Ushauri: Waziri Kalemani ateuliwe kuwa Naibu Waziri wa Nishati Ili kuboresha ufanisi katika wizara hiyo

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,125
22,616
Rejea thread niliyoanzisha ikisema,

Waziri wa Nishati anafanya nini kikaoni wakati Nchi Iko gizani?- Rabbon.

Hoja ya thread hapo juu ililenga kuuulizia ilipo nafasi ya waziri wa Nishati ambayo ni kama kivuli Cha nafasi ya Naibu waziri mkuu.

Naibu waziri mkuu Mh Biteko alimwagiza Ndugu Maharage kutohudhuria kikao Cha kujadili masuala ya Nishati Ili ajumuike na team yake kutatua tatizo la umeme, wakati ktk uhalisia, waziri wa Nishati alitakiwa pia kuondoka kikaoni kushughulikia tatizo.

HOJA yangu ililenga kuonyesha gap ambalo Kwa namna Fulani, Naibu waziri mkuu anashindwa kuliziba Kwa jinsi asivyoweza kujitenga na nafasi mbili alizopewa Kwa wakati mmoja.

Sishauri kuteuliwa mwingine Kwa nafasi ya Waziri wa Nishati kumtenga na nafasi ya Naibu waziri mkuu,

Nia yangu ni kushauri watu makini ambao wanaweza kushika nafasi ya Naibu waziri mkuu lakini hapo hapo Wana uwezo na uzoefu kuziba gap ikiwa Mh Biteko ametingwa Mahali.

Yaani anakuwa Naibu waziri Nishati, lakini hapohapo anakuwa waziri wa Nishati kivuli muda ambao Naibu waziri mkuu ametingwa.

Ushauri huu ni Kwa Maslahi mapana ya nchi, na ni ushauri wa dharura kuokoa jahazi kuzama Hasa katika kipindi hiki kigumu Nchi ikiwa gizani.

Karibuni🙏.

Amen
 
Concurrent activities, inahitaji vichwa vyenye uwezo mkubwa, watu wachache sana wenye uwezo huo.
Ukiona mtu hata akifungua mlango anatafuna ulimi au anauma meno hawezi kua na akili ya kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja. Ukiona mtu hata akiwa anaongea kama kashika vitu anaweka chini ndio aongee na kurushalusha mikono ujue hiko kichwa ni chepesi, hakiwezi kufanya vitu viwili au zaidi kwa wakat mmoja.
 
Pendekeza nini kifanyike ndugu Mlimilwa,

Mimi niliona gap Hilo kiutendaji nikashauri.
 
Kalemani aliachia ngazi kwa sababu moja tu

Kipindi chake chote ilikuwa mtu akitaka kuunganishiwa umeme ni 27,000 kijijini na ama mijini

Alipoitwa na mkulu kuambia anapaswa akubaliane na sera mpya ya kupandishwa kwa gharama hizo hadi 310,000/ na arudi kwa wana habari kuelezea hilo,

Nafsi ilimsuta akaona isiwe tabu, maana wananchi hawatamwelewa na atapata tabu sana kisiasa mbeleni

Sasa; sielewi iwapo atakubali akiombwa!
 
Kalemani aliachia ngazi kwa sababu moja tu

Kipindi chake chote ilikuwa mtu akitaka kuunganishiwa umeme ni 27,000 kijijini na ama mijini

Alipoitwa na mkulu kuambia anapaswa akubaliane ba mpango wa kupandishwa kwa gharama hizo hadi 310,000/ na arudi kwa wana habari kuelezea hilo,

Nafsi ilimsuta akaona isiwe tabu, maana wananchi hawatamwelewa na atapata tabu sana mbeleni

Sasa; sielewi iwapo atakubali akiombwa!
Akiombwa na wananchi atakubali,

Thread hii ni kumuombea aridhie ikiwa atapewa nafasi hiyo.
 
Kalemani aliachia ngazi kwa sababu moja tu

Kipindi chake chote ilikuwa mtu akitaka kuunganishiwa umeme ni 27,000 kijijini na ama mijini

Alipoitwa na mkulu kuambia anapaswa akubaliane na sera mpya ya kupandishwa kwa gharama hizo hadi 310,000/ na arudi kwa wana habari kuelezea hilo,

Nafsi ilimsuta akaona isiwe tabu, maana wananchi hawatamwelewa na atapata tabu sana kisiasa mbeleni

Sasa; sielewi iwapo atakubali akiombwa!
Sukuma gang mwisho sasa hatuwataki
 
Pendekeza nini kifanyike ndugu Mlimilwa,

Mimi niliona gap Hilo kiutendaji nikashauri.
Mm niliwahi kuchangia hapa. Kipindi kile jiwe anataka kupanga safu ya mawaziri.kwamba..wizara ya nishati na madini zitenganishwe.kutokana na unyeti wa kazi zake.lakini shida nchi yetu kuna vitu wanavichukulia poa sana wakati vitu hivyo ni muhimu na ndio nguzo kuu ya uchumi wetu. Sasa mtu unampa kazi zote muhimu hili ni tatizo.lazima watafute mtu wa umeme tu. Mifumo yetu ya umeme imepitwa na wakati..hata wafanyeje kama wataendelea kukaza shisho hawawezi kumaliza tatizo la umeme.
 
Back
Top Bottom