Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,547
- 41,060
Kinana amesema uwongo kuwa eti CCM imekuwa na utaratibu wa kutoruhusu kuwepo na ushindani ndani ya CCM wa kumpata mgombea wa chama kwenye kiti cha Urais pale ambapo Rais aliyepo madarakani hajamaliza vipindi viwili vya Urais wake. Amesema hayo akimlenga Rais wa Sasa.
Uwongo wa Kinana upo katika ukweli ufuatao:
1. Huko nyuma hakujawahi kuwa na Rais wa kipindi cha dharula. Hivyo hakujawahi kuwa na desturi ya kumpitisha Rais wa Dharula bila ya kura za wajumbe wa vikao vikuu vitatu vya CCM. Kifo cha Rais Magufuli ndiyo ilikuwa dharula ya kwanza kwa Taifa.
2. Rais wa sasa hakuwahi kupigiwa kura na wajumbe wa Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu kuwa mgombea wa CCM kwenye kiti cha Urais. Utamaduni anaousema ni kwa Rais aliyepo madarkani ambaye kipindi chake cha kwanza cha Urais alichaguliwa na vikao vilivyotajwa kuwa mgombea wa Urais kupitia CCM. Lakini siyo kwa mtu ambaye hajawahi kupigiwa kura hata moja na wajumbe wa vikao hivyo kwa nafasi ya Urais.
3. Rais wa sasa ni Rais wa dharula. Katiba, kwa kuzingatia ukweli kuwa nchi isiingie kwenye mkanganyiko pale inapotokea dharula ya kifo cha Rais akiwa madarkani, ndiyo inayotamka ni nani awe Rais wa dharula katika kipindi hicho cha dharula. Huyu anakuwa Rais wa dharula mpaka wakati ule ambapo chama kitampata mtu ambaye vikao vya chama vitamchagua mtu ambaye wanataka awe ngombea wa Urais kupitia chama chao. Kulazimisha Rais wa dharula, ambaye hakuna uhakika kama chama kinaridhika awe mgombea wao kwa nafasi ya Urais, ni kukiuka misingi mikuu ya demokrasia.
Kwenye nchi zenye watu wenye akili timamu, ambako viongozi nao wana akili timamu, siku zote viongozi hutafuta uhakika wa kutaka kujua kama watu wanaotaka wawaongoze wanataka waongozwe na viongozi husika. Watawala wanapojua kuwa wananchi wao wanawataka wawaongoze, inawapa nguvu viongozi katika utendaji wao wa kazi kwa sababu wanatambua kuwa nyuma yao kuna umma mkubwa wa watu unaowataka wao viongozi wawe mbele yao katika utendaji wao wa kuyaongoza mataifa yao. Huku kwetu, sijui ni ujinga, upunguani au ushetani, watawala wanaogopa wananchi kuwadhihirishia viongozi kama wanawataka wawe viongozi wao au la. Ndiyo maana akina Kinana wanatamka wazi kuwa ndani ya CCM hakutakuwa na nafasi kwa wanaCCM kuthibitisha kama wanataka aliyekuwa Rais wa dharula, sasa awe Rais wa kuchaguliwa au apumzike na kupewa heshima yake ya kuiongoza nchi katika kipindi cha dharula.