Bin Maryam
JF-Expert Member
- Oct 22, 2007
- 685
- 13
Eddy, hawa wanataka kuchimba na siyo kuwekeza kwenye kinu etc. Hii uranium watakayoichimba ni kama dhahabu na mineral nyingine wanazozichimba na sisi tunabakiwa na mashimo tuu! Hakuna mtaji hapa!
FM:
Sasa unalalamika nini? Tukisema tujifunze tuanze wenyewe unaleta longolongo. Tukiwapa WAPWEKEZAJI unasema watatuachia mashimo tu. Je unapendekeza nini? Maana mpaka sasa unakatoa hoja kwa kuonyesha uzembe kwa vile tulivyoshindwa au tunavyoshindwa.
Mimi nataka NYUKI na kama nina matatizo naomba uniambie nianze kujibadilisha na kujenga misingi ya technologia hiyo. Na hata kama itachukua miaka ishirini au hamsini weka estimation zako.
Tanzania imeshindwa kutengeneza viatu, imeshindwa kupambana na malaria. Na kwa ujumla imeshindwa kufanya vitu vingi ambavyo viko ndani ya uwezo wake.
Pamoja na kushindwa kwetu kuna uwezekano mkubwa sana kuwa kizazi kinalichozaliwa baada ya Azimio la Arusha kinaweza kuleta mabadiliko iwapo mambo fulani yatatimizwa au kutafutiwa ufumbuzi.
Unasema Tanzania inapenda miradi mikubwa kwa sifa. Hayo makosa yalifanyika na yametuingiza katika madeni mabaya. Katika miradi ya nguvu za umeme Tanzania haijafanya kwa sifa na miradi hiyo inatumikia taifa ukiondoa IPTL na Richmond ambayo haikufuata taratibu za kibiashara na ufundi.