mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,664
- 18,040
Kwa sasa imekuwa kama utaratibu. Kwa mfano ulio hai kuna baadhi ya waombaji wa ajira MDA's na LGA's walipewa taarifa ya kuitwa kwenye usajili tarehe 07/01/2023 na wengine wakaitwa kama majina ya nyongeza siku tano baadaye yaani tarehe 12/01/2023. Na wote hao watafanya usaili tarehe 15/01/2023.
Tunashukuru kwa sababu walioitwa baadaye ni kama walikuwa wamesahaulika kwa hiyo wakikumbukwa tunashukuru. Ni kama hatimaye wametendewa haki.
Lakini tunasema si haki kwa sababu hao walioitwa awali ana siku tano zaidi ya maandalizi kuliko hawa walioitwa baadaye maana tarehe ya usaili ni moja. Kwa kuwa tarehe ya usaili ni 15/01/2023 walioitwa awali wana siku nane (8) za kujiandaa na usaili wa kuandika (written interview) wakati walioitwa baadaye wana siku tatu (3) tu za kujiandaa na usaili huo.
Kwa hiyo hao waliopata muda mrefu wa maandalizi wana nafasi nzuri zaidi ya kufanya vizuri kwenye usaili kuliko waliopata muda mfupi wa maandalizi. Hapo ndipo tunasema si haki.
Kwa hiyo tunaomba sana tume ya ajira wajitahidi kutoa uwanja sawa kwa wasailiwa wote.