ushauri jamani

Bukayo jr

JF-Expert Member
Mar 24, 2011
2,782
1,638
Habari wana jf leo nina hitaji ushauri wenu, kuna rafiki yangu huku mwanza ana mchumba wake wamepanga waoane mwakani february lakini sasa huyu jamaa anaishi mwanza mchumba wake(msichana) dar es salaam, hivi karibuni binti kamkatia mwasiliano kisa anasoma cpa yani yuko busy hata sms hakuna kwa wiki mbili mfululizo nakumbuka aliwahi kunung'unika miezi kadhaa nyuma kachuniwa mpaka akadata akawa anahisi kuachwa na binti lakini binti akiulizwa anadai eti cpa inanipeleka lesi lakini jamaa anauliza hata sms? Jamaa kampigia mpaka kaniomba ushauri niasaidieni nikampe your advice
 
mwambie hizi ni dalili za jamaa yako kushika pembe huku wenzie wana.........
 
Habari wana jf leo nina hitaji ushauri wenu, kuna rafiki yangu huku mwanza ana mchumba wake wamepanga waoane mwakani february lakini sasa huyu jamaa anaishi mwanza mchumba wake(msichana) dar es salaam, hivi karibuni binti kamkatia mwasiliano kisa anasoma cpa yani yuko busy hata sms hakuna kwa wiki mbili mfululizo nakumbuka aliwahi kunung'unika miezi kadhaa nyuma kachuniwa mpaka akadata akawa anahisi kuachwa na binti lakini binti akiulizwa anadai eti cpa inanipeleka lesi lakini jamaa anauliza hata sms? Jamaa kampigia mpaka kaniomba ushauri niasaidieni nikampe your advice

...aaahhh, mbona ni dalili za kawaida kabisa hizi?...anashangaa shangaa nini sasa?
 
Nakumbuka mwezi uliopita alikwenda wapange mikakati ya marriage yao lakini akamkuta binti yuko bize kwa sana na hapo alikwenda kikazi akakaa wiki mbili, binti anadai akimaliza paper november inayoanza keshokutwa mambo yatakuwa mazuri lakini huo muda wa kupangilia ndoa yao unakuwa complicated kwani ruhusa ya kwenda dar hawez kuipata tena mi natamani nimshauri a atafte mwingne lakini mapenzi ya watu wawili si mnajua?
 
Kwanini amuwazie mabaya mchumba wake wakati mazuri yapo.
 
...aaahhh, mbona ni dalili za kawaida kabisa hizi?...anashangaa shangaa nini sasa?

anashindwa elewa ni Cpa au vp nadhani wanaofanya Cpa watueleze vp kama huwa hawawasiliani na waume au wenza wao mitihani ikikaribia
 
Kwanini amuwazie mabaya mchumba wake wakati mazuri yapo.

kwani mabaya ndo huangaliwa zaidi, sio issue ila anaogopa kama kweli ndo ubize akiajiliwa wakaoana atamjali kama mume kweli?
 
anashindwa elewa ni Cpa au vp nadhani wanaofanya Cpa watueleze vp kama huwa hawawasiliani na waume au wenza wao mitihani ikikaribia

Mimi nilikuwa napenda niambiwe best wishes kutoka kwa mchuchuuuu kabla ya pepa na nikimaliza pepa aniambie pole eeenh baby, ulikuwaje? Najisikia raha yaani kama dunia ni yetu wawili vile. Na mimi pia nilikuwa namuambiaga. Ninachomaanisha ni kwamba hata ratiba yangu ya mitihani alikuwa anaijua mapema na sio nimkumbushe.
 
kwani mabaya ndo huangaliwa zaidi, sio issue ila anaogopa kama kweli ndo ubize akiajiliwa wakaoana atamjali kama mume kweli?

Mwambie huyo mwanaume akajipange tena sawa sawa, mali yake yaliwa na wachakachuaji! akiajiriwa ndo atakuwa busy mara mbili ya hapo!
 
Mwambie huyo mwanaume akajipange tena sawa sawa, mali yake yaliwa na wachakachuaji! akiajiriwa ndo atakuwa busy mara mbili ya hapo!

nitamwambia...ila ebu nijuze ukiwa wakaribia paper ndo hata sms na simu hampigi wala kupigiana? Na kama kwa case ya thread hapo juu huyu demu anamwibia jamaa yangu si ndio?
 
Mitihani ya CPA ni kiboko inabidi ujizatiti sana ili kuhakikisha unafanya vizuri, lakini sidhani kama inakukosesha hata dakika chache kwa siku za kuwasiliana na watu muhimu katika maisha yako.
 
Mitihani ya CPA ni kiboko inabidi ujizatiti sana ili kuhakikisha unafanya vizuri, lakini sidhani kama inakukosesha hata dakika chache kwa siku za kuwasiliana na watu muhimu katika maisha yako.
Kweli bhana
 
moja jumlisha moja ni 2 na sio 12.hata uwe busy vipi,kama unae unaempenda.kutuma sms ni kitu simple tu.maybe hampendi kiivyo,bora ampe muda wa hayo masomo yake.na huyo jamaa bora na yeye akae kimya[ingawa ni ngumu]akiona mambo yanaenda hivyo hivyo.achukue maamuzi.kabla ya ndoa unakoleza mapenzi yeye ndio analegeza uzi.
 
Mwambie jamaa amwambie binti ameamua kusitisha ndoa kwanza au kuisogeza mbele.
Hlf asubiri reaction ya binti.
Kama kweli ni pepa zinazingua binti ataomba msamaa na kujirekebisha
Kama ni uzushi binti ataona poa tu kashushiwa mzigo ,maana nahisi binti hataki ndoa ana mtu mwingine
 
Kwani Novemba si hiyo hapo tu asubiri aone au?

Lkn namuelewa huyo mwanamke kuwa alivyokuwa na mitihani ya cpa hakutaka kuwasiliana na huyo jamaa, kuna wanaume wengine hawajui kuwa supportive. Wewe una mitihani ndo kwanza anataka wewe umpembejee yeye na matatizo yake ya kila kukicha.
 
Back
Top Bottom