengo la kuona mtoto lakini cha ajabu walipo pata taarifa kwamba naenda tu Mama mkwe amemtorosha mke wangu na wote hawatoi ushirikiano simu hawapokei wala kujibu sms yani ni kama hawataki mawasiliano kabisa na wakati tuna mtoto pamoja

Naomba msaada kwa mwenye uzoefu na mambo haya
 
Kausha mradi unajua yuko kwao endelea na mambo mengine, wakimchoka/akichoka atarudi mwenyewe.

Sent from my TECNO BE6 using JamiiForums mobile app
 
Kausha mradi unajua yuko kwao endelea na mambo mengine,wakimchoka/akichoka atarudi mwenyewe.

Sent from my TECNO BE6 using JamiiForums mobile app
Kwao nimeenda hayupo na kuna taarifa nimesikia kwamba ameenda nje ya mkoa japo sina uhakika nazo mimi mwenyewe nawaza nimpotezee kwasababu hataki mawasiliano labda siku akihitaji matumizi ya mtoto atanitafuta yeye mwenyewe
 
Mwanaume muungwana hupata Mwanamke wa hovyo,
Na mwanamke mstaarabu hupata mwanaume pasua kichwa

Kwao Mwanamke Hawajui Kujenga Wanajua Kuboa Ndoa, Sijajua Ulichosahau Kwao Mwanamke Ni Nini?

Shukuru Mungu Picha Umeiona, kazi ni kwako!

Simama kama mwanaume kumkosa kwao sio shida,
Na wewe tafuta namna wakija wajute kubeep!

Ila pia ni somo ikitokea ukataka kuoa tena nenda walipo wazazi wote na uhakikishe baba ndo final say
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom