Ushauri: Mke wangu anatembea na mfanyakazi mwenzie hadi kamzalisha

Kunywa sumu tu,mwanaume gani unashindwa kudeal na mkeo aliyepewa huko mtaa.
Kunywa sumu tupunguze wapuuzi kidogo.
 
Ai
Mpaka nimeamua kukuandika sijui nifanye nini, mimi ni kijana wa miaka 33 nimeoa na nina mtoto mmoja na sasa hivi mke wangu amekwenda nyumbani kwetu kujifungua na hii ndio sababu ya mimi kuja kukuandikia.

Iko hivi, mimi na mke wangu tulikuwa vizuri sana katika ndoa yetu, ni mwanamke ambaye niliona ananiheshimu na kujali kweli kila mtu anampenda. Hatujawahi kugombana lakini wiki mbili zilizopita alikwenda kujifungua nyumbani kwetu, mimi ndiyo nilimpeleka lakini kurudi nyumbani katika kuhangaika kufanya usafi ndiyo nikakuta kuwa kuna laini ya simu ambayo ilikuwa kama imedondoka.

Nilipanga kuitupa ila nikaamua kuiweka kwenye simu kuangalia. Sikukuta kitu cha maana hivyo nikaamua kuitoa ila kabla ya kuitoa kuna SMS Mbili ziliingia ni kama zile zinasubiri uwashe simu ndiyo ziingie.

Ni meseji za mwanaume ambaye alikuwa akilaumu mke wangu kwa kwenda kwetu kujifungua. Kuna SMS moja ndiyo uliniumiza zaidi, uliandikwa “Mtoto wa kwanza nilihudumia mimba unajifungua mtoto kafanana na huyo mwanaume wako! Huyu wa pili nimekuambia anataka niwe karibu na wewe umeenda kujifungulia kwenu?

Nataka ujue kwamba huyo mtoto kama ni wangu ukirudi namchukua sitaki mwanangu kuishi na huyo Boya!”

Niliiangalia ile namba nikaja kugundua kwamba ni namba ya mfanyakazi mwenzake, nikafuatilia mtandaoni nikajua ni mtu ambaye namfahamu hata kwenye harusi yetu alikuja huyo kaka na wafanyakazi wenzake tena kama familia yake hata ile kutafuta hoteli kwa ajili ya wageni nilitafuta mimi na huyo ni mmoja wao wale ambao alitoa list ya watu wake watakaokuja siku ya harusi.

Sikujibu chochote hizi meseji na mpaka sasa hivi hakijatumwa chochote, nahisi labda mke wangu kamwambia kuwa hiyo laini kashapoteza sijui, ila ninachowaza sasa hivi nifanye nini? Nimekaa na hiki kitu wiki mbili mwenyewe nahisi kuchanganyikiwa kweli najiona kabsai nafanya vitu ambavyo sivyo naomba ushauri nifanye nini?
Duuuh...aisee kuna vitu vinaumiza sana.

Ila mwamba mimi nisingevumilia, ningeamsha mda huo huo namfata home namchukua aende tu kwa msela huyo akajifungulie huko huko.

Nabaki na mwanangu wa kwanza na naoa mwingine chapu ili kupooza maumivu.

Wanawake hawaachanagi na ma X wao piga ua hata akiolewa ataendelea kumtunuku tu.

Pole sana brother, ili chukua hatua mapema, usiache lipite hivi hivi.
 
Mwache ajifungue kwanza, akirudi muulize na uombe kupima DNA za hao watoto....ikibainika si wako, tupilia mbali huyo mwanamke......hakufai
 
Wewe jamaa muongo muongo wewe kila siku tu ni wewe sini useme hizi story unatunga ...
 
Nawaonea huruma wanaojitahidi kuonesha juhudi za kushauri na kujali kwenye nyuzi za bwana huyu......maana huyu ni mtunzi mzuri wa hadithi hapa jukwaani........

Jambo pekee ambalo kujisingizia au kusema lilimtokea labda ni kulawitiwa lakini yote yashamtokea........

Inaonekana ni mtu mwenye msongo wa mawazo na hana kazi ya kufanya.......
 
Duuuh kumbe ndoa ndo zipo hivi!!!

Back
Top Bottom