McDeedanny
Member
- Apr 14, 2013
- 56
- 7
Zzk atulie kwa chadema narudia tena hakuna zito bila cdm mungu bariki chadema nawana chadema wote
......Hapo kwenye red, pamenisisimua kweli!...... [B said:sikuweza kushiriki kwani ni hatari mno kuacha PAC chini ya wabunge wa CCM peke yake.[/B] Leo kamati inahoji Wizara ya Elimu yenye madudu kibao, Hazina yenye kukusanya mapato yote ya Serikali na ratiba nzima nitawasilisha hapa. Haya yote uongozi wa chama unajua. Ni mgawanyo tu wa majukumu. Hata hivyo nimeshiriki kuandaa mikutano katika mkoa wa Kigoma na gharama zote za maandalizi nimetoa mimi. Hata gari anayotumia mwenyekiti huko Kigoma ni gari yangu. Kusema nimesusa ni uzushi sana wenye lengo la kuleta mgogoro kwenye chama.
Pili, mimi ni mbunge kutoka Kanda ya Magharibi. Kila kanda imepewa wajibu wa kujiimarisha kichama. Nimekuwa nilifanya hivi toka kanda zimeundwa. Kuanzia mkutano wa mwanzo nimekuwa nikitimiza wajibu wangu wa kuhakikisha kwamba kanda ya magharibi inakuwa imara kichama. Nimefanya ziara kadhaa mkoa wa Kigoma na mkoa wa Tabora. Hivi sasa kanda zote zinapaswa kufanya uchaguzi wa ndani ya chama. Nimeamua kuanzi tarehe 20 Septemba (mara baada ya Bunge mkutano wa 12 kumalizika) kuanza ziara ya kanda ya magharibi kuchochea ujenzi wa chama kuanzia matawi ili tuweze kuendana na ratiba ya uchaguzi. Ziara hii itafuata taratibu zote za chama na sijaamua naifanya na nani maana maafisa wa chama wanapingiwa na katibu Mkuu.
Ninasikitika sana kwamba kumekuwa na tabia za kuchonganisha viongozi wa chama bila sababu kwenye mitandao ya intaneti. Kwa mtu anayeipenda chadema hawezi kufurahi mambo haya.
Mimi kama Zitto siwezi kufanya jambo lolote la kuathiri chama changu ambacho nimeshiriki kukijenga kwa kadiri ya uwezo wangu. Ninaomba pia watu wengine watumie muda zaidi kuunganisha viongozi badala ya kuwagwa. Tunahitaji sana umoja na mshikamano wa dhati
Mimi sijui wewe ni nani. Ninachikifahamu ni kwamba wewe siyo Great Thinker na sababu unafahamu. Jaribu kuwa objective zaidi mwana jamvi!Mmajisumbua nini wakati January Makamba maeshatunukiwa uraisi 2015?
Zito+shibuda,hawaaminiki na hawana mvuto tena kisiasa,kwangu mimi wawepo cdm wasiwepo yote sawa.
Na ilikua hatari mno kuacha kushiriki bonanza na kuwaachia CCM peke yao kule national stadium wakati Kikao cha Kamati kuu kikiendelea.
Na ilikua hatari sana kuacha ziara za nje na posho na kuwaachia CCM pekee badala ya kuingia ofisini kumsaidia katibu mkuu
Na ilikua salama sana sana kutaka Lwakatare atoswe na kisha kuvujisha barua kwenye mitandao na kuandika kuwa barua imevuja ofisini kwa katibu mkuu.Hapo ulikua hauwapi watu wa nje faida!Hapo haukulenga kuichafua ofisi ya Katibu Mkuu.Watu wanakugombanisha au ujinga wako pamoja na kushikamana na maadui wa chadema ndiyo unakuponza?Acha unafiki kaka
Kuwa makini kaka Zito na mabepari ndani ya Cdm hawana kheri na wewe
ZZK ww ni jembe nakuamini sana kijana mwenzangu, usiogpe hii karata ya ccm kutugawa ila ujue tumesha wafahamu, ww piga kazi kwenye PAC wasije wakachachua hata sent moja.
HII NI LUMUMBA PROJECT wala kamanda usishangae.
MUNGU AKULINDE ZZK VIVA CDM
Kuwa makini kaka Zito na mabepari ndani ya Cdm hawana kheri na wewe