USAHIHI: Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe na kujitenga na ziara ya viongozi wakuu

Status
Not open for further replies.
Zzk atulie kwa chadema narudia tena hakuna zito bila cdm mungu bariki chadema nawana chadema wote
 
...... [B said:
sikuweza kushiriki kwani ni hatari mno kuacha PAC chini ya wabunge wa CCM peke yake.[/B] Leo kamati inahoji Wizara ya Elimu yenye madudu kibao, Hazina yenye kukusanya mapato yote ya Serikali na ratiba nzima nitawasilisha hapa. Haya yote uongozi wa chama unajua. Ni mgawanyo tu wa majukumu. Hata hivyo nimeshiriki kuandaa mikutano katika mkoa wa Kigoma na gharama zote za maandalizi nimetoa mimi. Hata gari anayotumia mwenyekiti huko Kigoma ni gari yangu. Kusema nimesusa ni uzushi sana wenye lengo la kuleta mgogoro kwenye chama.

Pili, mimi ni mbunge kutoka Kanda ya Magharibi. Kila kanda imepewa wajibu wa kujiimarisha kichama. Nimekuwa nilifanya hivi toka kanda zimeundwa. Kuanzia mkutano wa mwanzo nimekuwa nikitimiza wajibu wangu wa kuhakikisha kwamba kanda ya magharibi inakuwa imara kichama. Nimefanya ziara kadhaa mkoa wa Kigoma na mkoa wa Tabora. Hivi sasa kanda zote zinapaswa kufanya uchaguzi wa ndani ya chama. Nimeamua kuanzi tarehe 20 Septemba (mara baada ya Bunge mkutano wa 12 kumalizika) kuanza ziara ya kanda ya magharibi kuchochea ujenzi wa chama kuanzia matawi ili tuweze kuendana na ratiba ya uchaguzi. Ziara hii itafuata taratibu zote za chama na sijaamua naifanya na nani maana maafisa wa chama wanapingiwa na katibu Mkuu.

Ninasikitika sana kwamba kumekuwa na tabia za kuchonganisha viongozi wa chama bila sababu kwenye mitandao ya intaneti. Kwa mtu anayeipenda chadema hawezi kufurahi mambo haya.

Mimi kama Zitto siwezi kufanya jambo lolote la kuathiri chama changu ambacho nimeshiriki kukijenga kwa kadiri ya uwezo wangu. Ninaomba pia watu wengine watumie muda zaidi kuunganisha viongozi badala ya kuwagwa. Tunahitaji sana umoja na mshikamano wa dhati
......Hapo kwenye red, pamenisisimua kweli!
 
Mmajisumbua nini wakati January Makamba maeshatunukiwa uraisi 2015?
Mimi sijui wewe ni nani. Ninachikifahamu ni kwamba wewe siyo Great Thinker na sababu unafahamu. Jaribu kuwa objective zaidi mwana jamvi!
 
Mi nimefurahishwa na maelezo ya Mh Zitto, Musimamo huu unatakiwa ukatumika mahala pote utakapoona jina lako linitumikavibaya na watu wasio kutakia mema kisiasa, migongano mingi na viongozi wenzako inatokana na wewe kukaa kimya jina lako linapotumika kuleta migongano ndani ya CDM
 
Good, hiyo ndio kauli ya msemaji wa chama. nilionya aliyeanzisha ile thread ni mchonganishi. Ahsante hon. Zitto kwa ufafanuzi.
 
Na ilikua hatari mno kuacha kushiriki bonanza na kuwaachia CCM peke yao kule national stadium wakati Kikao cha Kamati kuu kikiendelea.
Na ilikua hatari sana kuacha ziara za nje na posho na kuwaachia CCM pekee badala ya kuingia ofisini kumsaidia katibu mkuu
Na ilikua salama sana sana kutaka Lwakatare atoswe na kisha kuvujisha barua kwenye mitandao na kuandika kuwa barua imevuja ofisini kwa katibu mkuu.Hapo ulikua hauwapi watu wa nje faida!Hapo haukulenga kuichafua ofisi ya Katibu Mkuu.Watu wanakugombanisha au ujinga wako pamoja na kushikamana na maadui wa chadema ndiyo unakuponza?Acha unafiki kaka
 
ZZK ww ni jembe nakuamini sana kijana mwenzangu, usiogpe hii karata ya ccm kutugawa ila ujue tumesha wafahamu, ww piga kazi kwenye PAC wasije wakachachua hata sent moja.
HII NI LUMUMBA PROJECT wala kamanda usishangae.
MUNGU AKULINDE ZZK VIVA CDM
 
Zitto hata aseme nini hakuna mtu anayemwamni tena! Naona muda umepita habari zake hazijatoka Mwananchi au rafiki aliyekuwa anamjenga kimkakati amegoma?
 
Kuna kashfa zilizotoka kwenye gazeti la Changamoto zikimhusisha zitto kuchota pesa kwenye taasisi za serikali zilizochini ya kamati yake ikiwepo Ngorongoro kreta kwa kutumia NGO yake. Mpaka sasa hajajibu kashfa hiyo, ina maana ni kweli.
 
ZZK ww ni jembe nakuamini sana kijana mwenzangu, usiogpe hii karata ya ccm kutugawa ila ujue tumesha wafahamu, ww piga kazi kwenye PAC wasije wakachachua hata sent moja.
HII NI LUMUMBA PROJECT wala kamanda usishangae.
MUNGU AKULINDE ZZK VIVA CDM

CCM ndiyo iliyomtuma ashikamane na Msacky na kutaka Lwakatare atoswe ili chama kije kifutwe sio?
 
Well said kamanda @ZITO,umegusa jambo la msingi kuwa Ziara yako itafuata taratibu zote za chama na hujui utaifanya na nani maana maafisa wa chama wanapingiwa na katibu Mkuu Dr.W.Slaa.
Tutumie muda wetu zaidi kuunganisha viongozi badala ya kuwagawa. Tunahitaji sana umoja na mshikamano wa dhati
 
Last edited by a moderator:
Kaka Zitto mie binafsi nakukubali sana ndani ya chama ila tatizo ni moja kuna kipindui huwa sikuamini napata sana mashaka nawewe. kubali kataa wanachadema wengi hasa vijana hawakuamini wanakuona kama unaajenda ya siri. jitathmini na ujirekebishe tumalize kazi tuliyoianza zamani. M4C 4rever.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom