Elections 2010 URAMBO: Jeshi la wanyama pori laua wapinzani 25

suala ni hili,kwanini wahalifu wapigwe bunduki? askari wetu wanapiga bunduki wananchi wetu ili kulinda wanyama?kwanini wasikamatwe na kupelekwa mahakamani? kama wamefanya hili, hakika yake Mungu na awalipe waaibike na Mungu atukomboe watz toka kwenye selikali ya aina hii. kwa wale msiojua, mimi nimezaliwa na kukulia eneo ambalo badaye lilikuja kuwa declared kuwa mbuga ya wanyama, huwa kuna kuwa na manyanyaso ya ajabu, binadamu wananyimbwa ardhi ili wanyama wakae vizuri.
 
Naaam sasa mmeona eee. sehemu ya jeshi imeanza kutekeleza kazi iliyopangwa ila wameanza mapema mno. Wamewaua watanzania wenzetu kibudu, tena wanawasingizia uhalifu kabla hakimu hajasoma hukumu.
Niliwaambia kwamba hata kwa damu kumwagika lazima CCM itajiimarisha madarakani
WAPO RADHI KUMWAGA DAMU YA WATANZANIA ILI WATANZANIA WAWAPE RIDHAA NYINGINE YA MUHULA.

Jamani are we going to be silent on this??????? Hell me!!
 
Katika taarifa ya habari ya itv jana usiku, prof. Lipumba alitoa habari hizo. Ufuatiliaji unahitajika. lakini hata kama wamevamia, si washitakiwe? Kwanini wauawe kwa risasi?

huo ni utulivu na amani wa tanzania
 
Kuna habari Zimenifikia hivi punde kutoka urambo tabora kuwa jeshi la wanyama pori
Urambo, Tabora limechoma nyumba za kijiji kimoja na kuua watu 25 kwa kuwasingizia
kua ni Majambazi.
Watu hao ambao inasemekana ni wafuasi wa CUF na wapinzani wakubwa wa CCM
Walizushiwa kuwa wamevamia Eneo la wanyama pori na baadae nyumba zao kuchomwa
moto. Baada ya watu kuhoji kuwa watu wale walikuwapo hapo kwa mda mrefu na si wavamizi, Askari wale waliamua kuwaua.
Mwenye kina tunaomba atujuze zaidi.
Shimbo yuko wapi???
 
Wakuu naomba uhakika wa hii ishu maana naona kuna mixed message here.
Hapa tuweke siasa pembeni tuingie kama watu wenye utu kwa ajili ya watu.
Tupate clues za uhakika maana tumeanza kuhuzunika na kuanza kusahau kwamba waliokumbwa na hiyo zahama ni watu ambao walipaswa kuwa hai muda huu.
je ni kweli wameuliwa au kuna any updates? maana nasikia polisi walikanusha na mkuu wa mkoa alikanusha. Kuna wenzetu walioko urambo pls tuleteeni ishu na kama akipatikana mmoja wa waathirika wa hilo tupate take yake please. Ninaposema waathirika kama kuna majeruhi, ndugu wa marehemu au kama dokta mkuu ambapo maiti zimehifadhiwa ili tujue nini kinachoendelea kabla hatujaanza kuingia undani wa hili.

Let us love Tanzania na watu wake just once. Tusiwaue wahalifu, tuwafikishe wahalifu mahali kunakohusika, tutoe ushirikiano na vyombo vya dola tunapopeleka mashtaka ili kama haki haitendeki tupate pa kuanzia.
 
yale yale ya ditopile na zombe,inchi hii haina utawala wa sheria kama wanavyodai
 
@ Msanii.
Kuhusu Clues, Sote Hatukua Eneo la tukio hivyo ningeomba unisamehe kwa hilo. Tungoje asasi za kiraia kama zitakua interested
juu ya swala hili maana sasa kila kitu ni kwa maslahi zaidi. Usidhani labda naleta Utani juu ya swala hili, hadi sasa Sina amani juu
ya hili.
Kama ni kweli, safari hii damu ikimwagika nadhani itaanza yangu. -Shimbo ujue hilo.
 
Back
Top Bottom