Ushauri: Rais Samia itisha kura ya maoni kupitia akaunti yako ya X kuhusu suala la Bandari, utapata picha halisi na ikusaidie kufanya maamuzi

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,018
144,377
Rais Samia kama unavyopenda kutumia mtandao wa X kuelezea mambo yanayohusu nchi na Watanzania ikiwemo kutoa taarifa mbalimbali za Serikali yako, nakushauri utumie mtandao huo kupata maoni ya wananchi ni namna gani wameupokea mkataba wa Bandari ambao umekuwa gumzo kuu hapa nchini.

Rais Samia ,mijadala mingi inaibuka na kupita, ila huu wa Bandari ni wazi umekuwa na utakuwa endelevu, hivyo fanya jambo la tofauti ,na hili si lingine bali kuitisha kura ya maoni isiyo rasimi kupitia mitandao na hapa napendekeza utumie mtandao wa twitter au ukiweza kupitia hapa JamiiForums vile vile.

Au ikiwezekana, jukumu hilo wape wasaidizi wako kama vile Msemaji wa Serikali ambae nae ana akaunti X

Swali la msingi liwe ni je, unaunnga mkono mkataba huu wa uwekezaji kwenye bandari zetu?

Majibu yawe ni ya kuchagua kati ya haya yafuatayo:

1. NDIO
2.HAPANA
3.SIJUI

Hilo swali mnaweza kuliuiza kwa kuliandika mnavyoona inafaa, ila ujumbe uwe ni huo huo.

Mhe. Rais, nukuu hii hapa chini ya Baba wa Taifa ikuongoze.

Julius Nyerere: Hatuwezi kutatua matatizo yetu kwa kujidanganya kuwa hayapo.
 
Unadhani haijui hali halisi au ameamua kukaa kimya kama alivyo sema?

Anaju watanganyika hawataki hilo swala na TEC walisaidia kuongeza sauti
Anaweza kutafuta maoni ya wananchi kwa namna yoyote halafu akapata pa kutokea ikiwa kwa sasa anashindwa kuusitisha.
 
Unadhani huko tweeter hapitii na kuona yanayoendelea huko?

Anajua sana lkn kwa sababu ni mkubwa basi uamuzi wake hakuna wa kuusimamisha.
 
Anaweza kutafuta maoni ya wananchi kwa namna yoyote halafu akapata pa kutokea ikiwa kwa sasa anashindwa kuusitisha.
Pengine sababu zinazofanya ashindwe au aone aibu kusitisha zipo nyuma ya pazia ama huwenda zipo nje uwezo wake au akisitisha yaliyonyuma ya pazia yatawelwa wazi na yatamfedhehesha sana na kulitia aibu taifa
 
Pengine sababu zinazofanya ashindwe au aone aibu kusitisha zipo nyuma ya pazia ama huwenda zipo nje uwezo wake au akisitisha yaliyonyuma ya pazia yatawelwa wazi na yatamfedhehesha sana na kulitia aibu taifa
Kina Musukuma hawawezi kukubali mradi usitishwe maana wakifikiria yale ma v8
 
Lkn huko Twitter na mitandao mingine ya kijamii kuna wengine hawana akili timamu, vp kama wakipiga kura kwenye ndivyo sivyo.?
 
1.ndio 4.7%
2.hapana 78.1%
3.sijui 17.9%
Ni wazi huko serikali wanajua kabisa hili jambo halikubaliki, tatizo wameshakosea sasa wanafanyaje kurekebisha? Maoni ya watu yanaweza kuwasiadia kuyatumia kama mbinu ya kubadili maamuzi na kuficha/kupunguza aibu.
 
Mhe. Raisi ,mijadala mingi inaibuka na kupita, ila huu wa Bandari ni wazi umekuwa na utakuwa endelevu hivyo fanya jambo la tofauti ,na hili si lingine bali kuitisha kura ya maoni isiyo rasimi kupitia mitandao na hapa napendekeza utumie mtandao wa twitter au ukiweza kupitia hapa JamiiForums vile vile.
Wanaomuingiza chaka huyu mama ni KKKT na Zito Kabwe wao
 
Umesemaje eti?
 

Attachments

  • IMG_20230823_174243.jpg
    IMG_20230823_174243.jpg
    58.9 KB · Views: 2
Au afuatilie mikutano ya CHADEMA Nchi nzima,

Wanapiga kura ya WAZI, Kwa wanaopinga na wanaokubali mkataba wa DP World.

Hadi sasa, hajatokea hata mmoja mwenye kuukubali mkataba Ule fake na BATILI.

Wote wanasema HAPANA waziwazi akiwemo Kishimba PM.
 
Back
Top Bottom