rangirangi
Member
- Jan 11, 2015
- 33
- 4
Jamaaa anafaaaa
Siku moja tukiwa kwenye Fast Jet tukielekea Dar kutokea Mwanza ulizuka mjadala kuhusu Tundu Lissu kwamba mwanasheria huyu maarufu ndiye mwanasiasa anayekuja kwa kasi na hana kashifa yoyote na mzalendo asiyeigiza. Watu walitoa sifa nyingi sana mpaka pale nilipochomeka swali kwamba je wanadhani anafaa kugombea kuongoza nchi hii? Majibu yalikuwa tofauti na kuliibuka mjadala upya.
Wapo waliodhani Lissu anafaa kuwa waziri mkuu ili aongoze utendaji wa serikali na kwamba tutakuwa tumepata Sokoine mpya, wapo waliosema anafaa kuwa rais na Tanzania itakuwa imempata Micheal Satta wake, wapo waliosema Lissu ni mkali sana na akiwa rais tutashudia dhahama ya watu kufungwa na amri za kama za kijeshi. Sisi tulishindwa kupata majibu maana tulifika mwisho wa safari mjadala ukiwa unaendelea na kabla ya kupata majibu.
Lete mtazamo wako hapa jukwaani.
Tatizo Dr hawezi kushinda hata kama CHADEMA na CUF wanaungana kwa jina la UKAWA.DR SLAA hatapata kura za wafuasi wa CUF na sababu inafahamika.CHADEMA msifanye hili kosaKwa mtazamo wangu mi naona lisu anafaa kuwa waziri mkuu na dr awe rais
. Ila huko mbeleni anaweza pewa huo wadhifa
mkuu mapuma miyoga, taasisi ya presidency nionavyo mimi ni complex sana. Unahitaji mtu mwenye multiple gifts katika hulka yake kwa maana ya proficiency ambayo ni multidisciplinary. A good orator, pasipo genius katika maeneo mengine unapata rais mbaya. Tundu lisu is a good orator, he is a good legal person. Tunahitaji muda kujua quality zake nyingine kabla ya kumu-endorse for president.
Nafasi ya waziri wa sheria anapita bila kupinga. Kwa hiyo tuombe mungu idadi ya wabunge ivuke nusu ya wabunge wanaotakiwa bungeni, na dr. Slaa au mtu mwingine katika chadema apate ushindi kwenye nafasi ya rais. Tundu lisu should fit squarely kwenye nafasi ya waziri fulani bila kupingwa--hasa hasa nafasi ya sheria. But president? Tunahitaji muda zaidi kumsoma....
Lowassa hawezi kusimama kwenye jukwaa hata kwa dakika 40..hizo kampeni labda apige akiwa kwenye dripu