"Jamani naitaji msaada mkubwa sana, wa mawazo na saikolojia. Mimi nina mke nimezaa nae. Tangu tufunge ndoa ni miaka 4 sasa.yeye yuko Mkoani mimi niko chuoni Dar es Salaam kimasomo elimu ya juu". By Kipusy
Maneno ya utangulizi wa thread ya ndugu yetu Kipusy kwa yaliyomkuta. Ndoa yangu ina miaka 4 na mtoto 1 na Wife yupo Dar kikazi wakati mimi nipo Mkoani kikazi pia. Tatizo tunalojaribu kukabiliana nalo ni kukwepa majaribu yanayotokana na umbali kati yetu. Hata hivyo kwa nature ya kazi zetu ni mimi tu mwenye uwezekano wa kuhamia Dar kwani mwajiri wa mwenzangu hana ofisi huku mkoani.
Nimejaribu kumshawishi mwajiri wangu anirudishe karibu na familia lakini dalili za kufanikiwa hivi karibuni hazionekani, labda baada ya miaka mitatu hivi. Kwa upande wangu nimechoshwa mno, mno na maisha haya ya kuwa Modified bachelor hasa ukizingatia matatizo ya ndoa za siku hizi.
Naomba ushauri wenu nifanye nini kati ya haya yafuatayo?
1 Kuomba uhamisho ambao nimeshaona mafanikio yapo mbali sana kwa sasa?
2.Kuomba kuhamia kwa mwajiri mwingine mwenye nafasi?. Hili nalo litakuwa gumu zaidi kwani sio rahisi kupitishwa kwa barua yangu ya uhamisho.
3.Nitautafute kazi nyingine serikalini (niliko) au taasisi binafsi ili nisogee jirani na familia au
4.Niendelee kulinda kibarua huku nikihatarisha ndoa yangu hasa ukizingatia tangu siku ya harusi hatujafanikiwa kuishi miezi zaidi ya 6 pamoja huku kila mwezi tukipoteza nauli kusafiri safiri?
Najua humu jamvini kuna watu wenye uzoefu mbalimbali hivyo natarajia nitapata ushauri utakaoniwezesha kufanya maamuzi.
Nawasilisha