Leak
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 52,210
- 42,072
Katibu wa Itikadi naUenezi chama cha Mapinduzi (Paul Makonda) amewataka viongozi wa Umma na wa siasa kuacha mara moja tabia ya kusubiri ziara ya Viongozi wakuu wa Umma ndio waje kueleza mazuri na mipango au kutoa ufafanuzi wa mambo muhimu yanayo husu miradi ya jamii na utekelezwaji wake!
Paul Makonda amewataka viongozi wote wa Umma hasa wabunge na madiwani wa chama cha mapinduzi kuwafata wananchi na kwenda kuwatatulia kero zao na kuwasikiliza siyo mpaka wasubiri ziara ya Mh Rais au Waziri Mkuu ndiyo waende kugombania kipaza sauti kueleza wakati muda wa kueleza wanao mwingi !
Amesema kumezuka tabia ya wana CCM kukaa kimya tuu bila kuisemea serikali na chama kuhusu mazuri yaliyofanywa na kuwapa mwanywa watoa taarifa kutoa taarifa za uongo huku viongozi na wahusika wanaopaswa kusema na kutoa ufafanuzi wakiwa wamekaa kimya wakati wanalipwa na wengine waliomba kura kuwa viongozi wa nafasi mbali mbali ndani ya CCM.
Amesema ni wakati wa viongozi wa ngazi zote ndani ya CCM na serikali kuendelea kujitafakari kwakuwa mambo mengi yanafanywa na serikali lakini watu hawasemi wala kutoa ufafanuzi mpaka wasubiri ziara ya Rais….
Paul Makonda amehitimisha ziara yake kanda ya ziwa akiwataka viongozi wa serikali na chama kuwafata wananchi na kuwasikiliza!
Inasemekana kanda inayofuata ni kanda ya kaskazini mwa Tanzania au kusini…