KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,590
- 4,603
Kwa kuwa Waziri wa Nishati umepewa na jukumu la kuratibu shughuli za serikali ukiwa kama Naibu Waziri mkuu, ninaamini jukumu hilo limekuja kipindi sahihi na linaweza kukusaidia katika majukumu yako kama Waziri wa nishati hususani kipindi hiki cha uhaba wa mafuta.
Kwanza ninakushauri, katika dharula hii ya uhaba wa mafuta uanze na kuratibu matumizi ya magari ya Serikali kwa viongozi ambayo mengi yanatumia mafuta mengi. Katika kipindi hiki cha mpito viongozi watumie usafiri wa Umma.
Pili, misafara mikubwa ya viongozi pia iratibiwe. Katika kipindi hiki cha mpito cha uhaba wa mafuta tumia madaraka yako kuratibu matumizi ya mafuta yanayotumika katika misafara.
Tatu, ili kubaini uhalisia wa mafuta yaliyopo tafuta Teknolojia ya kubaini kiwango ambacho kimeingizwa na kilichobaki kutoka hapo wizarani. Hiyo itakuwa rahisi kuwabaini wanaoficha mafuta.
Nne, matumizi ya magari binafsi pia yadhibitiwe na kuratibiwa kipindi hiki. Utaratibu maalumu uwekwe ili wenye usafiri binafsi watumie usafiri wa Umma.