Ushauri kwa Serikali na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu

musase

Member
Jan 7, 2022
31
25
Katika hali isiyo ya kawaida tumekuwa tunakaa na watoto wetu nyumbani ambao wanasifa ya kujiunga chuo kikuu au ameisha chaguliwa kujiunga chuo kikuu tayari lakini hajawa na uhakika wa kupata mkopo utakaomuwezesha kujiunga kutoka bodi ya mkopo kwa wasiwasi mkubwa sana kwa sababu zifuatazo.

1) Mtoto anaishi na mzazi nyumbani bila kufanya maandalizi yoyote ya mtoto kwa kuwa hajawa na uhakika wa mkopo.

2) Inamsababishia mtoto kutojiamini na maombi aliyofanya ya mkopo.

3) Mtoto na mzazi wake wote wanakuwa watu wa kuuliza kila siku bila kujenga msingi wa kujiamini.

4) Hali hii imejengea familia nyingi zenye watoto wenye sifa kuwa na hali ya masikitiko makubwa wakati wa kusbiri kuona mkopo kama mtoto amepata.

5) Hali hii imefanya watoto wengi kusubiria mkopo wakati vyuo tayari vimefunguliwa na baadhi yao wakiwa wanaendelea na masomo.

USHAURi
1) Kwa kuwa bodi ya mkopo ni chombo cha umma kiwe kinaweka wazi majina ya wanafunzi ambao watapata mkopo na asilimia ngapi atapewa kwenye magazeti kuondoa sintofahamu hiyo.

2) kutoa mikopo mapema kwa wanaostahili kabla ya vyuo kufunguliwa.

3)Kutoa majina mapema kunamuwezesha mzazi kufanya maamuzi ya kufanya au kutafuta njia mbadala ya mtoto wake kuliko kuwa anachungulia kwenye mtandao kila siku bila kuwa na uhakika.

4)Mwisho kutaimarisha kujiamini kwa mtoto, mzazi na kuongeza ufaulu.

Ahsante.
 
Nchi yetu hii haina uwezo wa mambo mengi sana!

Kuna kipindi kama miaka 2 huko nyuma Mzazi mmoja alinilaumu kuwa kwanini namsomesha mwanangu Shule binafsi ya bei ghali ( Milioni 4 kwa mwaka) sekondari sioni kama nitakosa mkopo atakapotaka kujiunga Chuo Kikuu?

Nilimjibu Nchi hii mambo mengi hayana guarantee kwani masharti ya mikopo yanaweza kubadilika na kuwa kwamba watakaopewa mikopo ni wale tu waliofaulu vizuri lakini pia wawe yatima waliofiwa baba na mama!
Nikamuuliza, je tukifika hapo itabidi tukafoji vyeti vya vifo kuwa tumekufa ili watoto wetu wapewe mikopo?

Mimi nilishaona mapema tunakoenda ni kubaya zaidi! Nchi hii Viongozi wengi hawana uwezo wala ubunifu, uzalishaji wa bidhaa uko chini mno, wananchi wengi ni oya oya mashabiki wa Simba na Yanga!

Wazazi tutafute pesa tusomeshe watoto wetu vinginevyo tutakwama kabisa!

Mambo ni magumu sana Nchi hii sijui tukifika population ya watu Milioni 100 hali itakuwaje!
 
Back
Top Bottom