Uranium Mining Projects In Tanzania: Progress...

Mi nadhani wote hapa mna point cha muhimu ni kuidentify our priorities. Tanzania yetu asilimia kubwa sana ya wananchi hawana uhakika na mlo wa pili, wanatumia nishati ya kuni za kuvuna porini, hawana elimu, wakiugua wanapona kwa kudra za Muumba na wala sio dawa za hospitali, nyumba niza majani..you can go on and on.....sasa jamani kwa mwendo huo ndo unahitaji Neuclear? uifanyie kazi gani? wakati watanzania wanaotumia umeme ni chini ya 10%!!!??

Neuclear power might be a good idea, but for now we have some pressing issues which are far far more important for our survival as a nation than Nukes! Mtu aliyelala njaa huwezi kumwambia achangie pesa ya kuvuta umeme! Kabla ya kumwambia huo umeme utamsaidia vipi.....atakushangaa. Au watu humu mko ughaibuni that you are so detached to the realities in our country?? Maybe!

Lets identify our priorities correctly. Huwezi kufikiria/kutamani gari wakati uwezo wa baiskeli haupo. Lets be realistic with our goals and aspirations! we should cross the bridge when we are there!
 
Masanja:

Nashukuru kwa mchango wako. Lakini sirudishi majeshi nyuma. Level ya umasikini ipo direct propotion na matumizi madogo ya enegy.

Unaposema kuwa watanzania wengi hawana uhakika na mlo wa pili, huko sahihi kabisa. Lakini unachotakiwa kukumbuka ni kuwa kukosa mlo ni kupunguza kiwango cha CALORIES (FOOD ENEGY) ambacho mtu huyo angetumia kufanya kazi za kuleta maendeleo. Na ukiona watu wanacheza bao, pool au kukaa kijiweni wakati wa kazi sio wajinga kwa sababu shughuli hizo zinahitaji CALORIES ndogo kuliko kwenda kazi za shamba.

Na upungufu wa CALORIES unamfanya mtu hasielewe anachofundishwa, na ashindwe na kujenga makazi ya maana.

You are what you eat. Magonjwa mengi Tanzania yanatokana na upungufu wa chakula bora.

Kama ni kuweka priorities zetu kisawasawa, basi program nyingi tunazoita za maendeleo zisimame. Na priority ya kwanza iwe uzalishaji na matumizi ya enegy. Kwani ni enegy peke yake itakayofanya uzalishaji wa mazao ya chakula uongezeke na ongezeko la chakula litawafanya watanzania kula vizuri na kuwa CALORIES (FOOD ENEGY) za kufanya kazi vizuri, kusoma vizuri na kupunguza magonjwa na kujenga nyumba nzuri.

Na nchi yoyote yenye kuweka masuala ya enegy mbele haitasahau NYUKI japokuwa katika masuala ya utafiti tu.
 
Again, Bin Maryam unaongea kama mwanasiasa. Aliyekuambia nani kuwa wanafunzi wa Pakistan na India wanakuta lab vyuo vikuu? India kila siku ilikuwa na matabaka. Imekuwa na world-class scientists kwa muda mrefu tuu.Naamini the same is true for Pakistan. Huu umahiri wao kwenye sayansi haukutokea hewani. Wameujenga kwa muda mrefu. Usisahau kuwa population ya India inazidi population ya watu weusi na kwa hiyo wana pool kubwa tuu ya utalamu. Industry ya technology na sayansi ni kubwa katika nchi hizi. Si maabara tuu, wanatengeneza wenyewe vifaa vya kwenye maabara, wanapublish wenyewe kwa bei nafuu vitabu vya sayansi na wanaandika wenyewe sehemu kubwa ya vitabu hivyo.

Sisi kote huko hatujafikia. Si shule za sekondari tu kukosa walimu wa sayansi, vitabu, maabara ( ndiyo maabara ni muhimu katika kupata uelewa katika nyanja hii), kompyuta hata kwenye vyuo vikuu vyetu hayo matatizo yapo. Hiyo pool ya wataalam wa nuclear science (kuanzia scientists, engineers, fundi wachundo n.k) tutaitoa wapi?
Fundi Mchundo mwenzangu ni lazima unaelewa kuwa the science behind nuclear power sio ngumu kiasi hicho. Ni namna gani unaweza kui'harness' bila kuleta madhara na cha msingi zaidi utakavyoweza kudispose hiyo inayoitwa 'spent fuel'! Huu uwezo hatuna kwa bahati mbaya na kwa hivyo ni foolhardy kuanza kuentertain mawazo kama haya badala ya kuangalia njia mbadala kibao zilizo ndani ya uweza wetu. Wazimbabwe wamepiga hatua katika matumizi ya wind power, Centre for Appropriate Technology wana utaalam wa kutoa umeme kwenye maporomoko yasiyozidi mita moja (ndio, moja), waizraeli wako mbele kwenye matumizi ya sola n.k.

Kwa bahati mbaya hii ni ishara ya the very mind-set unayoipiga vita. Kupenda makubwa badala ya tunavyoviweza. Maprofesa India hawaoni taabu kupanda baiskeli, sisi tunataka SUVs. Uwezo wa kuhudumia hayo mashangingi hatuna lakini bado tumeyang'ang'ania.

Ni vifaru vingapi na magari ya kivita vilivyotengenezwa na Nyumbu? Katika zaidi ya miaka kumi wameweza kutengeneza magari yasiyozidi 26! At what cost? Tumeweza kumuuzia nani? Hizi ndizo sifa zisizo na maana ambazo tunazipenda.

Tuvifanye tunavyoviweza kwanza. Hivyo vingine vitakuja tuu. Tuwekeze kwenye elimu kama walivyofanya wenzetu na haya unayoyataka yatakuja tuu. Tusipende pupa. Tujiulize, kuna nchi kibao zilizotuzidi uwezo lakini hazijajiingiza huko kwa sababu gani? Sio wajinga hao. Alternatives zipo, lakini si hii unayokazania. Itatupa false security ati kwa sababu tuna uranium tusiangalie njia mbadala! Tunajijua.

Mradi wa Nyumbu ni mafanikio. Kazi ya mradi huu ilikuwa ni kufanya research na sio production. Research zao zilionyesha kuwa vitu viko DOABLE.

Waliosoma masuala ya computation theories wanaelewa kuwa abstract machines zilikuwepo kabla ya computers tunazozifahamu. Technology ya DVD ilikuwepo kwenye paper toka 1972 na miaka michache iliyopita ndipo ilipoanza kutumika.

Masuala ya NYUKI au technologia yoyote ambayo iko juu ya uwezo wetu isitufanye tufunge vitabu mpaka pale tutakapokuwa na uwezo. Na hii ndio sera iliyokuwepo kwa matumizi ya TVs na Computers.

Kuhusu wanafunzi wa India au Pakistani, ni GUTS tu kuwa wanaweza. Na hiyo ndio tofauti kubwa kati yao na sisi. Somo kubwa ambalo linaweza kukufanya wewe ufanye vizuri katika university level hata kama shuleni kulikuwa hakuna lab za sayansi ni Mathematics pekee yake. Na hilo ndio tatizo lililopo Tanzanian students can't compute.

World-class scientists wanaotoka India ni matokeo ya programs zao na sio manna kutoka binguni. Kama huna program ya kuwa na wanasayansi basi hutakuwa nao. Tanzania ilikuwa na program ya kuwa na wanasiasa na tunao wa kutupwa.
 
Astoundingly as it may sound what an extraordinary way of cohesion shown by contributors to this thread.

I shall agree with Pedro

Bin Maryam I strongly agree with your views(on this thread), their quite coherent with IDIMI and the rest of the posts on this thread.

Hii mind-set, mind-set, mind-set! (VISION) Inatufaa kwa mambo mengi tu Watanzania.

Mimi nitahitaji strategically thinking people like you for 2025!

Pitiani na hapa basi-Nafikiri itaweza kuondoa woga kidogo.http://www.howstuffworks.com/nuclear-power.htm

2025 mbali sana huyu kada wa chama akiondoka tunataka aliyezaliwa baada ya Azimio la Arusha.
 
Points nzuri,

nafikiri kuna haja ya kujiandaa na the nuclear age.kwa sasa kama ilivyosemwa hapo mwanzo hatuna infrastructure na ku-delve into nuclear itakuwa ni disaster waiting to happen Ikiwa wenzetu walioendelea wana experiences za Manhattan projects na the arms race bado wamepata dhahma za "Three Mile Island" Chernobyl na hata Bhopal ya India, seuze sie wa chemli na vibatari?.

Sasa hivi tunatakiwa tu invest kwenye infrastructure kuanzia elimu mpaka communication networks tukiwa na vision ya kuwa na nuclear energy baada ya miaka 25-50.
 
Mradi wa Nyumbu ni mafanikio. Kazi ya mradi huu ilikuwa ni kufanya research na sio production. Research zao zilionyesha kuwa vitu viko DOABLE.

Hivi umefika Nyumbu, Kibaha au unasimuliwa? Pamoja na kuwa well-intended, mradi wa nyumbu ni failure. Wametengeneza APC ( sidhani kama wametengeneza Tank),gari la zima moto na maarufu zaidi lile lilotumika kuubeba mwili wa Mwalimu (RIP). Baada ya kuona matatizo ndiyo maana wakaelekeza kwenye biashara ya dhahabu na sisi hii tunayosikia ya bio-gas (ambayo carmatec wamejihusisha kwa miaka mingi). Ukiangalia critically, hatuna military industry ya kuweza kusustain mradi kama huu. Wenzetu (wamarekani, warusi, waafrika kusini n.k) wanategemea mauzo ya nje ya bidhaa zao kusustain industry zao. Wengine unaowasikia (India, China n.k.) walianza kubuild under licence. Hakuna mtu anayejisumbua kugundua gurudumu. Sasa sisi tumeshindwa kutengeneza baiskeli( Mwenge) tungeuweza kweli huu mradi?

Waliosoma masuala ya computation theories wanaelewa kuwa abstract machines zilikuwepo kabla ya computers tunazozifahamu. Technology ya DVD ilikuwepo kwenye paper toka 1972 na miaka michache iliyopita ndipo ilipoanza kutumika.

Sasa unachotaka kutuambia kuwa tukitaka kutengeneza DVD na sisi tuanze from scratch? Au twende kwa hao wenye hiyo teknoloji na tuitumie?

Masuala ya NYUKI au technologia yoyote ambayo iko juu ya uwezo wetu isitufanye tufunge vitabu mpaka pale tutakapokuwa na uwezo. Na hii ndio sera iliyokuwepo kwa matumizi ya TVs na Computers.

Hivi kwa sababu tuna vijana wana uwezo wa kuassemble kompyutas na sisi tujione magwiji kwenye hii industry? Sera ya kupinga na kuzuia TVs na Kompyuta ilikuwa based kwenye uwezo wa watu kununua na siyo kama tunaviweza kiteknoloji. Sasa vipo, vimeruhusiwa na vimejaa bwelele tuko wapi kwenye kuelekea kuviunda pale nyumbani?

Kuhusu wanafunzi wa India au Pakistani, ni GUTS tu kuwa wanaweza. Na hiyo ndio tofauti kubwa kati yao na sisi. Somo kubwa ambalo linaweza kukufanya wewe ufanye vizuri katika university level hata kama shuleni kulikuwa hakuna lab za sayansi ni Mathematics pekee yake. Na hilo ndio tatizo lililopo Tanzanian students can't compute.

Again, unaspin. Unataka kuniambia seriously kuwa hatuhitaji maabara katika shule zetu za sekondari? Hao physicists unaowataka watatokea wapi? Unarudia makosa yaleyale tuliyoyafanya kusisitiza kuwa Kiswahili na Siasa ndiyo basis ya elimu yetu. Tunahitaji maabara ili vijana waanze mazoea ya kutafiti. Haitoshi kugugl peke yake. Wahindi, wapakistani na wengine wali invest kwenye basic education kwanza. Hawakuanza na nuclear physics primary school. Mfundishe mwanafunzi kupenda elimu, kumdadisi na mchunguzi na mengine yatafuata.

World-class scientists wanaotoka India ni matokeo ya programs zao na sio manna kutoka binguni. Kama huna program ya kuwa na wanasayansi basi hutakuwa nao. Tanzania ilikuwa na program ya kuwa na wanasiasa na tunao wa kutupwa.

Tanzania ina kitengo cha masuala ya atomic. Tanzania ina physicists wazuri tuu. Hawa wote wanaweza kuelekeza nguvu zao kwenye hiki unachokitaka. Reality, however, ni kuwa kama tutahitaji tutanunua utaalam kutoka wenye nao na hatuta anza kwenye basics. Wairan imebidi wafanye hivyo kwa sababu soko limefungwa kwao. Tusikazanie hii mind-set ya kupenda SUVs wakati uwezo wetu ni baiskeli, kusafiri First Class wakati uwezo wetu ni kwenda economy. Tupange priorities zetu na yote haya tutayapata. Sio kesho lakini hatimaye tutayapata. Kwa kuzania huku unakotaka tunapunguza resources kwenye sehemu zenye umuhimu zaidi. Na mwisho, sidhani ulikuwa serious kwenye jibu lako kuhusu Calories. Au ulikuwa?
 
Raisi mstaafu wa msumbiji alisema "Poverty is a state of mind" hivi kweli mtz anajiona mnyonge kwa mpakistani??!!!!!!
 
Raisi mstaafu wa msumbiji alisema "Poverty is a state of mind" hivi kweli mtz anajiona mnyonge kwa mpakistani??!!!!!!

Wakati Gold Coast inapata uhuru uchumi wake ulikuwa umeuzidi wa Indonesia kwa mbali. Leo Indonesia uchumi wake unashindana na ule wa nchi zote za Afrika chini ya Sahara ukiondoa Afrika kusini! Tulipopata uhuru tulikuwa tunasikia njaa na adha ya umasikini kule India na Pakistan na baadaye Bandgladesh. Leo waafrika tumekuwa ndiyo mfano wa umaskini ukiokithiri. Kwa maneno mengine tumekuwa poster child wa umasikini. Ukweli ni kuwa nchi zote hizi zimetuzidi. Tunachotakiwa kufanya ni kujiuliza kwa nini imekuwa hivyo na kuhakikisha kuwa tunatoka hapa tulipo. Kukazania false feelings of grandeur hakutufikishi mbali. Singapore walipopata uhuru walikuwa maskini wa kutupwa. Hawakupinga hilo bali walikataa kubaki pale. Leo tunaona walipo. Hatutaweza kujikomboa bila kukubali hali halisi iliyopo. Tufanye hivyo kwanza halafu tupange namna ya kujitoa. Sijisikii mnyonge kwa mpakistani ila nakasirika kuwa ameweza kutupita na nitafanya kila jitihada watoto wangu wasiwe ndio poster children wa Oxfam!
 
Nikiongezea, India walianza na Bajaj ambayo walichukua utaalam kutoka Vespa. Wakaja na Maruti ambayo walitoa utaalam kutoka Suzuki. Wakati huo walikuwa na homegrown vehices kama Ambasador na Premium lakini waliona wamefika tamati ya ujuzi wao. Leo Tata wanataka kununua Jaguar na Landrover kutoka Ford! Hawakurupuka na kutaka kuanza kuunda Rolls Royce. Wachina walianza na baiskeli, vyerehani n.k. Wote hawa wameweza kutoka hapo walipoanzia. Na sisi tunaweza tukipanga priorities zetu inavyopaswa.
 
Tanzania tulianza na Diesel power, then Hydro power, sasa tuko Gas power, baadae thermo power, sasa tukitoka hapo tuende wapi sasa? yaani turudi tena soler energy!
 
Tanzania tulianza na Diesel power, then Hydro power, sasa tuko Gas power, baadae thermo power, sasa tukitoka hapo tuende wapi sasa? yaani turudi tena soler energy!

Hivi unaona kwenda kwenye sola ni kurudi nyuma? Kwa taarifa yako hii ndiyo cutting-edge technology sasa hivi. Zote hizo ulizozitaja hatujazi-exhaust. Tunahitaji kuongeza ufanisi katika matumizi yetu ya umeme. Tupunguze transmission losses, end-user losses n.k. Badaa ya kumchemshia maji umeme, kukausha bidhaa tutumie sola. Kwenye vijiji na miji midogo badala ya kungojea umeme wa grid tuangalie uwezekano wa kuzalisha kutumia bio, wood chips, maporomoko madogo n.k.Tutumie sola, upepo kupump maji, kusaga nafaka n.k. Tuhakikishe maofisi yetu, nyumba zetu zinajengwa kitaalamu kutumia mwanga wa jua na joto lake pale inapohitajika. Sehemu za pwani tutumie upepo kupooza nyumba zetu na kupunguza matumizi ya viyoyozi. Sehemu za rift valley tuangalie uwezekano wa kuzalisha umeme kutoka geo-thermal. Tuhakikishe bidhaa zinazoingizwa nchini zinatumia umeme kwa ufanisi mkubwa. Kwenye majengo ya serikali tudai energy auditing na yale yanayojengwa ziwepo standards za matumizi ya umeme. Wenye viwanda na mashamba waangalie uwezekano wa kugenerate umeme kutokana na by-products zao, k.m. kwenye mashamba ya miwa kuna kitwa kinaitwa bagasse (brazil wako mbali kwenye hili). Haya yote na zaidi yanawezekana bila kukimbilia nyuklia. Nyuklia ni kama bling kwetu sisi. Kuwa na meno yaliyojaa almasi hakujawahi kumsaidia mtu! Na mimi ni Fundi Mchundo tuu, je wataalamu walio bobea si watajua zaidi?
 
Na kwa wale wanaoona nyuklia peke yake ndiyo jawabu,

Brazil’s 29-year-old ethanol fuel program uses cheap sugar cane, mainly bagasse (cane-waste) for process heat and power, and modern equipment, and provides a ~22% ethanol blend used nationwide, plus 100% hydrous ethanol for four million cars. The Brazilian ethanol program provided nearly 700,000 jobs in 2003, and cut 1975–2002 oil imports by a cumulative undiscounted total of US$50 billion.[1] Today, Brazil gets more than 30% of its automobile fuels from sugar cane-based ethanol.[2]

Hiyo ya juu ni kutoka wikipedia.

Kutoka miwa, tunawaridhisha wanyakyusa na wapemba, tunapata ethanol ya kuendesha ma SUV yetu na tunatoa umeme! Wenye teknoloji wote ni washikaji ( Brazil, Cuba etc) hatugombani na mtu ati tunataka kutengeneza mabomu na tunatunza mazingira kwa kutumia waste kutoka miwa. Bado mnataka tutoe kipaumbele kwa nyuklia!
 
Asante fundi kwa mawazo mapana, nadhani hii yote ni micro energy, tz tunategemea kiwanda kikubwa wa chuma pale liganga, migodi mikubwa ya platinam kule rukwa na ruvuma, bado bati kagera na kigoma. viwanda vikubwa vya saruji mwanza na shinyanga. hivi vyote haviwezi kutegemea solar wala ethanol. uranium iko tele tu dodoma wala hatu-import kunaubaya gani tukiikodolea macho!
 
Points nzuri,

nafikiri kuna haja ya kujiandaa na the nuclear age.kwa sasa kama ilivyosemwa hapo mwanzo hatuna infrastructure na ku-delve into nuclear itakuwa ni disaster waiting to happen Ikiwa wenzetu walioendelea wana experiences za Manhattan projects na the arms race bado wamepata dhahma za "Three Mile Island" Chernobyl na hata Bhopal ya India, seuze sie wa chemli na vibatari?.

Sasa hivi tunatakiwa tu invest kwenye infrastructure kuanzia elimu mpaka communication networks tukiwa na vision ya kuwa na nuclear energy baada ya miaka 25-50.

Pundit:

Hicho ndicho kitu cha msingi. Nchi yetu na watu wetu wengi bado wana fikra za mabadiliko za kimapinduzi yenye kufanana na eletric switch.

Mabadiliko ya maendeleo hayatokei kama tunawasha na kuzima umeme. Gradually kitu kimoja kinapotea au kupungua mahitaji yake na kitu kingine kinaingia au kuongezeka matumizi yake. Lazima tuwe na mabadiliko yenye transition.

Tunaoona uwezekano wa matumizi ya Nyuki Tanzania, tunakubali kuwa tunahitaji wakati na kwamba haya mambo yanawezekana. Na wakati tunaohitaji sio wa kutumia resources zingine kwanza kama wachangiaji wengine wanavyodai. Hiyo dhana ilipitwa na wakati. Miaka 120 iliyopita kulikuwa hakuna hospitali Tanzania na tulikuwa tunategemea mitishamba. Hata siku moja hatukusema kuwa tutaanza kutumia madawa ya hospitalini pale tutakapoishiwa na mizizi.

Hivyo basi wakati tunaohitaji kabla ya kutumia nguvu za NYUKI ni kujifunza, kubalidisha tabia zetu katika uendeshaji wa shughuli muhimu na mambo mengine. Suala la kujifunza linaweza kuanza hata sasa.
 
Bin umegusa katikati ya ubongo wangu, watz tufikirie pia 20yrs 30yrs na hata 100yrs tz itakuwa wapi? EU wameanzisha vision 2100 plan! mchakato wa machimbo ya dhahabu ulianza 20yrs ago enzi ya tume ya Paul Bomani (tume ya Bomani) leo ndo tunavuna either mbivu au mbichi! unatakiwa usiwaze maisha yako tu waza pia na mjukuu wako atasoma vipi?
 
Hivi umefika Nyumbu, Kibaha au unasimuliwa? Pamoja na kuwa well-intended, mradi wa nyumbu ni failure. Wametengeneza APC ( sidhani kama wametengeneza Tank),gari la zima moto na maarufu zaidi lile lilotumika kuubeba mwili wa Mwalimu (RIP). Baada ya kuona matatizo ndiyo maana wakaelekeza kwenye biashara ya dhahabu na sisi hii tunayosikia ya bio-gas (ambayo carmatec wamejihusisha kwa miaka mingi). Ukiangalia critically, hatuna military industry ya kuweza kusustain mradi kama huu. Wenzetu (wamarekani, warusi, waafrika kusini n.k) wanategemea mauzo ya nje ya bidhaa zao kusustain industry zao. Wengine unaowasikia (India, China n.k.) walianza kubuild under licence. Hakuna mtu anayejisumbua kugundua gurudumu. Sasa sisi tumeshindwa kutengeneza baiskeli( Mwenge) tungeuweza kweli huu mradi?

Sasa unachotaka kutuambia kuwa tukitaka kutengeneza DVD na sisi tuanze from scratch? Au twende kwa hao wenye hiyo teknoloji na tuitumie?

Hivi kwa sababu tuna vijana wana uwezo wa kuassemble kompyutas na sisi tujione magwiji kwenye hii industry? Sera ya kupinga na kuzuia TVs na Kompyuta ilikuwa based kwenye uwezo wa watu kununua na siyo kama tunaviweza kiteknoloji. Sasa vipo, vimeruhusiwa na vimejaa bwelele tuko wapi kwenye kuelekea kuviunda pale nyumbani?

Again, unaspin. Unataka kuniambia seriously kuwa hatuhitaji maabara katika shule zetu za sekondari? Hao physicists unaowataka watatokea wapi? Unarudia makosa yaleyale tuliyoyafanya kusisitiza kuwa Kiswahili na Siasa ndiyo basis ya elimu yetu. Tunahitaji maabara ili vijana waanze mazoea ya kutafiti. Haitoshi kugugl peke yake. Wahindi, wapakistani na wengine wali invest kwenye basic education kwanza. Hawakuanza na nuclear physics primary school. Mfundishe mwanafunzi kupenda elimu, kumdadisi na mchunguzi na mengine yatafuata.

Tanzania ina kitengo cha masuala ya atomic. Tanzania ina physicists wazuri tuu. Hawa wote wanaweza kuelekeza nguvu zao kwenye hiki unachokitaka. Reality, however, ni kuwa kama tutahitaji tutanunua utaalam kutoka wenye nao na hatuta anza kwenye basics. Wairan imebidi wafanye hivyo kwa sababu soko limefungwa kwao. Tusikazanie hii mind-set ya kupenda SUVs wakati uwezo wetu ni baiskeli, kusafiri First Class wakati uwezo wetu ni kwenda economy. Tupange priorities zetu na yote haya tutayapata. Sio kesho lakini hatimaye tutayapata. Kwa kuzania huku unakotaka tunapunguza resources kwenye sehemu zenye umuhimu zaidi. Na mwisho, sidhani ulikuwa serious kwenye jibu lako kuhusu Calories. Au ulikuwa?

Nyumbu nimepita lakini kuna washikaji kutoka Mchundo walifanya kazi pale. Hivyo stori nyingi ninazo. Hata Nyumbu nao walifanya kama walivyofanya wengine watu wengine (under licence). Injini za mwanzo zilikuwa kutoka ujerumani mashariki kama sikosehi. Hawakufanya vitu vyote kutoka mwanzo.

Failure ya Nyumbu haitokani na matatizo ya kiufundi. Inatokana na Business Model waliyofuata, ndio maana naupenda UBEPARI. Kwa bahati nzuri nimeishi nchi za Ulaya mashariki. Na matatizo yaliyoikumba Nyumbu ni matatizo yaliovikumba viwanda vingi katika nchi za Ulaya mashariki.

Nyumbu haikuwa na Business Model yoyote hili. Misheni yao ilikuwa ni kutengeneza magari na vifaru na waliweza kufanya hivyo. Na hawakuwa na misheni ya kutengeneza gari na vifaru vya kuuza. Unapotoa maamuzi ya kutengeneza kitu kwa ajili ya kuuza, unaangalia masoko kwanza.

Katika university ranking, wa-marekani wanaongoza vizuri sana katika masuala ya Business Admin. Financial na Marketing. Technologia yoyote haiwezi kuuzwa na kuleta faida kama haitakuwa na watu wazuri wenye Acumen ya Business Admin. Financial na Marketing.

Hata kama Tanzania ina physicists, engineers wazuri lakini wakakosekana watu wazuri wenye ujuzi mzuri katika Business Admin. Financial na Marketing, ambao wanaweza ku-glue kile physicists na engineers wanachoweza kukifanya hakutakuwa na maendeleo yoyote.

Kama nitakuwa sijavuka mipaka na kuingilia taaluma za watu wengine, VALUE ni thamani ya kitu ambacho mteja yupo tayari kulipa. Hivyo unapofanya biashara ya aina yoyote nia yako kuweka VALUE ya huduma au vitu unavyoouza inayoweza kuwafanya wateja wanunue. Kwa mtaji huu nchi ulizotaja (wamarekani, warusi, waafrika kusini n.k) hawategemei mauzo ya nje ya bidhaa zao kusustain industry zao. Wanachotegemea ni VALUE gani iliyopo katika bidhaa zao itakayomfanya mteja kununua bidhaa hizo. Wateja wa nje wana-choice ya kununua bidhaa kutoka nchi mbalimbali. Lakini factor wanazoangalia wateja ni bei, ubora, support n.k.

Tukurudi kwenye mada, NYUKI ya Iran imeanza toka Shah akiwa madarakani. Wa-iran wa utaifa kuzidi udini. Hivyo program za taifa bado zinaendelea japokuwa madaraka yamebadilika.

Wako katika ujenzi wa taifa.

BM
 
Nikiongezea, India walianza na Bajaj ambayo walichukua utaalam kutoka Vespa. Wakaja na Maruti ambayo walitoa utaalam kutoka Suzuki. Wakati huo walikuwa na homegrown vehices kama Ambasador na Premium lakini waliona wamefika tamati ya ujuzi wao. Leo Tata wanataka kununua Jaguar na Landrover kutoka Ford! Hawakurupuka na kutaka kuanza kuunda Rolls Royce. Wachina walianza na baiskeli, vyerehani n.k. Wote hawa wameweza kutoka hapo walipoanzia. Na sisi tunaweza tukipanga priorities zetu inavyopaswa.

Hakuna mtu anayesema Tanzania tuanze upya. Magari unayoona sasa msingi wake ni magari ya kuvutwa na wanyama yaliotengenezwa miaka zaidi ya 3000 iliyopita.
 
Asante fundi kwa mawazo mapana, nadhani hii yote ni micro energy, tz tunategemea kiwanda kikubwa wa chuma pale liganga, migodi mikubwa ya platinam kule rukwa na ruvuma, bado bati kagera na kigoma. viwanda vikubwa vya saruji mwanza na shinyanga. hivi vyote haviwezi kutegemea solar wala ethanol. uranium iko tele tu dodoma wala hatu-import kunaubaya gani tukiikodolea macho!

Eddy:

Wanachotaka ni kushimba uranium na kuuza.
 
Hivi unaona kwenda kwenye sola ni kurudi nyuma? Kwa taarifa yako hii ndiyo cutting-edge technology sasa hivi. Zote hizo ulizozitaja hatujazi-exhaust. Tunahitaji kuongeza ufanisi katika matumizi yetu ya umeme. Tupunguze transmission losses, end-user losses n.k. Badaa ya kumchemshia maji umeme, kukausha bidhaa tutumie sola. Kwenye vijiji na miji midogo badala ya kungojea umeme wa grid tuangalie uwezekano wa kuzalisha kutumia bio, wood chips, maporomoko madogo n.k.Tutumie sola, upepo kupump maji, kusaga nafaka n.k. Tuhakikishe maofisi yetu, nyumba zetu zinajengwa kitaalamu kutumia mwanga wa jua na joto lake pale inapohitajika. Sehemu za pwani tutumie upepo kupooza nyumba zetu na kupunguza matumizi ya viyoyozi. Sehemu za rift valley tuangalie uwezekano wa kuzalisha umeme kutoka geo-thermal. Tuhakikishe bidhaa zinazoingizwa nchini zinatumia umeme kwa ufanisi mkubwa. Kwenye majengo ya serikali tudai energy auditing na yale yanayojengwa ziwepo standards za matumizi ya umeme. Wenye viwanda na mashamba waangalie uwezekano wa kugenerate umeme kutokana na by-products zao, k.m. kwenye mashamba ya miwa kuna kitwa kinaitwa bagasse (brazil wako mbali kwenye hili). Haya yote na zaidi yanawezekana bila kukimbilia nyuklia. Nyuklia ni kama bling kwetu sisi. Kuwa na meno yaliyojaa almasi hakujawahi kumsaidia mtu! Na mimi ni Fundi Mchundo tuu, je wataalamu walio bobea si watajua zaidi?

Fundi Mchundo:

Nakushangaa sana unaposema pwani watumie hiki, vijijini watumie kile. Je ni nani atakusaidia katika mambo hayo? Je ni kila siku tununue hivyo vitu bila ya kuwa na wataalamu wenye kuelewa hivyo vitu?

Ukikubaliana na mimi kuwa tunahitaji watu wa kuelewa siri ya teknologia hizi, basi NYUKI hatakuwa mbali sana nasi.

Katika hoja yako moja umezungumza masuala ya computer nilipoeleza mambo ya DVD. Samahani ukunielewa. DVD ina kama sehemu mbili muhimu, sehemu ya kwanza ni ya mathematics (Data compression) na sehemu ya pili ni media (laser disk) ambayo inaweza kustore data. Sehemu ya kwanza ya mathematics ilishagunduliwa zamani lakini ilisubiri laser technology. Hivyo sikuzungumzia masuala ya computer repair kwani ayefaidika zaidi kwenye biashara ya computer ni mwenye intellectual property, kutengeneza chip au mwenye ku-develop software.

Kama vile mathematics part ya DVD ilisubiri kwa muda mrefu maendeleo katika masuala ya laser technology, amini usiamni watu wanalifanyia kazi usiku na mchana usalama wa NYUKI.
 
Back
Top Bottom