ushauri wapendwa si mimi ni ...

anawaza atafanyaje au atatoka vip ndani ya hiyo ndoa
je anaweza kwenda mahakamani ili aweze kusaidiwa ?

hayupo serious huyo, karidhika na hayo maisha, anawaza atatoka vipi? hivi ni kitu cha kuwaza hicho, labda aseme yeye bado ana mapenzi na mumewe tumuelewe.....
 
haaa ZD ,nyamayao,Pretty,MJ1 , leo mbona my head iko empty jamani ni nini?
Carmel yuko wapi ??
 
msindima kwa imani nguvu ya mungu ipo na inafanya kazi lakini ndo majibu hayawezi kuonekana leo au kesho sometimez inatake time

Ni kweli kabisa nguvu ya Mungu ipo,lakini kubadilika kwa mtu kunamtegemea mtu mwenyewe,mfano labda mtu unakuta ana tabia ya ugomvi unaweza ukaomba miaka nenda miaka rudi na asibadilike mpaka yeye mwenyewe atakapoamua kubadilika,Mungu hakulazimishi wewe ubadilike ni wewe uamue kubadilika na kuhitaji msaada wa Mungu hapo ndo tutaona mabadiliko.
 
kuna member mmoja humu anaamini hakuna Mungu, sasa huyo ndio mumeo utamuombea kivipi na yeye haamini? wacheni bwana anaeombewa nae aonyeshe dalili za mabadiliko, sio kuomba tu wakati mtu hayupo huko..........

Nyamayao naunga mkono hoja,nimeipenda sana hiyo yenye red color,anaeombewa nae anapaswa kuonyesha dalili za mabadiliko,kama hakuna hata dalili ni ngumu kuendelea kumuombea,na ndo maana nilisema kuwa kubadilika kwa mtu kunamtegemea yeye mwenyewe kama hayuko tayari hata tuombe na kufunga ni bure hatutaona changes zozote sana sana tutashuhudia vituko vikizidi siku hadi siku.
 
'Je! watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana? Amos 3:3'.

mimi naona mapatano masuluhisho nk yanawezekana tu kama wote wanakubaliana kupatana na kuendelea na ndoa, vinginevyo bora Q apaki mabegi yake aangalie ustaarabu mwingine, sio lazima a file divorce direct, wanaweza kuwa tu separated kwanza halafu Q aangalie hali inavyoendelea na awe tayari kwa lolote, kurudi kwa mumewe kama ataonyesha kubadilika au ku anza mbele kama kuondoka kwake kutakuwa ni sawa na kumnyima punda mbaazi...
 
Hivi lini wazazi wataacha kuingilia maisha ya watoto wao na kuwaacha wachague wenza wao wenyewe? Haya sasa hapo bibie kashaambiwa yeye hakua chaguo lake ata semaje tena?
Mwana F1
kILICHOTOKEA HAPA SIYO KUINGILIA BALI KU -INFLUENCE.Wakati mwingine kama mzazi, unatamani mwanao aoe au kuolewa na mtu kutoka familia unayoifahamu.Sidhani hawa wanandoa walilazimishwa bali walijengewa mazingira ya kushamiri na kustawisha uhusiano wao.Ninachokiona hapa ni kule kuchukua muda mfupi wa kufahamiana na kutangaza ndoa.Huenda wangekaa kipindi cha kutosha, ulevi wa jamaa ungeonyesha ni kero bayana, huenda jamaa angemkinai binti na kuona siyo chaguo lake.
Maadam maji yameshamwagika, tuwashauri nini cha kufanya.Nitashauri kama hivi;
1. Kutegemeana na imani zao, wangejaribu kuwa na mazungumzo yao wenyewe kwanza ili watafakari tena maana ya viapo vyao.Kama ni vile viapo vya hadi kifo kiwatenganishe, basi wajaribu kutafutana yale mazuri wanayoyaona kama wanandoa na kuyaendeleza na kuendelea kuishi.
2. Wajisachi ni maeneo gani kila mmoja hayapendi kuhusu mwenzie kisha wapange namna ya kuyakabili
3. Wawaone washauri nasaha kama wenyewe wameshindwa kufikia muafaka
4. Kama imani zinaruhusu kuachana, na kama kila jitihada zimeshindikana basi waachane au watengane.
 
Ni kiasi cha kwenda na kuwaeleza wazazi juu ya tabu hii then wataamua! Unajua ni rahisi kuambiwa amvumilie mlevi kuliko yule aliyetamka kabisa kuwa si choice yake. Otherwise Yeye ndie mvaa kiatu so anajua wapi kinambana zaidi so blahblah za vumilia azipime kwanza na situation yenyewe!!
...Haya mambo kila mkipalangana na mwenzio ndani ukimbilie kushitaki kwa wazee/wazazi, sijui mshenga na wazee wa kanisa mnajidanganya tu...Kama mambo yamewazidi ni nyie wenyewe wa kuamua hatma yenu. Kumbuka hao wazee/wazazi baada ya kikao wanaondoka mnabaki peke yenu wawili na mwenza wako...mh! mnarudi kule kuleee!!! Me i don't believe on this kuwashtakia wazazi....amueni, zungumzeni, mnafikia muafaka na maloveee yanaendelea na kama itakuwa ni pingili basi mtaamua wenyewe kubwaga manyanga...
 
'Je! watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana? Amos 3:3'.

mimi naona mapatano masuluhisho nk yanawezekana tu kama wote wanakubaliana kupatana na kuendelea na ndoa, vinginevyo bora Q apaki mabegi yake aangalie ustaarabu mwingine, sio lazima a file divorce direct, wanaweza kuwa tu separated kwanza halafu Q aangalie hali inavyoendelea na awe tayari kwa lolote, kurudi kwa mumewe kama ataonyesha kubadilika au ku anza mbele kama kuondoka kwake kutakuwa ni sawa na kumnyima punda mbaazi...

nimependa ushauri wako Triplets thanks so very much
 
Dah kama ni wewe nakupa pole mama F1 nasikia jamaa wanao soma Urusi wanapiga sana ulabu
 
Triplets

Ushauri wako umekaaaa vyema sana na niwakibusara sana na baadhai wa watu nimerishudia hilo likifanyika na wengine hujirudi na wengine husepa mazima no baby come back no more,

Ila kwa huyo sister yangu hapo ipo kazi kweli kweli Kijana ati kasomea Urusi?? Na ndipo tatizo lilipoanzia kwani nami nimeisha fundishwa na walimu wangu wawili kutokea Urusi na ndoa zao zilikuwa na matatizo mpaka twamaliza secondary kweli walimu hao walikuwa walevi kupindukia.

Dada nakuomba umwambie akapumzike kwao kwa muda wajaribu kusuruhisha mammbo kama patakuwa hapatoshi waaangalie ustaarabu mwingine wa maisha yao kila mmoja kivyake period.

Duuhh ni issue nzito sana hiyo
 
Pole sana kwa ndoa ndoano yako ndugu yangu. Mi nakuomba usiondoke, ila jaribu kutafuta ushauri, hata viongozi wa dini wanasaidia sana katika hali ya namna hiyo, unaweza kumrudia mchungaji aliyewaweka pamoja ukamwelezea yote kisha omba kukutanishwa na mwenzio ili muweze kuangaliana na kusema kwa uwazi, mimi nina hakika maneno matakatifu ya biblia yanaweza mbadili japo kiasi. Maana ukisema uondoke katika ndoa hiyo huwezi jua unaweza kujuta baadae, maana hata rafiki utakayempata ukimsimulia atakwambia wewe sio mvumilivu na hukujaribu kufuata utaratibu kumsaidia mwenzio. Pombe ni kitu mungu alikiumba jaribu ushauri huu, inaweza kusaidia.
 
ushauli wako mzuri pia jethro
naomba nitoke nje ya mada kidogo samahani we ni Me/Ke
asante
 
Pole sana kwa ndoa ndoano yako ndugu yangu. Mi nakuomba usiondoke, ila jaribu kutafuta ushauri, hata viongozi wa dini wanasaidia sana katika hali ya namna hiyo, unaweza kumrudia mchungaji aliyewaweka pamoja ukamwelezea yote kisha omba kukutanishwa na mwenzio ili muweze kuangaliana na kusema kwa uwazi, mimi nina hakika maneno matakatifu ya biblia yanaweza mbadili japo kiasi. Maana ukisema uondoke katika ndoa hiyo huwezi jua unaweza kujuta baadae, maana hata rafiki utakayempata ukimsimulia atakwambia wewe sio mvumilivu na hukujaribu kufuata utaratibu kumsaidia mwenzio. Pombe ni kitu mungu alikiumba jaribu ushauri huu, inaweza kusaidia.

thanks sydney message itamfikia mhusika
 
kina dada kuna kitu nimekaa usiku kabla sijalala nimewaza sana juu ya huyu dada sijapata jibu
kama mjuavyo ndoa zetu za kikristo zinasema kilichounganishwa duniani na mbiguni kkimeunganishwa hakuna mwanadamua anayeweza kukitenganisha

Swali ...Kama huyo Bibie kwa sasa ana miaka 27 akitoka kwa mmewe itakuwaje kama in future atahitaji kuwa na watoto wake na kiumri bado ni mdogo hataweza kuwa na mahusiano na mtu mwingine na kuyaita mahusiano halali yaani aishi nae kama mme na mke ???

Y kwa nini??

Mimi jamani nachukia!! Kusema kweli mambo ya ndoa ni magumu but all I can say ni kwamba inapofikia mahali its beyond repaireble sidhani kama kuna haja ya kuangalia alichokiunganisha sijui nani aanze mbele asimame kwanza kwa miguu yake miwili then yatakayojiri baada akubaliane nayo tu. Akishahakikisha muda wa kutosha umepita basi akimpata wa kwake ajizalie mwana kwanza kisha mambo yanakuwa mazuri kwa sababu hata kanisani ndoa itavunjwa kwani itahesabika kama amefanya uasherati ambao inampa mamlaka padri kuivunja ndoa yake ya awali.

Kisha anatubu na kurudishwa kundini na mumewe mpya then wanabariki ndoa.
 
...Haya mambo kila mkipalangana na mwenzio ndani ukimbilie kushitaki kwa wazee/wazazi, sijui mshenga na wazee wa kanisa mnajidanganya tu...Kama mambo yamewazidi ni nyie wenyewe wa kuamua hatma yenu. Kumbuka hao wazee/wazazi baada ya kikao wanaondoka mnabaki peke yenu wawili na mwenza wako...mh! mnarudi kule kuleee!!! Me i don't believe on this kuwashtakia wazazi....amueni, zungumzeni, mnafikia muafaka na maloveee yanaendelea na kama itakuwa ni pingili basi mtaamua wenyewe kubwaga manyanga...

Ni kweli usemayo Laligeni but nimesema hayo kwa kuwa influence ya hawa kuwa pamoja imeanzia kwa wazazi na isitoshe kama mwenzio hana mpango wowote wa kulizungumzia hili kwa kuwa anaona hakuna issue mtayamalizaje? Ufunge mizigo kimya kimya uondoke? Hutaeleweka na bado unawezarudishwa ukaambiwa kuna chance ya kushauriwa na kupatanishwa wakati ukipitia kwao kwanza hata ukijaondoka hakuna atakayekuuliza kwani watakuwa wanajua!

But yeah all in all uamuzi wanao opsss anao bibie maana nditye mvaa kokoko ati!
 
pole zake huyo mdada, yaani hata sijui tumsaidiaje.
kosa ni lake mwenyewe na yeye alikubalije kwenda kanisani kufunga ndoa na mtu ambaye hamfahamu? kumfahamu nina maana kujua current tabia zake. wew unafunga ndoa na mtu eti wazazi ni family friend ndo unasacrifice maisha yako yote? hapo kwa kweli alichemsha.
kwa ushauri tu ni kwamba, ni sawa ndoa ya kanisani haitenganishwi na binadamu, lakini kwa swala hilo anaweza akachukua break kidogo. arudi kwao akatulie, na asali sana kuomba Mungu ambadilishe huyo mume. kuendelea kukaa kwa huyo mume kutamwongezea stress, maana kila akimuona anawaza kuwa nakuja kusimangwa, na hilo la kusimangwa ndo linaudhi sana. Huyo mume kama atamuhitaji basi atajirekebisha na wataendelea kuishi vizuri. umri wake unamruhusu kukaa nyumbani hata kwa 5 years akisubiri Mungu atende Miujiza. asikate tamaa.
Ila kusema ampeleke sijui kwa mchungaji au ndugu au wapi haitasaidia, hilo ndo litabia lake kwa sasa.
 
yaani inatokea sana kuna mwingine kafanyiwa kparty juzi anauliza sasa huyu mwanaume jamani mie nitaanzaje nae huko room maana naenda kukutana nae harusini tu kwa mala ya kwanza yuko ovasizi sijui ndo anakuja kufunga ndoa na kuondoka
sijui wamepima ???
 
huyo dada namshauri afanye uhamuzi binasfi ambao anadhani utamfanya afurahie maisha yeye kama yeye, regardless of parents, that all na pia ajue si yeye peke yake anaekumbana na matatizo kama hayo, wapo wengi so asijione kama mbuyu baharini, what she needs if to find light at the end of tunnel, na sio kuwa mchunga nyumba, WAKE UP AND DO SOMETHING!
 
ni mahusiano na urafiki wa familia zao ndio uliopelekea yeye na mwenzi wake kuwa wife & husband mwaka mmoja na nusu sasa

Mwanaume alikuwa anasoma urusi -mwanamke akiwa TZ anafanya kazi kutokana na ukaribu wa familia zao na maelewano ..ndipo wakaamua wafanye muunganiko kati ya sistery and brother
mahusiano ya muda mfupi yakafanyika na ndoa takatifu ikafungwa
Sasa ndani ya nyumba mme hashikiki ni mlevi kupindukia anarudi usiku wa manane akirudi home bibie hapewi haki yake na akipewa ni kwa ugomvi na masimango
eti we Q sio choise yangu ni family ndo zilituunganisha imekuwa kama wimbo wa Taifa
Q anauliza je aondoke katika hii ndoa ya masimango au afanye nini

INDOCTRINATION!!! wote waliosoma urusi wameharibiwa kisaikolojia na warusi. si kosa lake
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom