Usaili kada za Serikali kufanyika Dodoma ni kipengele. Mfumo ubadilishwe

Just Distinctions

JF-Expert Member
May 5, 2016
2,728
5,365
Habari za wakati huu,

Hili suala la usaili kufanyika Dodoma lizingatiwe tena na tena, sikatai lengo lilikuwa ni jema ila changamoto zimekuwa ni nyingi unakuta mtu anaitwa usaili wa kuandika tarehe 25 kisha ukipita hapo wa vitendo tarehe 28 ama mahojiano 29, sasa ukiangalia kwa haraka, asie na ndugu wala rafiki (ambao ndio asilimia nyingi) gharama ni kubwa kwani guest sio chini ya siku 5, japo mchakato unafanyika ili kupoza na waomba ajira wafanyie katika kanda zao.

Kwa wakati uliopo basi wajitahidi kama wa kuandika ukifanyika tarehe 25 kwa mfano basi wa mahojiano au vitendo uwe siku inayofata, vinginevyo ni kupeana gharama zisizoepukika.

Ukifika pale Nyerere Square ndio balaa, wanaosaka ajira kama wote maana ndio sehemu ya kupotezea muda na huu mji ulivyo hakuna pa kwenda kuzuga hivyo unakuta kwenye kimbweta wasailiwa kama wote wana-buy time, ukifanya ka-survey kadogo utakuta wengi ambao wanazuga hapa ukiacha wazawa ni watu waliokuja kwenye usaili, utaenda wapi tena wakati mji hauna vipengele vingi?

Kila la heri kwa wote ambao bado wanapambania kombe, one day Yes.

Je wewe ulikumbana na changamoto ipi kwenye hizi saili za Dodoma?
Karibu

Pia soma: Kikwete: Mfumo wa usaili wa ajira sasa kufanyika online. Hakuna tena kwenda Dodoma kwa usaili
 
Ni changamoto kwakweli, ila ishu napo walifanya kwa Kanda majibu yanachukua mwezi hapo napo mtu unakuwa hujielewi upo upande upi sasa daah, hii nchi ni ngumu sana mtu Hadi uje upate ajira.

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Nilienda kwenye usaili wa kuandika ulikua tarehe 5 September kwahiyo nilienda tarehe 4. Tarehe tano hiyo niliingia kupiga paper na kutoka saa 5:30 pm. Nikachukua boda kutoka UDOM mpaka magorofani(Iringa road) nikapata usafiri wa bus na kusepa niliingia Iringa saa sita usiku. Nikalala next day nikaunga home.
 
Nilienda kwenye usaili wa kuandika ulikua tarehe 5 September kwahiyo nilienda tarehe 4. Tarehe tano hiyo niliingia kupiga paper na kutoka saa 5:30 pm. Nikachukua boda kutoka UDOM mpaka magorofani(Iringa road) nikapata usafiri wa bus na kusepa niliingia Iringa saa sita usiku. Nikalala next day nikaunga home.
hapo sijaelewa vyema matokeo ya written yalikuwaje? au uliyapata baada ya kutoka, maana si huwa baada ya kuandika kunafata kipengele cha mahojiano au vitendo kutegemeana na kada uliyopo?
 
Back
Top Bottom