Freightliner
JF-Expert Member
- Aug 22, 2013
- 720
- 522
..je kubadili course hapo udom inawezekana ama!
Plz waelewa mnijibu
Plz waelewa mnijibu
Ndugu yangu first year karibu sana UDOM, ikiwa kuna jambo unataka kulijua la UDOM kwenye college ya humanities and social science niulize nitakusaidia kwa kukujibu na kukupa ufafanuzi.KARIBU SANA UDOM
..........
Nikuulize Wewe ukiwa kama na ni?????
hivi ni kwel udom chuo cha kata?
me cwez kumuuliza mlinzi wa chuo me namuulza vice chancellar kwan we nan kwanza ? na nan kakupa haya majukumu?
Hivyo ni suti za kutosha???
Jamani wanaChuo wote wa Mji wa Dodoma Stand imehamishwa Nzuguni NaneNane kilometa 12 kabla hujaingia mjini km una mabegi jiandae na 20,000/ Taxi mpaka UDOM au.Chuo cha Mipango
Km ukitokea njia ya Singida shukia mjini ni nafuu zaidi usiende stand. Mpya njia ya Dsm
MAKOLE na wenzako, please admit that this must be a stupid University!
After all those years; 1 or 2 kindergarten, 7 primary level, 4 secondary level, 2 A-level/certificate level (followed by two years diploma level), making a total of not< 16 years of schooling, do we still need to be told how to dress? Is UDOM different from UD, SUA, MUHAS, etc.?
This makes a big problem, no where in this world people get cultured by rules or guidelines. School life should have changed their mind to reject half-up trousers, half-down skirts, smelling mouths, jigger infested legs, keratinised legs, etc. Which breed of leadership exists at UDOM? Is the leadership in tune with its position?
Nimesikia mengi kuhusu UDOM na nawaona vijana munaongozwa na mijitu isiyofaa kuwa hapo ilipo. Mingine tunaisikia inasifika kwa wizi, mingine kwa ushirikina, nk. Yaweza kuwa sababu hata vijana hawajui waendeje. Yaani hata University munawekewa mwalimu wa nidhamu? yaani munafundishwa adabu?
Muhimu ni kufuata sheria siyo kufundishwa adabu chuo kikuu. Mazingira ya chuo na wenzako ni mwongozo safi kabisa! Yaani tena eti munataja askari wa JKT. halafu munasifu?!!
Kwa utaratibu kama huo labda baadaye tutahitaji mkuu wa nidhamu na mienendo ya wabunge na hata Rais ili kukomesha suti za ki-paaa! na suti zinazobana mapaja ya Rais. Nonsense!!!!!!!!!
It seems that UDOM needs to be reconfigured/reformatted.
Sasa ndio umeongea nini?eti great thinker
Sorry jamaa zangu Stand imesharudi Mjini TAFADHALINI SHUKENI STAND YA MKOA ni mjini kabisa hapo utapata usafiri wa kufika UDOMnikitokea dar nishukie wapi mkuu?
Hongereni kwa kuchaguliwa "The White University" Nawashauri hivi:-
1. Yapo makampuni ya mabasi yatawataka mlipe pesa benki ili yawasafirishe hadi UDOM- Kataa kwani watakupiga hela halafu safari utaiona chungu. Hata wakijifanya wameingia mkataba na chuo, usiingie mkenge. Chukua basi kwa kujitegemea wewe mwenyewe.
2. Stendi ya daladala zote ndani ya Dodoma huanzia safari zake stendi ndogo ya daladala-Jamatini. Kuwa makini na eneo hilo kwani waleti na simu za mkononi hapo zinasakwa kwa udi na uvumba.
3. Uwe na uhakika wa College unayokwenda. Kwa kifupi, ziko daladala zinazokwenda Education, jina jingine wanapaita Ng'ong'ona ama Ng'ox. Wale waliochaguliwa college of Education, Medicine, Informatics na natural Science upande daladala hizo, vinginevyo utapata tabu kubwa.
4. Wewe unaekwenda College of social science pamoja na humanities panda daladala inayokwenda Social au Bondeni.
Kinyume na hapo utajiju.
5. Nauli kwa daladala ni Tsh 350 kwa safari yoyote ndani ya College, Kutoka Jamatini hadi Chuo ni 350 pia. Wahuni wanapiga hadi 1500/- kwani wanajua kuwa ni wageni hamjui kitu.
6. Tax inategemea maelewano, standard bei ni elf 8-10. epuka kupanda tax kwani utazungushwa mjini mitaa karibu yote na watakwambia bei kubwa, hata hivyo, kama huna uhakika wa college yako pia wanaweza kukuingiza ndani ya chuo wakakuzungusha college zote, watakuchanganya na majengo then watakupiga hela ndefu.
7. (kwa wanaokwenda social science) Chagua mavazi ya heshima kwani ukidhani unakwenda kujiachia unaweza ukajikuta unarudi nyumbani siku hiyo hiyo, Kwa wanadada, vimini, suruali za kubana, nguo za ajabu ajabu waachie wadogo zako. Kama huna za kushonesha anza kuzitafuta. Kwa wanakaka, punguza idadi ya majinzi (Hasa kwa wanaokwenda social science), mitindo ya kata K, kusuka nywele, kuvaa heleni potezea kwenu.
8. Kama mnasafiri kwa kampani, kuweni makini na College mnazokwenda, ikitokea kwamba mmefika Dodoma na si wenyeji hivyo kwenda chuoni moja kwa moja, na ikiwa College zenu ni tofauti mtalazimika kutengana hapo ili kila mmoja apande gari ya college inayomhusu ili kuepusha usumbufu,
9. Wenyeji wenu (mwaka 2na 3) hawapo na mtakuwa wageni watupu eneo hilo, Usimwamini mtu yeyote pahala popote pale ndani na nje ya College.
Huu ni ushauri wangu kwa uzoefu mdogo nilioupata pindi nilipokuwa huko Idodomiya. Kila la Kheri!