Usanii unaofanywa na Mnyika na CHADEMA juu ya swala la Bei za Umeme na Maswala ya tanesco.

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
1,657
2,252
Usanii anaokujanao Mnyika juu ya kukusanya maoni juu ya ongezeko la umeme ni mkubwa sana na unalengo la kutupumbaza kama maswala ya kuundwa tume kilasiku na serikali.


Usikubari mtu akakufundisha jinsi ya kuanza Kufikiri. Kisha ukakariri. Muulize Mnyika waliitaji sahihi za watanzania Kugomea hotuba ya Raisi Bungeni ili kushinikiza katiba mpya? Walipata sahihi za watanzania wangapi kugomea vikao vya bunge kushinikiza maswala mbalimbali ya katiba. Ukitafakari msisitize aache usanii.

Swala la tanesco hoja sio bei ya umeme tu. Ila uendeshwaji unaopelekea shirika hilo kushindwa kujiendesha na kuelekea kufa, Migao mikubwa ya umeme na Umeme kukatika katika muda mrefu.

Ni waz kuwa

1. Makampuni yanayoiuzia tanesco umeme kwa bei ya juu sana yana mikono ya maswaiba wa viongozi Kama Lowasa, Rostamu na huwaingizia Mabilioni ya fedha wanazotumia kuutafuta uraisi.

2. Makampuni hayo pia yanachangia zaidi ya 80% ya fedha za Mbowe nje ya Nchi ili Mbowe na Chadema wasije na hoja na Vurugu dhidi ya uendeshwaji wa shirika hili. CHADEMA ina uwezo kabisa wa kufanya mashinikizo nje na ndani ya bunge hadi mfumo mzima wa uendeshwaji tanesco utakapobadilishwa

3. Mnyika na Chadema inajua kuwa Miundombinu ya Tanesco ni Michakavu sana zaidi ya 60% ya nguzo za umeme za mbao zimepita muda wake wa kubadilishwa na zaidi ya 35% ya nguzo hizo zimeoza kabisa na hiyo inatokana na asilimia kupwa ya mapato ya tanesco huishia kulipa garama za uzalishaji umeme.

4. Kuna upotoshwaji mkubwa ulifanywa na waujumu wa miradi ya Tanesco juu ya kuzuia uanziswaji wa miladi wa miradi mikubwa ya umeme wa maji na isiyo na garama kubwa za uendeshaji kama Mradi mkubwa wa Bwawa la Kihansi na wa Bonde la Mto Maragarasi ambayo yote visingizio ni kulinda spishi za Vyura ambao wanapatikana maeneo husika ili wasitoweke duniani kutokana na miradi hiyo huku ukweli halisi dili za kuagiza mafuta ya mitambo ya umeme kwa mkoa wa Kigoma na Iptl ingeyeyuka.

Upotoshwaji mkubwa hapa ni hasa juu ya öngezeko la bei zenyewe.
Tanesco na Mnyika mwenyewe wanasema watumiaji wadogo hulipia tsh 100 kwa unit kwa uniti 0-75 za awali hapa si kweli kabisa.
Kuna usanii mkubwa hapa. Gharama hizo zinawahusu watumiaji wenye mita za zamani tu na hizi hazilalamikiwi na huwa zinatajwa haraka kuonesha garama za umeme sio kubwa.
Ukweli ni kuwa ukiwa na Mita ya Luku tu ata ukiwa mtumiaji mdogo kiasi gani wa nyumbani hutalipia tsh 365 +vat kwa unit kuanzia unity ya kwanza + tsh 7,000 kila mwezi kama service charge.

Kwa wanaounganishwa na umeme sasa vijijini pia wote huwekewa Luku na hulipia Garama hizi(365 per unity na 7000 ya service charge kuanzia unity ya kwanza).
Na Watumiaji wengine wenye mita za kawaida zaidi ya asilimia 80 ziling'olewa na kuwekewa Luku na hulipa Garama za juu kabisa za umeme(hizo juu) ambao wengiwao matumizi yao ni kati ya uniti 10 hadi 70 kwa mwezi.
Hivyo Hawa ambao matumizi yao ni ya chini kabisa ndio wenye kiwango cha juu kabisa na pia kiwango hiki cha Juu kuliko vyote za bei ya umeme huwagusa watengeneza barafu, karakana mbalimbali mashine za kusaga na wajisiliamali mbalimbali.

Swali hapa vipi watumiaji wadogo kabisa waliofungiwa Luku ambao ni zaidi ya 90 asilimia ya watumiaji wadogo walipie kiwango cha Juu kabisa cha umeme ambao ni tsh 306bila vati au 365+vat+ewura huku wakubwa kabisa wanaoutumia kwa kuzalishia wakilipia tsh 159 kwa unity?

- Hizi gharama za Service charge tsh 7000kwa mwezi kwa watumiaji wadogo zina uhalali gani? Mbona kwa watumiaji wa mita za zamani wadogo hazipo na ndio zinagarama kubwa za uendeshaji kama wasoma Mita, zinachakachulika kirahisi na ni za malipo ya baada?

- Huu usanii wa kuwaita wenye matumizi madogo kuwa ni watumiaji wakubwa wa nyumbani mara baada ya kuunganishiwa mita za Luku umeanza Lini?

Mnyika na Tanesco acheni ufafanuzi wenye upotoshaji juu ya watumiaji kwa kuweka makundi mara T1, D1, Sijui T2 ni kutaka kutuchanganya na kutuona wote hatujui lolote linaloendelea.

Mlicharuka juu ya katiba swala ambalo ni indirect kwa wananchi mkaweza. Vipi swala hili direct kwa maisha ya watu. Vipi tukae kimya sababu ya mtu mmoja kula Mbowe?
 
Mkuu kwa jinsi bei ya umeme inavyoumiza mimi nitaunga mkono juhudi zozote kushinikiza umeme ushuke bei.

Hii inaathiri maisha yetu ya kila siku, wekeni pembeni chuki zenu binafsi dhidi ya Mnyika na roho zenu mbaya za kiCCM tumuunge mkono Mh Mnyika tusizidi kuwaendeleza mafisadi.

Watanzania tunaishi kwa kuwaneemesha Rostam, Lowassa na Ridhiwani Kikwete tu
 
Hoja ni bei ya umeme kwa kuwa ndio inayomgusa mwananchi hizo nyingine ni blah blah tu.

Kama umeme unawafaidisha kina mbowe vipi kuhusu bei ya gesi,simu,sukari,unga,elimu,n.k
 
Mnyika jembe!

Umeme ni lazima ushuke,usiposhuka tutakutana kwenye sanduku la kura 2015!

Mabazazi wakubwa nyie!
 
Hoja ni bei ya umeme kwa kuwa ndio inayomgusa mwananchi hizo nyingine ni blah blah tu.
Kama umeme unawafaidisha kina mbowe vipi kuhusu bei ya gesi,simu,sukari,unga,elimu,n.k

Huna la maana umekaa kushabiki zaidi,Mbowe anahusikaje na kupanda kwa bei ya umeme?jaribu kushirikishaga na kichwa kidogo so kutumia makalio tu mud a wote.
 
Hoja ni bei ya umeme kwa kuwa ndio inayomgusa mwananchi hizo nyingine ni blah blah tu.
Kama umeme unawafaidisha kina mbowe vipi kuhusu bei ya gesi,simu,sukari,unga,elimu,n.k

Tukusanye Signs....Umeme ushuke bei...
 
Umeme unaumiza jamani.......tuache siasa, hili shirika la tanesco limeprove failure. We need competition in this sector so that we as consumer would have choice and alternative ways of budgeting our incomes. As of now this monopoly institute cant do anything to help us.
 
Huna la maana umekaa kushabiki zaidi,Mbowe anahusikaje na kupanda kwa bei ya umeme?jaribu kushirikishaga na kichwa kidogo so kutumia makalio tu mud a wote.

Na Wewe Uwe Unamwelewa Kwanza Mwenzako...Alichookosea Hapo Ni Kipi?
 
Umeme unaumiza jamani.......tuache siasa, hili shirika la tanesco limeprove failure. We need competition in this sector so that we as consumer would have choice and alternative ways of budgeting our incomes. As of now this monopoly institute cant do anything to help us.

Right....Right...*Nodding*
 
Nildhani ni muda wa M4C sasa nchi nzima bila kujali itikadi,kumbe signature!!!!!!??????

Mpaka mkiamka wanasiasa watakuwa wamemaliza yao!!!!!!!!!
Maandamano ya nusu siku tu nchi nzima,saa kumi jioni ya siku hiyo hiyo bei ingeshuka mbona!!!!


Kalamu na karatasi katika kudai haki!!!!!!!??????
 
Ningumu sana kwa great thinker yeyote kukubal hizo hoja mufilisi. Mimi namsapot JJ MNYIKA kwan bei ya umeme inaniumiza mimi.Tatizo la ccm kila kitu kikiwashinda mnasingizia Cdm , meshendwa kuendesha serekal kilichobaki ni kuwanyonya watanzania maskini. Ccm shame on you.
 
Mijitu mingine bana hivi nyie kila kitu mbowe na chadema tu? Gesi je? mbona kila kitu kimepanda nchi hii? Tembo wanauliwa kila siku napo mbowe anahusika?sijui mnalipwa kiasi gani kuleta upuuzi humu
 
Mnyika jembe!

Umeme ni lazima ushuke,usiposhuka tutakutana kwenye sanduku la kura 2015!

Mabazazi wakubwa nyie!
Khaa!! Mie namshangaa Mnyika, umeme umepanda bei si zaidi ya 40% amelikomalia. Huku jimboni kwake bei halali ya maji ya dawasco ni shs 1,050/- kwa lita 1000 lakini sisi tunanunua kwa shs 15,000/- kwa lita 1000 ambayo ni karibu na ongezeko la 1000%. Yote kwasababu anahisa kwenye hii biashara ya maji. Miaka mitano tunaumia huku yeye akitajirika. 2015 tunampiga chini vibaya afanye kazi za chama kwa uhuru.
 
We Mshumbizi huoni umeme unaumiza kwa bei? au we mambo safi sana.. sukuelewi acha kushambulia mtu mmoja mmoja kwenye hili tunacholalamika ni umeme ushuke kila mtanzania asiumie na sio siasa,

Umeme si wa ccm wa chadema kuumia tunaumia sote kwapamoja.
 
Hii post yako inaonekana umetumwa Ms serikali ya ccm.huwezi post ya kijinga kama hiyo.kwa hiyo unataka watu waendelee kunyonywa kwa maslahi ya Akina lowasa na rostam?tumia akili
 
Back
Top Bottom