Ushauri kwa Serikali kwa mambo ya nje hasa Balozi

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,609
8,753
Mimi kama diaspora nitaanza na mawazo mawili makubwa halafu naomba wadau muongeze

1. Nashauri Mabalozi ambao wanateuliwa wapimwe uwezo sio tu kuchagua watu ambao ni madiplomasia wa wizarani na ofisi zetu za balozi lakini kuchagua watu ambao wanauzoefu wa biashara, uwekezaji na ushawishi. Tunahitaji wafanyabiashara, diaspora, na watu ambao wamewahi kuongoza biashara kubwa kama banks kuwa mabalozi. Tumechoka watu ambao wanaenda kujifunza kazi na wengi wa mabalozi ni slow sana na hawajui majukumu yao vizuri.

2. Balozi zote ziunde group za ushauri kwa ubalozi-Tanzania. Group hizi ziwe ni wataaalamu tofauti Watanzania au wadau wanaopenda maendeleo ya Tanzania. Mfano kwa hapa USA na Canada ambako mimi nina makazi kuwe na washauri wa mambo ya technologia, elimu, afya, ujenzi, ushirikiano na uwekezaji. Uzuri wa hizi group wadau ambao ni wataalamu watatoa ushauri bure lakini kwa kuhakikisha ushauri unatolewa moja kwa moja kwa balozi na wenyewe kupeleka Tanzania. Lakini hizo group vilevile kama kuna mtu anataka kuwekeza wanakuwa na uwezo kufanya mikutano moja kwa moja na wahusika kwa kutumia zoom meetings za kimkakati.

Hii inasaidia kwennye kutoa misaada Tanzania, kuongeza utaalamu na ushauri na kuongeza umoja. Tatizo la sasa balozi zetu zimekuwa zinasubiri badala ya wenyewe kuwa wadau wa kwanza wa kuanzisha group. Mfano Balozi badala ya kukimbilia kuandikisha majina ya diaspora wangetakiwa kuanzisha group hizi totafuti kwa kupitia wenyeviti wa jumuia za watanzania ambao wapo kija mji mkubwa. ingeweza ikawa website, wahatapp groups ... lakini lengo ni kutoa ushauri, kuongeza uwekezaji na misaada. Hizi group zitakuwa kama vyama ambapo uongozi ndani ya haya makundi unaweza ukawa na ukomo wake ili kutoa fursa za mawazo mapya.

 
Back
Top Bottom