The thinker27
Senior Member
- Sep 15, 2023
- 123
- 131
Habari za wakati huu wadau wa elimu
Kama picha inavojieleza hicho ndicho kiasi ambacho nimepangiwa na HESLB kwa mwaka wa masomo 2023/2024....
Nahitaji ushauri, maoni, faida na hasara za kukata rufaa pamoja na utaratibu wake unavyokuwa
Sababu kuu ya kuomba kukata rufaa ni kutokana na mfumo wa bodi kukataa kusave taarifa za TASAF wakati nilipokuwa nafanya application.
Mzazi wangu ni mnufaika wa TASAF na jina langu lipo katika mfumo wake wa malipo anaopokea kutoka TASAF na hata wakati najaza namba ya utambulisho ya kaya ya TASAF katika mfumo wa maombi ya mkopo jina langu lilikua likionekana pia na nilipokuwa naliclick dashbnard ikawa inaload then inaonesha kuwa "TASAF details saved succesfully" na katiki ka kijani. ila ikawa nikienda kupreview my details kwenye kipengele cha TASAF sponsored inaandka "NO" nikawa najaribu kuwapigia bodi wakawa wananiambia kuwa ni tatizo la kimtandao tu hivyo basi nikawa najaribu kujaza namba ya TASAF mara kwa mara .nikajaribu kurudia kwa takribani mwezi mzima bila mafanikio yoyote mpaka ikawa imebaki wiki 1 dirisha kufungwa ikabidi tu nisubmit taarifa maana hakukuwa na ahueni yoyote
Sasa majibu yametoka kama hivyo katika kiwango hicho na ada yangu inayotakiwa ni 1.6M. Kwa sasa baada ya majibu nimejaribu kuangalia kile kipengele cha "TASAF sponsored lakini bado imeandikwa NO, na hiyo inamaana kuwa bado HESLB HAINITAMBUI KAMA MLENGWA WA TASAF. je tatizo hili lilitokea kwangu tu au pia na kwa wengine?
Pia naomba kufahamu faida na hasara za kukata rufaa na pia je navyokata rufaa kiwango nilichopewa mwanzo kinakuwa stopped kwa muda au kinakua kishalipwa?
Naomba kuwasilisha wakuu na samahani kwa kutumia lugha ndefu ni katika hali tu kujenga kueleweka. Nawatakia majukumu mema katika ujenzi wa taifa