Uwezo Tunao
JF-Expert Member
- Nov 14, 2010
- 6,942
- 1,190
... mtoto acha kupiga mayowe, siku ya siku itakapofika utaona sisi waheshimiwa wapiga kura tukijiamulia wenyewe tena bila papara wala fungu la mafisadi hapa.
Huyu Mchange jina lake liliondolewa kugombea uenyekiti Bavicha alipokamatwa akigawa rushwa kama njugu kupitia mtandao.
Pia huyu ndiye mara nyingi kwa kutumia facebook akishirikiana na mtu anayejiita Said Kulwa na Juliana Shonza wamekuwa wakiwatukana matusi ya nguoni viongozi wakuu wa chama Dr Slaa,Freeman Mbowe na John Heche.Matusi wanayotukana hayandikiku
Makundi ndani Chadema ndio kwanza yanaanza, Chadema Kaskazini povu linawatoka.
fmpiganaji Katiba itakamilika mapema 2 na itamruhusu ZITTO kugombea. Hata kama itakuwa bado na kama ambavyo tumesikia hata lile jukwaa la CHADEMA linavyolumbana na kamati ya maoni ya Katiba mpya , lazima tu uchaguzi wa 2015 utaongozwa na sheria mpya aidha kutokana na Katiba mpya au kwa kufanyia marekebisho baadhi ya vipengele na nadhana kipengele cha umri kitakuwa kimojawapo.
Yap,na hiyo ndo sababu ya jina lake kuondolewa kwny kinyang'anyiro hicho!but it seems bado ana hasira...trust me,zzk hatagombea urais kupitia cdm labda kupitia chama kingine!na mchange ulijue hili,endeleeni kupiga kelele weee,cdm ni taasisi sio zzk
Wanaodhani wengine tunaipenda tu Chadema (kama makada wa CCM walivyo) wanakosea sana,akina Habib Mchange ni mmojawapo wa watu wanaodhani Chadema imefika hapo pa kupendwa tu.
Sina muda wa kujadili hoja zake dhaifu lakini namtahadharisha kuwa Watanzania tunataka mabadiliko kwa namna yeyote,Watanzania watampa nafasi yule waliyenae mtaani kila siku akiwatetea kwa moyo mmoja bila hila,Watanzania wanataka mtu safi na kiongozi aliyekomaa kwelikweli na amedhihirisha hivyo kwa vitendo na si kwa simulizi zake kutuambia aliyofanya kama vile sisi ni vipofu!
Hawa akina Mchange wasameheni tu ni vijana wadogo wanaodhani wameshakomaa kisiasa na sifa zinawaharibu sana.Someni makala hiyo muone kama kuna kijana aliyeiva hapo!!!
yeye na mwezake nyakanguru ndio vibaraka wakubwa baada ya kushndwa kupenya bavichaamekuwa watu wa majungu
Watu wenye upeo finyu huishia kujadili watu badala ya kujadli masuala! kwa siasa hizi nyepesi nyepesi za kunadi watu kwa ajili ya kupata mkate wa siku (kumtumikia kafiri ili upate mradi wako!) ndio maana hata vyama vya upinzani havifanikiwi! upuuzi huu wa kumnadi mgombea (wakati hakuna uchaguzi sasa) badala ya kueneza sera za chama zieleweke hauwezi kututoa hapa tulipo! Ndugu mchange kama unataka chama chako kifanikiwe na huyo mgombea wako apite 2015 shiriki katika kampeni ya kunadi sera na kukitangaza kwa wananchi, ACHANA NA SIASA ZA VISASI!
Hata mimi sielewi. Wanajaza nafasi humu JF.Hiyo habari inahusu nini?,,,, nna mambo mengi ya kufanya.