Swali la wanawake wanatoa nini kwenye mahusiano zaidi ya ngono ni la kipuuzi

mamamzungu

JF-Expert Member
Nov 17, 2019
2,374
3,887
Hivi mtu mpaka anauliza hili swali huwa anawaza kitu gani haswa?? Yaani umekaa ukafikiria ukaja kuuliza swali ambalo majibu yake unayo

Mwanamke ana mengi ya kutoa kuliko hata wewe mwanaume… kwanza waulizaji wengi humu ni single( hawajaoa).. waliooa wanajua nini wanapata kwa wake zao zaidi ya papuchi…

Kuna mmoja huko kwenye nyuzi kasema kama wanawake wanawapa ushaurii basi hata mbuzi anaweza kutoa ushaurii… kwanini sasa usianzishe mahusiano na mbuzi akupe ushauri ukatafuta mwanamke

Hilo swali limekaa kimtego sana ni kama mnataka na nyie muanze kupewa matumizii muachiwe pesa ya mboga

Kwani ninyi wanaume mnakitu gani cha kuoffer zAidi ya pesaa???

Na Kama ni pesa wapo wanawake wanahonga wanaume sana tu, Je na hao mnataka wawape na kipi zaidi

Msichokijua ni kwamba asilimia 90 ndani ya Ndoa wanawake wanajihudumia wenyewe… wanaume wa siku hizi hawajui wajibu wao… wanaoa wanatelekeza wanawake

Yeye akiacha hela ya mboga ndio kamaliza…. Hajui mkewe anapaka mafuta gani chupi zake zimeishaa au hana nguo na mpaka aambiwe

Hivi unamuoa mtu unajua hana kazi ulitegemea avae kwa hela ganii au matumizi yake madogo madogo…

Hamjiulizi kwanini wanawake wengi siku hzi wanacheza mavikoba mpk kausha damu ili tu waweze kuhudumia familia zao

Kina Zamaradi wanakopa mpk ma benk ili kujihudumia

Sisi wanawake tuna vingi vya kuwaoffer kuliko ninyi wanaume

Hebu nipeni jibu


Wanaume mnanini cha kuoffer kwa mwanamke zaidi ya pesa???
 
Hivyo vichokoraa vinakuumiza kichwa?
Hao ni wale waliomaliza chuo ramani haisomi wanakua wana makasiriko na kila Mwanamke sababu wanawaonea wivu, kiufupi kwa jinsi walivyopigwa na maisha, wanatamani hata wangezaliwa Wanawake.... Hakuna Mwanaume rijali, aliyejitafuta akajipata akauliza maswali kama hayo....

Relax Mama, tafuta Mvinyo uuburudishe Moyo wako, it's a weekend
 
Hivyo vichokoraa vinakuumiza kichwa?
Hao ni wale waliomaliza chuo ramani haisomi wanakua wana makasiriko na kila Mwanamke sababu wanawaonea wivu, kiufupi kwa jinsi walivyopigwa na maisha, wanatamani hata wangezaliwa Wanawake.... Hakuna Mwanaume rijali, aliyejitafuta akajipata akauliza maswali kama hayo....

Relax Mama, tafuta Mvinyo uuburudishe Moyo wako, it's a weekend
Vichokoraa...??? Una mume kweli wewe?
 
kuna comment moja nimeona kwenye thread leo hapa kuwa
Mwanamke sio binadamu ni mfano tu wa mtu,,,kama kigezo kuzaa ata chura anazaa pia

Na Mimi ndio nimeuliza kama chura anazaa wawatie hao vyura wazae nao… usimfananishe mtu na viumbee vinginee

Ndio maana siku ya 6 Mungu aliitumia kwa kumfanya mtu kwa mfano wake
 
Ona huyu nae

Baada ya mungu ni mwanaume ndo anafata

Ebu fikiria hii dunia tu,bila mwanaume ingekuwaje,ugunduzi wote ni mwanaume

Ujenzi kuanzia mabarabara mpaka majengo ni mwanaume

Sasa ngoja nikujibu,unajua pesa ndo maisha

Pesa ndo ulinzi,pesa ndo kila kitu

Mbona hakuwaamini akaona hanuweZi peke yenu akamuumba mwanamke
 
Hivyo vichokoraa vinakuumiza kichwa?
Hao ni wale waliomaliza chuo ramani haisomi wanakua wana makasiriko na kila Mwanamke sababu wanawaonea wivu, kiufupi kwa jinsi walivyopigwa na maisha, wanatamani hata wangezaliwa Wanawake.... Hakuna Mwanaume rijali, aliyejitafuta akajipata akauliza maswali kama hayo....

Relax Mama, tafuta Mvinyo uuburudishe Moyo wako, it's a weekend

Wanakera sana wanazani kila mwanamke anahitaji pesa ya mwanaume ili aishi
 
Most times hua nikisoma comments humu naamini 95% ya watu wanaotoa controversial ideas, wao hawa practice what they say. Possibility n kubwa wengi wa "kataa ndoa" wameoa au wana wapenzi but wako na frustrations mob humo ndani ya mahusiano yao.

Iko wazi kuwa in this life, a woman is not all about sex. Wanawake wana mchango mwingi sana but shida n kwamba tunafanya quantification kwenye material things kama hela n.k.
Personaly sikubaliani na kukataa ndoa maana najua kbsa gap ambayo mwanamke wangu anacover kwenye life yangu.

Chimbuko la hili tatizo ni wanaume wengi kukosa msingi wa kiume kwaio wanakua kama wavulana. Hawajui majukumu yao n.k.

Kama mwanaume, kumhudumia mkeo na familia ni kitu cha ufahari na sio suala la kulia lia na kulalamika.
Its jus that un-matured boys, wanakutana na un-matured girls wanaishia kuleta maneno ya kudang dang kama kangaroo.

Swali kubwa la kujiuliza n kwamba, hao wanao support kukataa ndoa, mara kupiga na kuacha e.tc, wanapozaa watoto wa kike, what future do they expect watoto wao wapate?

NA wengi wao n vijana wadogo wa early 20s ambao bado hawajui maisha. Wengi wao ni KKB(KUla, kulala, kunya bure)
 
Hebu nipeni jibu

Wanaume mnanini cha kuoffer kwa mwanamke zaidi ya pesa???
Basi na wewe huna tofauti na hao wavulana unaolaumu hapa.
Kwamba kazi nyiiingi za pesa huzijui?!!
1694859371143.png
 
Na nyie mtujibu hapa mnatupa nini zaidi ya hela ambayo na ye nywe kwa sasa wanawake tumeshikiria msukani tunatafuta na zetu na tunawahongaa piaa
Unavyoandika tu inaonyesha hata kuwaelekeza watoto homework aeiou hutaweza.
 
Hii yote ni Matokeo ya kukosa elimu ya mahusiano. Na huu ni mwanzo tu, kwa hawa vijana wakike na wakiume waliozaliwa miaka ya hivi karibuni mambo yataharibika zaidi.

Kinachopaswa kufanyika ni vijana kupata elimu ya mahusiano wakiwa ngazi ya Secondary ili iwasaidie kujua mwenza sahihi ni yupi, kujua uhuru na mipaka kwenye mahusiano, kuhimili misukosuko ya mahusiano, kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi kwenye mahusiano na kuwa na mchango kwenye mahusiano.

Naimani hayo yakifanyika hatutakuwa tunaulizana maswali ya namna hii pia tutakuwa na ndoa zenye changamoto chache kuliko ilivyo sasa.
 
Back
Top Bottom