Ushauri wa Wabunge kwa JK kumtema Pinda: Nashauri kama Mwandosya amepona ateuliwe kuwa Waziri Mkuu

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Ushauri umetolewa Bungeni kwamba JK amtoe Pinda kwenye U-PM kwa sababu inaonekana Pinda ni kikwazo katika mambo mengi. Mie nashauri kwamba kama Prof. Mwandosya amepona, basi JK afikirie kwa makini sana juu ya kumteua Professor Mwandosya kuwa Waziri Mkuu mpya. Mwandosya anaonekana kuwa mtendaji makini sana, na anaheshimika ndani na nje ya CCM, na ndani na nje ya nchi. Kama afya yake sio tatizo basi katika kipindi hiki kilichobaki cha uongozi wa JK ingekuwa busara sana kwa JK kumteua Prof Mwandosya kama Waziri Mkuu.

Nyongeza: Tunahitaji PM mwenye sifa muhimu zifuatazo:

1. Mtu aliyethibitika kuwa mchapa kazi, makini (asiyekurupuka kuongea au kutenda) na mwenye uwezo wa kuelewa changamoto za utendaji wa serikali
2. Mtu anaeheshimika si tu ndani ya CCM, bali na nje pia kwa vyama vingine vya siasa, na ndani ya Bunge
3. Mtu ambae ana uwezo wa kuwakemea mawaziri na wakamheshimu anachosema, wakijua ni mtu serious na kazi
4. Mtu ambae kuteuliwa kwake kuwa PM kutasaidia sana kuziba nyufa ndani ya CCM za huko nyuma zilizotokana na kugombea uraisi, hasa katika pindi hii ya lala salama ya JK.
5. Mtu atakaetoa ushauri mzuri kwa JK katika mambo ya kila siku yanayohusu Baraza la Mawaziri na utendaji wake
6. Mtu atakaesaidia kurudisha hadhi na heshima ya cheo cha Waziri Mkuu katika macho ya wananchi kwa ujumla
 
Ushauri umetolewa Bungeni kwamba JK amtoe Pinda kwenye U-PM kwa sababu inaonekana Pinda ni kikwazo katika mambo mengi. Mie nashauri kwamba kama Prof. Mwandosya amepona, basi JK afikirie kwa makini sana juu ya kumteua Professor Mwandosya kuwa Waziri Mkuu mpya. Mwandosya anaonekana kuwa mtendaji makini sana, na anaheshimika ndani na nje ya CCM, na ndani na nje ya nchi. Kama afya yake sio tatizo basi katika kipindi hiki kilichobaki cha uongozi wa JK ingekuwa busara sana kwa JK kumteua Prof Mwandosya kama Waziri Mkuu.

Mie nakupinga kwa nguvu zoote. Amteue Mheshimiwa saana Prof. Juma Kapuya. Ni mtu adilifu na anaijua saana kazi yake na ni mchapa kazi mzuri akipewa nafasi. Tena atapata nafasi ya kujizoeza hiyo nafasi ili aimudu vizuri kipindi kijacho kwani ameahidiwa hiyo nafasi na EL. Tena ni Profesa na ni wa ile dini yetu na si mkanda huyo wala mkabila. Ni mawazo tuuu
 
Ha, ha, ha! Mkuu, naona umeamua kunogesha JF!
 
Amteue mulugo. Yuko komited na akili zao yani jk na mulugo zinalandana.
 
hawezi kumrudisha uwaziri mkuu lowasa maana hata leo kamruka kumpa mkono wakati akisalimia viongozi jukwaa kuu katika sherehe za uhuru
 
Ushauri umetolewa Bungeni kwamba JK amtoe Pinda kwenye U-PM kwa sababu inaonekana Pinda ni kikwazo katika mambo mengi. Mie nashauri kwamba kama Prof. Mwandosya amepona, basi JK afikirie kwa makini sana juu ya kumteua Professor Mwandosya kuwa Waziri Mkuu mpya. Mwandosya anaonekana kuwa mtendaji makini sana, na anaheshimika ndani na nje ya CCM, na ndani na nje ya nchi. Kama afya yake sio tatizo basi katika kipindi hiki kilichobaki cha uongozi wa JK ingekuwa busara sana kwa JK kumteua Prof Mwandosya kama Waziri Mkuu.

Ili ugange njaa au nini Mwandosya hana tena uwezo wa kufanya kazi. Wapo wachapakazi na niwazima.
 
Kuna vitu hata Mark akisikia unachosema atakuona mwehu kiaina japo nguo umepiga pasi. Anapaswa kupumzika wewe unasema uPM???
 
Hizo ni chuki binafsi ulizo nazo kwa Prof. Mwandosya, au mapenzi potofu uliyonayo kwa mtu unayetaka awe Waziri Mkuu. Kama ungekuwa makini ungegundua nimesema ikiwa Mwandosya amepona. Sasa wewe unasema hana uwezo wa kufanya kazi, kwa kigezo kipi ulichotumia kama sio kutupotezea muda wetu kwa ushabiki tu hapa usio na mbele wala nyuma? Watu kama wewe mnatupotezea sana wanachama wa JF wenye akili ya kujadili mambo, wanasoma upuuzi kama wako na kuamua JF hakufai kusoma chochote.
 
Tatizo baraza la mawaziri kuwa Baraza, litakuwa Mwabaraza la Mawaziri
 
Amteue mulugo. Yuko komited na akili zao yani jk na mulugo zinalandana.
Mie ningemshauri amuweke Mwigulu Nchemba. Amekifanyia mengi chama chake. Na kwa kuwa hana huruma basi mawaziri ambao watakuwa hawawezi kazi anaweza hata kuwamwagia tindikali ili washike adabu.
 
Kuna vitu hata Mark akisikia unachosema atakuona mwehu kiaina japo nguo umepiga pasi. Anapaswa kupumzika wewe unasema uPM???

Ungekuwa kweli umepewa cheo cha kuwa mwili na akili ya Mwandosya, angalau ungekuwa unaandika vitu vya maana humu ndani JF. Labda umepewa cheo cha kuwa kiungo kingine muhimu cha Mwandosya, lakini unfortunately pamoja na umuhimu wako kila utakachosema kitanuka tu.
 
Back
Top Bottom