Ushauri wa bure kwa Rais Kikwete, muombe msamaha Lowassa kabla ya October 25!

Hii ni moja bandiko mbovu kabisa humu iliyoandikwa na huyu nguli wa humu kwasababu ya ujinga tu na ushabiki wa kipuuzi tu.

Anayeamua nani awe kiongozi aka rais wa nchi si JK, kilichotokea kwa habari ya wawili hawa si kigeni kutokea kwenye maisha haya.

Kwa utaratibu waliojiwekea CCM mwaka ule wa 1995 ilikuwa ni zamu ya Rais kutoka upande wa pili wa jamhuri na most likely Salim Ahmed Salim alikuwa ndiye mtu sahihi kwa nafasi ile then, lkn tuliona jinsi mtandao kwa affluence yao walivyo'influence matokeo, huku wakimdhalilisha sana Salim wakiongozwa na Lowassa huyuhuyu, kilichotokea baina ya JK na Edo kwa mujibu wa karma ni what goes around comes around au kwa kindengereko chetu ni apandacho mtu ndicho atakachovuna.

Hivyo basi JK hana cha kuomba msamaha kwa EL.

Tatizo lako huo upuuzi wako unaouita karma ni kujidanganya kwasababu umeamini EL atakuwa Rais baada ya Tar. 25 Oktoba 2015, huu ni upuuzi ambao kwa bahati nzuri tu umeonyesha makengeza ya kimtazamo. Pole na maisha.
 
alibanwa mbele na myuma, kulia na kushoto... ilikua si mchezo

And i definitely agree with you about JPM, ni mtu wa visasi na vinyongo visivyokwisha

Mshindi halali alikuwa yule mama mzanzibari kwa hisani ya kura za wafuasi wa Lowassa.
Lakini kwa sababu zao binafsi waliamua kuelekeza ushindi kwa Dr. Magufuli..

Dr. Magufuli hakujiandaa. Unaweza kuthibitisha hili kwenye mwenendo wa kampeni zake...!!
Kibaya zaidi ni kuwa haaminiki na pengine anaogopwa na wengi ndani ya ccm na miongoni mwa makundi ya wananchi...!!
 
Mimi alichonishangaza JK ni kumteua Magufuli

both Magufuli na Lowasa wana vinyongo nae
yeyote atakaeshinda still anaweza lipa 'visasi' kwake

so nimemshangaa JK......halioni hilo?

The Boss, kwani si upo Tanzania mkuu? Hukumbuki kilichojiri kule Dodoma? Magufuli hakuwa kipaumbele kamwe! Magufuli ni zao la mnyukano wa kambi mbili, nazo ni Team Lowassa na Team Membe. Lilipoenguliwa jina la Lowassa Team Lowassa waliapa kutoruhusu Membe kuwepo. Kumbuka team Membe ilikuwa ikiungwa mkono na uongoz wa juu wa CCM huku Team Lowassa ikiungwa mkono na Wajumbe wengi. Sasa ilionekana kuwa baada ya Team Lowassa Kujiapiza kuwa ni afadhali CCM ife kuliko kumuunga mkono Lowassa hapo Mwenyekiti ikabidi aombe ushauri. Hivyo mzee Mkapa akamshauri amchukue Magufuli. Hivyo Magufuli ni ushauri uliotolewa na mzee Mkapa, na kiukweli imesaidia kidogo. Yaani mwenyekiti angethubutu kumuacha Membe CCM ilikuwa inasambaratika! Mkapa ni jembe tuseme tu ukweli, angalau amesaidia CCM ipo japo ina makundi lakini yamepungua kidogo!
 
If JK and Lowassa are playing a game with us and are still best buddies behind the curtains ntaamini JK is very very smart and ntampa my ultmost respect.

Mkuu hilo swala nilishalifikiria siku nyingi sana.
Kwa mawazo yangu binafsi na nilishacoment humu jamvini ni kua ilimuwia vigumu sana JK kumtengenezea njia EL ndani ya CCM kutokana na migawanyiko iliyoko ndani yake na makundi mengi hivyo basi JK akaona njia rahisi ni EL kahamia Upinzani.

Na dhihaka anazofanyiwa sasa EL na wapiga domo wa CCM kila mtu anaamini JK ashamtosa EL.

Kinachonishangaza zaidi EL anajiamini kwa kitu gani hadi kahamia Upinzani? Ili hali anajua kabisa Demokrasia ya Nchi hii haipo fair kwa Vyama vya Upinzani na hakuna Tume huru ya Uchaguzi?

Kihalali kabisa chaguzi zote zilizopita zingekua huru na za haki Nchi hii ingekua ishatawaliwa na Chama cha Upinzani au Bunge lisingekua la upande mmoja kama lilivyokua kwani asilimia kubwa ya Wabunge wa upinzani walifanyiwa zengwe sana na hata hao walioingia Bungeni ni kwa sababu ya nguvu ya Umma.

Rejea chaguzi zote zilizopita za Visiwani Z'bar CCM hua haishindi Kihalali na hapo Tume ni yao lakini angalia tofauti ya asilimia za Ushindi wao.
 
Mimi alichonishangaza JK ni kumteua Magufuli

both Magufuli na Lowasa wana vinyongo nae
yeyote atakaeshinda still anaweza lipa 'visasi' kwake

so nimemshangaa JK......halioni hilo?

JK alizidiwa hadi akasahau jina la mchezo, na hapo ndipo Magufuli alipopenya!
 
tanzania na africa zitaendelea kua masikini kwa miaka mingi sana ijayo kutokana na ujinga na umbumbumbu wa watu wake. yaani watu wanakubaliana kuachiana uraisi kama vile wanarithishana mali ya familia na bado kuna watu mnaona ni vema, na hata baada ya mmoja wao kuvunja makubaliano hayo ya kipumbavu kuna watu mnaona ana haja ya kuomba msamaha...... dah inawezekana kweli africa imelaaniwa.
 
Pasco

Kuna uzi niliwahi kuleta hapa kukuomba unifunulie ki fikra mods wakafuta, tena walifuta baada ya wewe kuitikia wito na kusema Naam umesikia wito na utakuja! Niliumia sana, hata leo bado naumia sana.

Nilipomaliza kusoma huu uzi, nilitokwa machozi mengi sana. Kuna mengi nimekumbuka sana!
 
Last edited by a moderator:
bavicha kwa kujidanganya hawajambo,,,tuseme tu lowasa kashinda hivi atamfanya nini jk?,kwasababu huwezi kuwa rais halafu ukaondoka bila kuweka system ambayo kama kuna dalili mbaya itakulinda au ikibidi kumpiga chini huyo anaingia...
hata hivyo bifu la jk na lowasa linakuzwa na bavicha,usikute hawa jamaa walipanga move yote,,,,unamuona jk anahangaika na kampeni?,,,,na yale maneno yake kuwa ccm lazima wajiandae kwa lolote je?,alijua kuwa lowasa ataenda upinzani ama aliinitiate lowasa kwenda upinzani baada ya kujua kuwa lowasa kupitia ccm haitawezekana?..

hata hivyo lowasa uwezekano wa kupita ni mdogo sana japo upo
 
tanzania na africa zitaendelea kua masikini kwa miaka mingi sana ijayo kutokana na ujinga na umbumbumbu wa watu wake. yaani watu wanakubaliana kuachiana uraisi kama vile wanarithishana mali ya familia na bado kuna watu mnaona ni vema, na hata baada ya mmoja wao kuvunja makubaliano hayo ya kipumbavu kuna watu mnaona ana haja ya kuomba msamaha...... dah inawezekana kweli africa imelaaniwa.

kama kuna bifu lowasa ndp anapaswa kujilauimu na si jk,,,,,hadi lowasa anajiudhulu jk bado alimtetea kuwa kapata ajali ya kisiasa,na pia 2010 alimnadi katika uchaguzi mkuu na kumwagia sifa tele ili achaguliwe kuwa mbunge wa monduli,mpaka hapo hakuna dalili za bifu...
2012 katika uchaguzi mkuu wa ccm,lowasa akataka kumpindua jk kutoka katika umwenyekiti wa ccm,hapo nadhani ndo ishu imeanzia,,,,,,,,mpaka hapo mwenye kosa ni lowasa,,,,,,,lowasa angetulia na kufanya siasa za kiistaraabu si ajabu sasa angekua mgombea wa ccm,lakini alianza faulo mapema mno,bad timing.
 
Hii ni moja bandiko mbovu kabisa humu iliyoandikwa na huyu nguli wa humu kwasababu ya ujinga tu na ushabiki wa kipuuzi tu.
Anayeamua nani awe kiongozi aka rais wa nchi si JK, kilichotokea kwa habari ya wawili hawa si kigeni kutokea kwenye maisha haya. Kwa utaratibu waliojiwekea CCM mwaka ule wa 1995 ilikuwa ni zamu ya Rais kutoka upande wa pili wa jamhuri na most likely Salim Ahmed Salim alikuwa ndiye mtu sahihi kwa nafasi ile then, lkn tuliona jinsi mtandao kwa affluence yao za


zamani nilipokuwa mdogo nilikuwa nikiwaona watangazaji kama akina paskal mayala,etc kuwa labda ni very exceptional,na wana upeo mkubwa,kumbe wapi bana,,,,,,
 
Wapo watu wanaamini kabisa Lowassa atashinda?

Kwa sasa picha iko dhahiri,haina mikwaruzo atashinda!! Muhimu ni ccm kujiandaa na kukubali kukataliwa na watanzania maana ni matokeo ya yale waliyokuwa wakiyapanda..attempts kung'ang'ania madaraka na ku twist matokeo ya uchaguzi inaweza kuliingiza taifa katika machafuko..ccm imefikiri kuwa iko juu ya watanzania miaka yote.ukweli ni hii nchi ni ya watanzania na kufikiri kwamba hata watu waamue kiasi gani ccm haiwezi toka ni kujidanganya sana...
 
Pasco Andishi lako linaukakasi Ndani Yake kwa kuwa umeonyesha ww ni wa upande upi... Kumshauri Jk Akamuombe Msamaha Edo ni Kuonyesha ni Jinsi Gani Unafikra fupi katika Siasa Za Tanzania. Tanzania Haina mkataba kwa Marafiki Kuachiana Nafasi Ya Urais kwa Kuwa Urais ni Taasisi Nyeti Ambayo Haiwezi Kuachiwa kwa Watu Kupeana Zamu. Kama Umetumia Maneno Ya Mwapachu Kumhukumu Jk Unaonyesha ni Jinsi Gani Umejawa na Mapenzi Kwa Edo. Tanzania Ni nchi Ya Wote Sio Ya Jk wala Edo, Kumtetea Edo na Kumshusha Jk Ili Akamuombe Edo msamaha kwasababu Ya Maneno Ya Mwapachu Nikuonyesha Wazi Kuwa Taaluma Yako Ya Uandishi Huitendei Haki Pasco.

KUAMINI JK NA EDO WANAUGOMVI NI KUJITOA UFAHAMU LAKINI MIMI NAAMINI HUU NI MCHEZO NA MUDA UKIFIKA TUTAUJUA TU. time will tell
 
Wapo watu wanaamini kabisa Lowassa atashinda?

Hatashinda kutokana na kauli ya Mheshimiwa A.F.MBOWE kua hawaendi kulipiza kisasa/visasi bali kuna wengine lazima washughulikiwe kwa kusababishia hasara nchi? au hatashinda kwa sababu ya watu kutomchagua? au hatashinda kwa sababu CCM hawatashindwa milele? au hatashinda kwa sababu hutaki hashinde? naomba msaada MM
 
Mkuu,
Mbona inasemekana Pombe hakua chaguo la Jk!! Pale siku ya uchaguzi ndani ya kamati kuu yalifanyika mapinduzi na kupelekea wajumbe kumchagua Pombe, baada ya kuona Kipenzi chao Lowasa amekatwa. Na kwa taarifa zisizo rasmi, inasemekana kwamba chaguo la Jk lilikua ni Membe.
mkuu hizo zote zilikuwa sarakasi fungua link ya kwanza aliyoiweka pasco ni ya August 2014 hata michakato haijaanza ila pasco alikuwa amepewa tetesi na mtu anayemwamini kuwa ni kada wa ccm kwamba inawezekana Magufuli akawa mgombea urais kwa tiketi ya CCM. hayo yalisemwa mwaka mmoja kabla na yanatokea vile vile kwa maana ya kwamba huu mpango wa kumteua magufuli haukuwa wa kubahatisha kabisa
 
Sio kuwa Jk alimteua Magufuri jamaa Magufuri ilitokea kama Zari la Mental@The Boss
mkuu link ya kwanza ni ya August 2014 mwaka mmoja before kuanza harakati za uchaguzi ule uzi pasco alidai Magufuli could be presidential candidate for CCM in 2015. aliambiwa na mtu mkubwa tu ndani ya CCM. mwaka mmoja baadaye kweli Magufuli anateuliwa hivi unafikiri ni bahati mbaya hiyo? hivi vitu vimepangwa kwa ustadi mkubwa na vimetimia. nilichogundua hatusomi. jaribu kufungua link moja baada ya nyengine kuna link imeonyesha namna ambavyo ccm itaweka vigezo vya kuchagua wagombea wa urais again inatokea vivyo hivyo. hivi vitu havifanywi kwa bahati mbaya hata kidogo
 
Back
Top Bottom